jmushi1
Platinum Member
- Nov 2, 2007
- 26,394
- 25,520
- Thread starter
- #41
Mkuu nadhani kuna namna inatakiwa tuangalie issue hii kwa jicho la tatu.Muanzisha hii thread leo kaja na maada eti 'Lowassa angekuwa rais bora kabisa kuliko Magufuli'
muwe mnasimamia maamuzi na mitazamo yenu, mnakuwa na thamani zaidi
Fisadi anabaki kuwa fisadi haijalishi kaenda chama gani, yuko nje au jela, kama kaokoka na kujifanya malaika au la!!!
Fisadi ni identity hatakasikiki, wala kuosheka...wakiishafanya ufisadi kuna watu wanakufa kwa namna mbalimbali directly au indirectly! you can not reverse the damage done
Hata fisadi akaongea maneno matamu namna gani, au akaenda kukaa na watakatifu wa chadema! hata hawa watakatifu waliomuita kuja kunajisi ukuu wao bado haitamfanya fisadi kutakata!!
Vyama au mahali anapoenda na anapohamia havina mechanism ya kubadilisha moyo, damu na akili yake asiwe fisadi!
Lowassa ni fisadi sawa na walioko ccm, ambao for years wamejiwekea misingi ya unyonyaji, kuwa na biashara nzito na hawakutumika
Infact kisiasa Lowasa ni chadema, mirija, moyo na base zake zote za kupata hela ziko CCM inajulikana,
Lowasa na hao akina kikwete, mkapa, mwinyi , karamagi n.k wana biashara mbalimbali ambazo wako share
Leo anapokuja mwanachadema anatoa povu kana kwamba Lowasa alikufa akafufuka na akasahau na kuacha mambo yake ya kale unamwonea huruma!!
anapokuja ny.umb.u mmoja na kusema mbona hauyuko gerezani unacheka, kwani nani aliyesema ccm wasafi? hawa wote lao moja!!!!
endeleeni kusaga lami na ndala zenu zilizoisha
Lowasa kuwa Fisadi ni SI Unit, ni kama kuku KFC, au football barcelona, ni sawa na dhahabu barrick au ubongo wa lissu na sheria, Lowasa na ufisadi ni inseparable!!
Mengine yote semeni ila mtu huyu anapendeza sana kwa ID yake ya fisadi, imemvaa
Kwanza utambuwe kuwa hizo kashfa zilitoka ndani ya serikali kwa wana ccm wenyewe.
Kwa mantiki hiyo, kuna mawili
1) waliowapa siri chadema wana malengo yao binafsi na ya kisiasa. Nina imani kwamba vita ndani ya ccm ndo inapelekea hizo siri kuvuja. Na wanaozivujisha, pengine wakiwa na malengo ya binafsi ya kisiasa nk.
2) Kwamba walivujisha siri kwasababu ya uzalendo. Hii pointi nina mashaka nayo sana. Kwasababu kama bado wamo humo humo, hawataki kutoka, zaidi zaidi wanazidi kuji position kwa madaraka zaidi, ulaji nk, basi nasita kusema ni uzalendo. Naona kama ni malengo binafsi zaidi na ya kisiasa.
Hilo nimegunduwa kwasababu hadi sasa yule aliyekuwa akipigiwa makelele kama fisadi mkuu, hayuko kwenye kashfa kuu za kifisadi. Hapo unaweza kuona pengine wapiga kelele wale walikuwa wanataka wawachafue baadhi ya wanasiasa wanaowaona ni kizingiti kwa malengo yao binafsi ya kifisadi pamoja na yale ya kisiasa.
Inawezekana kabisa hao watu waliwaingiza chaka chadema. Hilo sikatai.
Lakini kitendo cha Lowassa kuondoka ccm, kinaoyesha wanafiki na walafi na waoga wakabaki ccm. Mkuu kitendo cha kuwa upinzani siyo kizuri kwa maslahi binafasi ya mtu.
Kwahiyo chadema kumpokea Lowassa ni sawa na kukubali wamechezewa akili na ccm kwa kuwa misinformed na wana ccm wenye malengo yao binafsi dhidi ya Lowassa ambaye tuache utani, viongozi wengi wa umma walikuwa hawampendi kwasababu hataki mchezo na ujinga ujinga kwenye kazi za umma. Hilo liko wazi.
Sasa ccm kumbebesha zigo haina maana yenyewe chini ya uncle Magu imekuwa safi, no!
Kwahiyo kwa uadui unaoonyeshwa dhidi ya upinzani hata siasa kupigwa marufuku, angekuwa fisadi angeshaswekwa ndani tuache masihara. Serikali hii? Refer to people like Sumaye na Manji nk