Mafisadi Wakamatwe!-wasiruhusiwe Kuligawa Taifa!

jmushi1

Platinum Member
Nov 2, 2007
26,027
24,673
Nimeshangazwa sana na vitendo vya watuhumiwa wa ufisadi wakienda mikoani kwa kile kinachoitwa kujisafisha!

Ni gharama za nani wanatumia?

Kwanini sheria isifuate mkondo then wananchi wenyewe ndio wajiamulie kama ni kweli ni mafisadi ama la?

Serikali iko wapi ili kuwakinga na kuwaprotect wananchi na ulaghai wa mafisadi na propaganda!?

Serikali haiwajali wananchi wake ambao wengi wao ni masikini na wasio na uelewa wa kutosha kutokana na lack of education?

Kama kweli Serikali iko upande wa wanchi kwenye vita vya ufisadi..

Then kwa nini isiwalinde dhidi ya propaganda za mafisadi ambazo ndio walizitumia ili kuweza kuingia madarakani na kufanya ufisadi?

Je wanataka kuexploit ignorance ili wawatumie wananchi kama ndio kinga ya kujisafisha na hivyo kupelekea migawanyiko!?

Wananchi wapelekewe kesi ya "kujisafisha" baada ya sheria kuchukua mkondo na kuwasafisha na si vinginevyo!

Hawa kamwe kujisafisha hawawezi! Kivipi?

Mambo ya siasa ni next time..Hawa watu ni watuhumiwa!

Wana pesa nyingi za ufisadi hivyo wasipewe nafasi ya kuwarubuni wananchi hivyo haki kutotendeka hence machafuko na umasikini!

Maoni yangu ni kuwa hawa watu wawe under uangalizi kwa sasa then waruhusiwe kwenda kuelezea kesi yao mara baada ya sheria kuchukua mkondo wake!

Kikwete hawezi kukaa na kuwaangalia wakiwarubuni wananchi huku wakiwatisha wale wenye kuwanyooshea vidole!

MUUNGWANA UKO UPANDE WETU AMA WAO?

Walijiuzulu kwasababu ya tuhuma na si propaganda za kisiasa!

Ni tuhuma zilizowafanya wajiuzulu na wala si wananchi!

Ni tuhuma wanazotakiwa wazijibu na si eti "kujisafisha"

Ni tuhuma hizi hizi zitakazowasafisha mara baada ya mahakama kutoa uamuzi!

Hivyo wajiandae kisheria na si kuwavaa wananchi!

Kama ni kujisafisha waende ndani kwenye vyama vyao husika na ijulikane wazi kwamba wanawaelezea wana CCM na wala siyo Taifa zima!

Ni maoni tuu!
 
Nimeshangazwa sana na vitendo vya watuhumiwa wa ufisadi wakienda mikoani kwa kile kinachoitwa kujisafisha!

Ni gharama za nani wanatumia?
Kwanini sheria isifuate mkondo then wananchi wenyewe ndio wajiamulie kama ni kweli ni mafisadi ama la?
Serikali iko wapi ili kuwakinga na kuwaprotect wananchi na ulaghai wa mafisadi na propaganda!? Serkali haiwajali wananchi wake ambao wengi wao ni masikini na wasio na uelewa wa kutosha kutokana na lack of education?

Kama kweli Serikali iko upande wa wanchi kwenye vita vya ufisadi..Then kwa nini isiwalinde dhidi ya propaganda za mafisadi ambazo ndio walizitumia ili kuweza kuingia madarakani na kufanya ufisadi?

Je wanataka kuexploit ignorance ili wawatumie wananchi kama ndio kinga ya kujisafisha na hivyo kupelekea migawanyiko!?
Wananchi wapelekewe kesi ya "kujisafisha" baada ya sheria kuchukua mkondo na kwasafisha!
Hawa kamwe kujisafisha hawawezi! Kivipi?

Mambo ya siasa ni next time..Hawa watu ni watuhumiwa!

Wana pesa nyingi za ufisadi hivyo wasipewe nafasi ya kuwarubuni wananchi hivyo haki kutotendeka hence machafuko na umasikini!

Maoni yangu ni kuwa hawa watu wawe under uangalizi kwa sasa then waruhusiwe kwenda kuelezea kesi yao mara baada ya sheria kuchukua mkondo wake!
Kikwete hawezi kukaa na kuwaangalia wakiwarubuni wananchi huku wakiwatisha wale wenye kuwanyooshea vidole!

Walijiuzulu kwasababu ya tuhuma na si propaganda za kisiasa!

Kama ni kujisafisha waende ndani kwenye vyama vyao husika na ijulikane wazi kwamba anawaelezea wana CCM na wala siyo Taifa zima!
Ni maoni tuu!

Hivi ni kwanini watuhumiwa waachwe wakiranda randa mitaani? Wakiwatisha watu! Na kuwahadaa wananchi?
Hii haiwezi kuwa ni kuharibu ushahidi infront of the public eyes?
 
Chenge: Nimezushiwa

na Jane Kajoki, Bariadi

MBUNGE wa Bariadi Magharibi aliyejiuzulu uwaziri hivi karibuni kwa kashfa ya kukutwa na fedha zinazohusishwa na ufisadi, Andrew Chenge amewataka wananchi wa jimbo lake kuendelea kumwamini kwa kuwa yeye ni mtu safi na asiye na hatia yoyote kwani tuhuma dhidi yake ni za kuzushwa.
Mbali ya hilo, Chenge alisema alifikia uamuzi wa kujiuzulu wadhifa wa Waziri wa Miundombinu zaidi ya wiki mbili zilizopita si kwa sababu ya kukiri makosa, bali ili kutoa fursa kwa taasisi zinazochunguza kashfa yake kufanya kazi yake kwa uwazi.
Chenge ambaye jana alihutubia mikutano ya hadhara katika maeneo ya Bariadi Mjini, Ramadi, Nyakabimbi na Kapiwi, alisema wakazi wa Dar es Salaam ndio ambao wamekuwa wakimuona kuwa mtu asiyefaa kutokana na kubebeshwa tuhuma zisizo za ukweli, ikiwa ni pamoja na kuzushiwa kifo.
“Dar es Salaam wanasema sifai labda kwa sababu ya sura yangu...Pamoja na watu wa Dar es Salaam kupiga kelele kuwa sifai, naamini sina hatia yoyote, na ndiyo maana nilijiuzulu. Ninyi wakazi wa jimboni kwangu ndio mnajua kama sifai au nafaa.
“Haya mambo yaliyotokea ni ajali ya kisiasa. Ni mambo ya kupikwa na watu, lakini kwa tuhuma hizi wacha tuwape nafasi waendelee na uchunguzi. Sitakiwi kuzungumzia hilo kwa sasa, nimekuja nyumbani kuhimiza shughuli za maendeleo katika jimbo letu katika nyanja zote za barabara, elimu, afya na maji,” alisema Chenge ambaye alivuta umati mkubwa wa wananchi waliokuwa wakimshangilia kila alipokuwa akihutubia.
Alisema pamoja na kujiuzulu uwaziri, aliahidi kuendelea kuwatumikia wananchi wa jimbo lake na akasema anaamini ifikapo mwaka 2010 atakuwa ametekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005-2010.
“Walio na ndoto za ubunge tukutane kwenye hoja za utekelezaji wa ilani mwaka 2010. Mmeona tulivyojenga shule za sekondari, barabara, mabwawa, visima, vituo vya afya vyote hivyo ni katika jimbo letu. Pamoja na habari ya kuzushiwa kifo, nawaomba mtulie, tushirikiane kwa kutembea kifua mbele kufanya kazi na kujiletea maendeleo,” alisema Chenge ambaye anatembelea jimbo lake kwa mara ya kwanza tangu ajiuzulu.
Akiwa katika Kijiji cha Dutwa alisema alitaja vijisenti si kwa nia ya kukejeli bali akiwa na mtazamo wa Kisukuma ambao wao wanapoongelea ng’ombe 100 kwa mfano wanasema ‘vijing’ombe’.
Hii ni mara ya pili kwa Chenge kuzungumzia kauli yake ya vijisenti ambayo kwa kiwango kikubwa ndiyo inayoonekana kuwa iliyokuza tuhuma alizokuwa akihusishwa nazo.
Kwa mara ya kwanza, Chenge alizungumzia kauli yake hiyo jijini Dar es Salaam wakati alipofanya mahojiano kwa njia ya simu na gazeti hili, ambapo aliwaomba radhi Watanzania ambao walikwazika au kuumizwa na kauli yake hiyo ya vijisenti.
Alisema halikuwa lengo lake kuwakera wananchi kwa kauli hiyo iliyozua mjadala kiasi cha baadhi ya makundi ya watu wa kada tofauti kutoa maoni yao wakimtaka Rais Jakaya Kikwete amwajibishe.
“Mimi siyo Mzaramo. Hiki ni Kiswahili. Sisi wengine kule Usukumani kusema vijimambo, au vijisenti, vijitoto hivi ni kawaida kwa desturi zetu...ndiyo maana napenda kusema wazi kwamba iwapo kuna Watanzania niliwaumiza kwa kauli ile niliyoitoa kwa nia njema kabisa na wala si kwa lengo la kuwakejeli, naomba radhi kwa hilo,” alisema Chenge wakati huo.
Tuhuma dhidi ya Chenge ziliandikwa kwa mara ya kwanza katika gazeti la The Guardian la nchini Uingereza likikariri taarifa kutoka Taasisi ya Uchunguzi wa Makosa Makubwa ya Jinai ya nchini humo (SFO).
Gazeti hilo liliandika kuwa, uchunguzi wa SFO uligundua akaunti moja inayohusishwa na Chenge ikiwa na zaidi ya dola za Marekani milioni moja iliyopo kwenye kisiwa cha Jersey.
Gazeti hilo liliandika kwamba, SFO ilikuwa ikitarajia kuanza upya kufanya uchunguzi kuhusu fedha hizo ili kuangalia iwapo zilikuwa na uhusiano na zile zinazoaminika kuwa zilitolewa kwa njia ya rushwa wakati Tanzania iliponunua rada ya kijeshi kutoka nchini humo kwa paundi milioni 28 ambazo ni sawa na shilingi bilioni 70, mwaka 2002.
The Guardian katika habari yake hiyo liliripoti kuwa, taarifa hizo zinakuja ikiwa ni miaka mitatu sasa tangu Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) kwa kushirikiana na SFO na taasisi za uchunguzi za Uswisi na Jersey zilipoanza kuchunguza kuhusu kashfa nzima ya ununuzi wa rada.
Gazeti hilo lilimkariri Waziri Chenge akikiri kwamba fedha hizo ni zake na akatumia fursa hiyo kukanusha kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha hizo na kashfa nzima ya ununuzi wa rada, uliofanywa wakati yeye akiwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
“Jambo la wazi linalotaka kuonekana hapa ni kwamba mimi nilipokea kwa lengo la kujinufaisha mwenyewe fedha za rushwa kutoka BAE. Huu ni uongo,” alisema Chenge.
Aidha, gazeti hilo lilimkariri Chenge akisema kuwa, wakati rada hiyo ilipokuwa ikinunuliwa yeye alihusika kwa kiwango kidogo sana katika mchakato mzima, kwani jambo hilo lilishughulikiwa na wizara nyingine na uamuzi ukaidhinishwa na Baraza la Mawaziri.
Mbali ya hilo, gazeti hilo lilimkariri mwanasheria wa Chenge anayeishi Cleveland, Ohio, nchini Marekani, J Lewis Madorsky, akikanusha kwa niaba ya mteja wake huyo, kuwapo kwa uhusiano wowote kati ya fedha zake na tuhuma zozote.
“Wakati tukitambua kuwa masuala hayo yalitokea muda mrefu uliopita, tunaweza tu tukathibitisha kuwa, tuhuma zozote za ukiukwaji wa sheria, ukiukwaji wa maadili, kutenda isivyo sawa na mambo mengine ya hivyo dhidi ya mteja wetu ni mambo ambayo kimsingi tunayakanusha kwa nguvu kubwa,” alisema mwanasheria huyo wa Chenge. Hata hivyo, gazeti hilo liliandika uchunguzi huo dhidi ya Chenge unamfanya yeye kuwa tu shahidi muhimu, kwani wanaielenga zaidi BAE ambayo inadaiwa ilimlipa wakala mmoja wa Tanzania mamilioni ya fedha ili kujenga ushawishi wa rada iliyokuwa ikiiuza kununuliwa. Wakala huyo ambaye amekuwa akitajwa kwa muda mrefu, na ambaye sasa anaaminika kukimbia nchini na kutafutwa na polisi wa kimataifa ni, Shailesh Vithlani.
 
KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.
Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.

26.jpg

JAJI Warioba

“Niliyosoma hasa kutokana na taarifa ile ya Serikali, ukiisoma kwa makini unaona kuwa haukuwa ununuzi wa madeni, huo ulikuwa ni wizi wa fedha za umma,” anasema Jaji Warioba.
Anasema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, baadhi ya madeni si madeni bali kuna watu wametumia ulaghai kuchukua madeni ambayo yamekwisha kulipwa na wao kufanya udanganyifu kuyadai.
“Wapo ambao wamefanya hivyo kwa kughushi. Sasa kuna makosa mawili hapo. Wizi na kughushi, ni makosa mazito, na kama nilivyosema wakati ule ilipotoka mara ya kwanza, ukiona makampuni ambayo yametajwa si makampuni makubwa na mengi yake yaliundwa kwa kazi hii tu,” alisema katika mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.
Akionyesha kuwapo kwa watu wakubwa nyuma ya wizi wa fedha za EPA, Warioba anasema biashara ya kununua madeni inataka mtu mwenye fedha na mwenye ujuzi wa biashara hiyo lakini makampuni yaliyoorodheshwa na serikali mengi yanamilikiwa na watu wa kawaida kabisa wasio na uwezo huo.
“Kampuni hizi ni ndogo, watu wenye kampuni hizi wameandikwa watu wenye majina ya kawaida. Kwa mtu yeyote mwenye busara atajua hii ni hadaa tu. Wanaoshughulika hawakujiandika kwenye kampuni hizi, wamechukua watu wengine tu. Kwa hiyo, kuna kazi, kuna kazi ya kuwatafuta hawa wazito waliokuwa wanahusika. Na kama ni wazito na wameingia katika wizi wa mali ya Taifa na kughushi, suala hili ni zito kuliko tunavyoliona,” anasema na kuongeza;
“Mimi naamini kama kweli tunaishughulikia kwa nguvu zote, EPA ni kubwa kuliko Richmond, kuliko haya yaliyotokea. Kwa hiyo tutangojea matokeo. Na hapa kwa kuwa walau ushahidi wa kawaida upo, taarifa zinasema zile nyaraka zilizowezesha madeni hayo kununuliwa ni za kughushi, basi unaanzia hapo. Ukihakikisha kwamba ni za kughushi, kwamba haya madeni hayakuwapo, ukithibitisha kwamba hili deni halikuwapo sasa huyo aliyechukua fedha hizo alitumia wapi?”
Alisema akiwa kama raia mwema wa Tanzania anasubiri kwa makini kuona matokeo ya EPA, na kuongeza kwamba kama kweli nia ya kusafisha ipo, ni lazima waliofanya makosa wapatikane na kushughulikiwa na si wale waliotangulizwa.
“Mimi sijui utaratibu wanaotumia. Lakini kwa utaratibu wa kawaida, mimi nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi, kwa suala hili la jinai unalishughulikia linakwenda mahakamani. Adhabu inatolewa pamoja na kurudisha hizo fedha, hilo ndilo nalitarajia,” anasema.
Anasema kwa kawaida hatua za kisheria ni lazima zichukuliwe na kwamba unapokwenda mahakamani unaweza kutumia sheria kurudisha fedha zilizoibwa hata ikibidi kufilisi wahusika.
Hivi karibuni timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia waliochukua fedha za EPA ilieleza wazi kwamba imekua ikipokea fedha kutoka kwa watuhumiwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuepuka kupoteza fedha hizo huku wanaozirejesha wakiendelea kuwa siri.
Timu hiyo ya Rais inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, wote wakisaidiwa na maofisa kutoka ofisi zao na kutoka asasi nyingine za umma.
Akizungumzia kitendo cha viongozi hao wa juu wa dola kufanya mazungumzo na watuhumiwa, Jaji Warioba anasema; “Kwamba hawa ndio kweli viongozi wa ngazi ya juu wa vyombo vya dola vinavyoshughulika na uhalifu wanafanya kazi hiyo. Imani yangu ni kwamba hawatapinda sheria. Wakipinda sheria tutakuwa tumeleta madhara makubwa sana kwa nchi hii. Kwa sababu wananchi lazima kwa upande wa sheria waamini ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni lazima waamini ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, lazima waamini ofisi ya TAKUKURU.”
Warioba anasema watendaji hao wa dola wakipinda sheria, imani ya wananchi itapungua na hivyo ni jukumu lao ni kubwa, na kwamba yeye ana imani kwamba hawatapinda sheria.
Akizungumzia hali ya kisiasa ya nchi kutokana na kukwama kwa mambo mengi ikiwamo muafaka wa kisiasa Zanzibar na kuibuka kwa wimbi kubwa la tuhuma za ufisadi, Jaji Warioba anaonekana kutokua na imani na hali hiyo na anakiri kuwapo kwa udhaifu katika uongozi wa juu wa kitaifa.
“Kama nilivyosema, kila mtu ni kuzungumzia ufisadi, hata mafisadi wenyewe, maana ukiona wote hawa wanaozungumzia, huwezi kusema ni watu safi, pamoja na vyombo vya habari, navyo haviwezi kujisifu. Wengine wanaoandika juu ya ufisadi ndio hao hao waliokuwa wakichukua fedha za hawa, wanawaandika kuwa ni wazuri wakati wa uchaguzi. Walikuwa wakiwapamba. Kwa hiyo kuna wengine ni unafiki tu, ama ni ufisadi na wenyewe,” anasema.
Warioba anapongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari na wabunge katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini anaonya vita hiyo isitumike kufunika madhambi yaw engine ama kuwaumiza baadhi yao.
“Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?
“Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?” anahoji Jaji Warioba.
Anasema wamo wengi ambao ni sehemu ya uongozi, na hivyo isije tokea mapambano ndani ya uongozi yakageuzwa kuwa ni vita ya kweli kumaliza ufisadi.
“Mimi nataka niwe na uhakika tukifika mwaka 2010 tuweze kuchagua viongozi safi, tusipate viongozi ambao katika mchakato wa uchaguzi watakwenda na takrima kwa sababu kama wanakwenda na takrima wamezipata fedha hizo kwa ufisadi,” anasema.
Akizungumzia muafaka kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Wariona anasema tatizo kubwa ni mgawanyiko katika uongozi. Anasema wapo ambao hawataki muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa.

Kuhusu wanaotishia kurejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF, Warioba anasema hivyo ni vitisho visivyo na maana katika mazingira ya sasa kwani hata wakiachwa hawana uwezo huo na kwamba tatizo kubwa ni udhaifu wa viongozi.
“Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu,” anasema na kuongeza;
“Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi.”
Pamoja na kuonekana kukwepa kumshutumu Rais Mstaafu Mkapa, Jaji Warioba anasema kinga waliyonayo viongozi akiwamo rais ni ya kisiasa tu, na hivyo kwake yeye suala la kinga ya kisheria si tatizo bali ukweli na uhakika wa tuhuma zinazomgusa kiongozi husika na kwamba ni mahakama inayoweza kutoa uamuzi wa haki.
“Nimeona wanaandika na nimeona mjadala mkubwa tu unaolenga kwenye immunity. Mimi nafikiri suala hilo si la msingi kwa sasa hivi. Na mjadala unalenga kwamba aseme, naona si la msingi. Kwa sababu hatutaki kwamba huyu awe tried na vyombo vya habari. Maana hapa naona kama ni trial kwenye vyombo vya habari.
“Waseme ni kosa gani, amefanya kwa msingi wa sheria gani, sasa waendelee. Sasa mengi wanayosema ni ya kisiasa. Yakisemwa ya kisiasa unataka mtu awajibike kisiasa. Kama ni kosa la jinai, waseme amevunja wapi sheria, lakini kusema kweli mimi sioni kwa vyombo vya habari kusema yote haya na wanachotaka ni kwamba ajitetee, ajitetee wao ndio wamekuwa Mahakama?” anahoji Jaji Warioba ambaye amewahi kufanya kazi kwa karibu na Mkapa.
Warioba anasema vyombo vya habari vinataka kuwa Mahakama na akashauri kwamba kama kuna kosa alilofanya Mkapa ni vyema wakasubiri afikishwe mahakamani ambako atakuwa na nafasi ya kujitetea na kueleza upande wake.
“Immunity nasema sasa hivi siyo issue. Sema kosa lililotendeka. Anashitakiwa lakini wanasema hatuwezi kuendelea kwa sababu kuna immunity. Bila kusema kosa huwezi kufika kwenye immunity. Huwezi kuanza na immunity bila kuwa na kosa, kwa hiyo mimi sitaki kujiingiza katika mjadala wa immunity. Hii ni ya kisiasa tu,” anasema.
 
KATIKA kauli ambazo zitawashitua watawala, Waziri Mkuu wa zamani, Jaji Joseph Warioba, amesema nchi ina viongozi dhaifu, umma unanyonywa, rushwa imeongezeka, wezi wa fedha za EPA waanikwe na Rais Msitaafu, Benjamin Mkapa akajibu tuhuma zake mahakamani.
Katika mahojiano maalumu na Raia Mwema, Warioba amesema kuna dalili ya kuwapo watu wakubwa nyuma ya kashfa ya fedha zilizopotea katika sakata la EPA na kwamba yaliyotokea ni wizi wa hali ya juu na baadhi wameghushi na kwamba hatua za kisheria ni lazima zichukue mkondo wake.

26.jpg

JAJI Warioba

"Niliyosoma hasa kutokana na taarifa ile ya Serikali, ukiisoma kwa makini unaona kuwa haukuwa ununuzi wa madeni, huo ulikuwa ni wizi wa fedha za umma," anasema Jaji Warioba.
Anasema kwa mujibu wa taarifa ya Serikali, baadhi ya madeni si madeni bali kuna watu wametumia ulaghai kuchukua madeni ambayo yamekwisha kulipwa na wao kufanya udanganyifu kuyadai.
"Wapo ambao wamefanya hivyo kwa kughushi. Sasa kuna makosa mawili hapo. Wizi na kughushi, ni makosa mazito, na kama nilivyosema wakati ule ilipotoka mara ya kwanza, ukiona makampuni ambayo yametajwa si makampuni makubwa na mengi yake yaliundwa kwa kazi hii tu," alisema katika mahojiano ambayo sehemu yake ya kwanza imechapishwa katika kurasa za 12 na 13 za toleo hili.
Akionyesha kuwapo kwa watu wakubwa nyuma ya wizi wa fedha za EPA, Warioba anasema biashara ya kununua madeni inataka mtu mwenye fedha na mwenye ujuzi wa biashara hiyo lakini makampuni yaliyoorodheshwa na serikali mengi yanamilikiwa na watu wa kawaida kabisa wasio na uwezo huo.
"Kampuni hizi ni ndogo, watu wenye kampuni hizi wameandikwa watu wenye majina ya kawaida. Kwa mtu yeyote mwenye busara atajua hii ni hadaa tu. Wanaoshughulika hawakujiandika kwenye kampuni hizi, wamechukua watu wengine tu. Kwa hiyo, kuna kazi, kuna kazi ya kuwatafuta hawa wazito waliokuwa wanahusika. Na kama ni wazito na wameingia katika wizi wa mali ya Taifa na kughushi, suala hili ni zito kuliko tunavyoliona," anasema na kuongeza;
"Mimi naamini kama kweli tunaishughulikia kwa nguvu zote, EPA ni kubwa kuliko Richmond, kuliko haya yaliyotokea. Kwa hiyo tutangojea matokeo. Na hapa kwa kuwa walau ushahidi wa kawaida upo, taarifa zinasema zile nyaraka zilizowezesha madeni hayo kununuliwa ni za kughushi, basi unaanzia hapo. Ukihakikisha kwamba ni za kughushi, kwamba haya madeni hayakuwapo, ukithibitisha kwamba hili deni halikuwapo sasa huyo aliyechukua fedha hizo alitumia wapi?"
Alisema akiwa kama raia mwema wa Tanzania anasubiri kwa makini kuona matokeo ya EPA, na kuongeza kwamba kama kweli nia ya kusafisha ipo, ni lazima waliofanya makosa wapatikane na kushughulikiwa na si wale waliotangulizwa.
"Mimi sijui utaratibu wanaotumia. Lakini kwa utaratibu wa kawaida, mimi nilikuwa Mwanasheria Mkuu wa nchi, kwa suala hili la jinai unalishughulikia linakwenda mahakamani. Adhabu inatolewa pamoja na kurudisha hizo fedha, hilo ndilo nalitarajia," anasema.
Anasema kwa kawaida hatua za kisheria ni lazima zichukuliwe na kwamba unapokwenda mahakamani unaweza kutumia sheria kurudisha fedha zilizoibwa hata ikibidi kufilisi wahusika.
Hivi karibuni timu iliyoundwa na Rais Jakaya Kikwete kushughulikia waliochukua fedha za EPA ilieleza wazi kwamba imekua ikipokea fedha kutoka kwa watuhumiwa kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kuepuka kupoteza fedha hizo huku wanaozirejesha wakiendelea kuwa siri.
Timu hiyo ya Rais inaongozwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, akisaidiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, Saidi Mwema, na Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU, Edward Hosea, wote wakisaidiwa na maofisa kutoka ofisi zao na kutoka asasi nyingine za umma.
Akizungumzia kitendo cha viongozi hao wa juu wa dola kufanya mazungumzo na watuhumiwa, Jaji Warioba anasema; "Kwamba hawa ndio kweli viongozi wa ngazi ya juu wa vyombo vya dola vinavyoshughulika na uhalifu wanafanya kazi hiyo. Imani yangu ni kwamba hawatapinda sheria. Wakipinda sheria tutakuwa tumeleta madhara makubwa sana kwa nchi hii. Kwa sababu wananchi lazima kwa upande wa sheria waamini ofisi ya Mwanasheria Mkuu, ni lazima waamini ofisi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi, lazima waamini ofisi ya TAKUKURU."
Warioba anasema watendaji hao wa dola wakipinda sheria, imani ya wananchi itapungua na hivyo ni jukumu lao ni kubwa, na kwamba yeye ana imani kwamba hawatapinda sheria.
Akizungumzia hali ya kisiasa ya nchi kutokana na kukwama kwa mambo mengi ikiwamo muafaka wa kisiasa Zanzibar na kuibuka kwa wimbi kubwa la tuhuma za ufisadi, Jaji Warioba anaonekana kutokua na imani na hali hiyo na anakiri kuwapo kwa udhaifu katika uongozi wa juu wa kitaifa.
"Kama nilivyosema, kila mtu ni kuzungumzia ufisadi, hata mafisadi wenyewe, maana ukiona wote hawa wanaozungumzia, huwezi kusema ni watu safi, pamoja na vyombo vya habari, navyo haviwezi kujisifu. Wengine wanaoandika juu ya ufisadi ndio hao hao waliokuwa wakichukua fedha za hawa, wanawaandika kuwa ni wazuri wakati wa uchaguzi. Walikuwa wakiwapamba. Kwa hiyo kuna wengine ni unafiki tu, ama ni ufisadi na wenyewe," anasema.
Warioba anapongeza juhudi zinazofanywa na vyombo vya habari na wabunge katika mapambano dhidi ya rushwa na ufisadi lakini anaonya vita hiyo isitumike kufunika madhambi yaw engine ama kuwaumiza baadhi yao.
"Sina hakika kama wote wamezinduka hivi. Jana walikuwa wanasema hakuna rushwa, hakuna ufisadi. Leo ndiyo wako msitari wa mbele wanatafuta mafisadi na ukiangalia zaidi ni viongozi. Na hasa wabunge ndio wanaongoza vita hii. Ni vizuri Bunge liongoze lakini je, tunawaamini wote? Kwamba nia yao hasa ni kumaliza ufisadi au kuna sababu nyingine?
"Ikifika mahali tuwaulize hawa ambao sasa wanaonekana wana uchungu sana na ufisadi. Mwaka 2005 tuliona yaliyotokea. Hivi ni wangapi ambao wako safi? Mwananchi akimwuliza mbunge wake, na hii inawezekana kwa zaidi ya nusu ya wabunge, kwamba mbona wewe ulikuja na fedha nyingi sana kwenye uchaguzi na wewe si tajiri, ulizipata wapi?" anahoji Jaji Warioba.
Anasema wamo wengi ambao ni sehemu ya uongozi, na hivyo isije tokea mapambano ndani ya uongozi yakageuzwa kuwa ni vita ya kweli kumaliza ufisadi.
"Mimi nataka niwe na uhakika tukifika mwaka 2010 tuweze kuchagua viongozi safi, tusipate viongozi ambao katika mchakato wa uchaguzi watakwenda na takrima kwa sababu kama wanakwenda na takrima wamezipata fedha hizo kwa ufisadi," anasema.
Akizungumzia muafaka kati ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Wananchi (CUF), Jaji Wariona anasema tatizo kubwa ni mgawanyiko katika uongozi. Anasema wapo ambao hawataki muafaka wanaona njia ni kusema tupate maoni ya wananchi wakitarajia kwamba wananchi watakataa.

Kuhusu wanaotishia kurejea kwenye Afro Shirazi Party (ASP) kuliko kuingia katika Muafaka na CUF, Warioba anasema hivyo ni vitisho visivyo na maana katika mazingira ya sasa kwani hata wakiachwa hawana uwezo huo na kwamba tatizo kubwa ni udhaifu wa viongozi.
"Zaidi wanaosema warudi ASP ni watu wa Zanzibar, lakini nadhani pia kuna udhaifu katika viongozi Bara. Wakiisha kusikia madai hayo ya ASP, wanasema jamani waachieni mambo yao! Lakini haya si mambo yao, ni mambo ya nchi. Zanzibar ni sehemu ya Tanzania, likitokea tatizo Zanzibar ni tatizo la Tanzania. Hawa wanaosema waachieni haya ni mambo yao ni viongozi dhaifu," anasema na kuongeza;
"Hilo ni suala muhimu, hapo ndipo uongozi unapohitajika. Huwezi kukwepa. Uongozi kazi yake ni kuamua mambo mazito, na wakati wote unaweza kuwa na wasiwasi, lakini unaamua kwa maslahi ya taifa. Hata kama katika kuamua huko unahisi kuwa kuna baadhi watakulaumu. Usiogope lawama, dira yako iwe kuwa hii ni kwa manufaa taifa ama hapana. Manufaa ya Taifa sasa hivi ni kumaliza mpasuko wa Zanzibar. Lolote linalohitajika kumaliza mpasuko huo ni vizuri viongozi wakachukua uamuzi, utakuwa ni mgumu lakini ni wajibu wao kuchukua uamuzi."
Pamoja na kuonekana kukwepa kumshutumu Rais Mstaafu Mkapa, Jaji Warioba anasema kinga waliyonayo viongozi akiwamo rais ni ya kisiasa tu, na hivyo kwake yeye suala la kinga ya kisheria si tatizo bali ukweli na uhakika wa tuhuma zinazomgusa kiongozi husika na kwamba ni mahakama inayoweza kutoa uamuzi wa haki.
"Nimeona wanaandika na nimeona mjadala mkubwa tu unaolenga kwenye immunity. Mimi nafikiri suala hilo si la msingi kwa sasa hivi. Na mjadala unalenga kwamba aseme, naona si la msingi. Kwa sababu hatutaki kwamba huyu awe tried na vyombo vya habari. Maana hapa naona kama ni trial kwenye vyombo vya habari.
"Waseme ni kosa gani, amefanya kwa msingi wa sheria gani, sasa waendelee. Sasa mengi wanayosema ni ya kisiasa. Yakisemwa ya kisiasa unataka mtu awajibike kisiasa. Kama ni kosa la jinai, waseme amevunja wapi sheria, lakini kusema kweli mimi sioni kwa vyombo vya habari kusema yote haya na wanachotaka ni kwamba ajitetee, ajitetee wao ndio wamekuwa Mahakama?" anahoji Jaji Warioba ambaye amewahi kufanya kazi kwa karibu na Mkapa.
Warioba anasema vyombo vya habari vinataka kuwa Mahakama na akashauri kwamba kama kuna kosa alilofanya Mkapa ni vyema wakasubiri afikishwe mahakamani ambako atakuwa na nafasi ya kujitetea na kueleza upande wake.
"Immunity nasema sasa hivi siyo issue. Sema kosa lililotendeka. Anashitakiwa lakini wanasema hatuwezi kuendelea kwa sababu kuna immunity. Bila kusema kosa huwezi kufika kwenye immunity. Huwezi kuanza na immunity bila kuwa na kosa, kwa hiyo mimi sitaki kujiingiza katika mjadala wa immunity. Hii ni ya kisiasa tu," anasema.

Hizi highlight safi sana!
They've made my day!
 
Hapo ndipo tatizo lilipo, tunaomba hao Takokuu wasikae tu chini wachunguze haya mambo na wahusika washitakiwe, wakishindwa kufanya hivyo siku itafika wananchi watachukua sheria mkononi, mbona hayo ya masaki ni madogo lakini ni dalili! tafadhali msitulazimishe kwenda huko, washitakini.
 
Kituko kingine ni serikali imesema kuwa Balali ni mtuhumiwa huru asiyetakiwa kuhojiwa kwenye wizi wake!
Ngoja niilete makala hapa...
 
Ikulu: Tukimtaka Ballali tutampata

na Irene Mark

SERIKALI imesema haimtafuti aliyewahi kuwa Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Daudi Ballali, ambaye mapema mwaka huu alifutwa kazi na Rais Jakaya Kikwete kutokana na kubainika kwa wizi wa mamilioni ya shilingi katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akizungumza na waandishi wa habari Ikulu Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu, Salvatory Rweyemamu, alisema kuwa serikali ina mkono mrefu na iwapo itafikia hatua ya kumtafuta gavana huyo wa zamani wa BoT, haitashindwa kamwe kumfikia alipo.
Alisema kutokuwepo nchini kwa Ballali, au kutojulikana alipo, si jambo linaloisumbua serikali kwa sasa, kwa sababu hivi sasa yeye ni raia wa kawaida, hivyo anao uhuru wa kuishi popote anapopenda.
“Serikali haimtafuti Ballali (kwa sasa), lakini ikiamua kufanya hivyo haitashindwa. Kwanza ni private citizen (raia huru) siyo mwajiriwa wa serikali tena,” alisema Rweyemamu na kuongeza kuwa, mkono wa serikali ni mrefu hautashindwa kumpata Ballali iwapo itamhitaji.
Akifafanua zaidi, alisema baada ya kutenguliwa kwa uteuzi wake, serikali iliunda timu ya kuwachunguza watuhumiwa wa EPA, kuhakikisha fedha zilizoibwa zinarudi na kuwachukulia hatua waliohusika, akiwemo Ballali.
Alisema: “Ninachofahamu ni kwamba, timu iliyopewa kazi kuhusu ubadhirifu wa EPA inaendelea na kazi yake na tunaona jinsi fedha zinavyorudishwa.” Mkurugenzi huyo pia alikiri kwamba serikali haifahamu hospitali aliyokuwa akitibiwa Ballali, licha ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkullo, kukaririwa akisema alimtafuta Ballali bila mafanikio alipokuwa jijini Washington, Marekani.
“Kwa kweli sifahamu hasa Ballali alikuwa akitibiwa katika hospitali gani, lakini najua alikuwa nchini Marekani katika Jimbo la Boston, ila hospitali kwa kweli siijui.
“Lakini huyu ni mtu huru, hivyo anaweza kuishi popote… huyu ana nyumba yake nchini Marekani… yupo huko anaishi na familia yake,” alisisitiza Rweyemamu katika ufafanuzi wake.
Alisema mafanikio ya timu inayochunguza suala la EPA yanaonekana, hivyo aliwaomba Watanzania kusubiri ripoti itakayotolewa baada ya kukamilika kwa kazi hiyo.
Hivi karibuni, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Johnson Mwanyika, ambaye pia ni kiongozi wa timu hiyo, alibainisha kuwa kazi ya timu hiyo inafanyika kwa siri na kwamba zaidi ya sh bilioni 67 zilikuwa zimerejeshwa na kampuni zilizodaiwa kujichotea fedha hizo kutoka EPA.
Kwa upande wake, mjumbe wa timu hiyo, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Said Mwema, aliwahi kukaririwa akisema aina ya uchunguzi unaofanywa dhidi wa kampuni na wamiliki hao haitakiwi kuwataja watuhumiwa wanaorudisha fedha hizo hadi watakapohitimisha kazi yao.
Timu hiyo ina wajumbe watatu ikihusisha pia Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru).
Mwanzoni mwa mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete alitengua uteuzi wa aliyekuwa Gavana wa BoT, baada ya taarifa ya uchunguzi wa hesabu uliofanywa na Kampuni ya Ukaguzi ya Ernst & Young na kubaini ubadhirifu wa zaidi ya sh bilioni 133.
Taarifa hiyo ilibaini kuwapo kwa kampuni hewa 22 zilizolipwa mamilioni ya fedha kutoka kwenye akaunti hiyo kati ya mwaka 2005 na 2006.
Hata hivyo, ilibainika kwamba, baadhi ya kampuni hizo zilidanganya kuhusu usajili na wamiliki wake huku nyingine zikimilikiwa na vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wengine wakitumia nyaraka za kughushi kuiba mabilioni hayo.
Mbali na udanganyifu huo,fedha za EPA zinadaiwa kusaidia kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2005.
Kutokana na kashfa hiyo na nyingine zilizoikumba serikali ya awamu ya nne, nchi wahisani na washirika wa maendeleo walitishia kusitisha misaada yao katika bajeti ya serikali.
Tishio hilo la wahisani ambao mchango wao kwenye bajeti ya serikali ni asilimia 43, liliifanya serikali kuwaangukia kwa kuchukua hatua za haraka katika mapambano dhidi ya ufisadi. Jitihada hizo za serikali zinaonekana kuzaa matunda kwani siku mbili zilizopita, wahisani hao wametangaza kuendelea kuchangia bajeti ya serikali baada ya kuridhishwa jinsi Rais Kikwete alivyoshughulikia suala la ufisadi nchini. Hata hivyo, uamuzi huo wa wahisani uliingia doa juzi baada ya Makamu Mwenyekiti wa Chadema, Chacha Wangwe kuutuhumu hadharani Umoja wa Ulaya (EU) akisema uamuzi wao wa kurejesha misaada unaonyesha kwamba umekuwa na ajenda ya siri ya kulinda ufisadi kwa ushirikiano na serikali.
 
Wanaligawa Vipi Taifa Wakati Wao Ndio Viongozi Wa Taifa ? Kwa Sababu Wewe Ni Chadema Basi Chochote Kikisemwa Na Ccm Ni Kugawa Taifa , Kugawa Watu Sijui Udini Na Mambo Mengine Kama Hayo

Taifa Haliwezi Kugawa Kwa Mtindo Huo Na Tanzania Yote Ni Moja Kama Mtu Ana Malalamiko Yake Apeleka Katika Vyombo Vya Sheria Au Sehemu Husika Atasaidiwa Zaidi Katika Hilo Na Sio Kuwahukumu Watu Kwa Maneno Ya Vijiweni Kama Haya
 
(1)Wanaligawa Vipi Taifa Wakati Wao Ndio Viongozi Wa Taifa ? Kwa Sababu (2)Wewe Ni Chadema Basi Chochote Kikisemwa Na Ccm Ni Kugawa Taifa , Kugawa Watu Sijui Udini Na Mambo Mengine Kama Hayo

Taifa Haliwezi Kugawa Kwa Mtindo Huo Na Tanzania Yote Ni Moja Kama Mtu Ana Malalamiko Yake Apeleka Katika Vyombo Vya Sheria Au Sehemu Husika Atasaidiwa Zaidi Katika Hilo Na (3)Sio Kuwahukumu Watu Kwa Maneno Ya Vijiweni Kama Haya

1)Hapa unapingana na usemi wa serikali kuwa sasa kina Balali ni huru baada ya kutuhumiwa! Uongozi wa Taifa wanautoa wapi? Kwanza hujui hizo ni issue za kitaifa!

WASILIGAWE TAIFA WAENDE MAHAKAMANI AMA HUKO KWENYE VYAMA VYAO! HUKO NDIO WATAKAOUPATA HUO USAFI WANANOULILIA NA SI KUTOKA KWA MASIKINI WALE WALE ALIOWAFISADI!
Who's on THE PEOPLE'S SIDE?

Hawa ni watuhumiwa pale inapokuja kwenye tuhuma za uhujumu uchumi wa taifa! NI KOSA ZITO!

Hawatakiwi wapewe nafasi kama waliyokuwa nayo hapo awali na kupata uwezo wa kuwarubuni wananchi na hivyo kuchaguliwa bila ya kudig background yao ya ufisadi!

Kuanza kampeni za ubunge etc etc kwa girini la kujisafisha!

Kucreate mixed feelings hence migawanyiko na pengine vurugu!

Huwezi kutaka kuchaguliwa ili urudi kwenye ufisadi upya kabla mahakama haijatoa uamuzi wala kabla bado hawajahojiwa!

WATUHUMIWA WA KINAMNA GANI HAWA AMBAO HAWAHOJIWI?

2)Mimi sio CHADEMA! "I am for the next generation forget about me"-Jmushi1

3)Sijatumia maneno ya kijiweni...Everything has an evidence and the evidence comes from the credible sources na kama ni tofauti waje wataalam wa kisheria hapa watueleze!

NB: HIVI UNAFIKRI SADDAM ANGEPEWA JUKWAA LA KISIASA WAKATI WA KUHOJIWA WANGEMWEZA KWELI? SI NA YEYE ANGEENDA KUWARUBUNI WANANCHI UPYA?
 
takakimbilia mikoani kwani wanajua habari zao hawazijui vizuri....dar kwao ni pachungu,watatembelea magari tu
 
takakimbilia mikoani kwani wanajua habari zao hawazijui vizuri....dar kwao ni pachungu,watatembelea magari tu

Na ndio maana ni muhimu kubanana nao huko huko na pia wasiruhusiwe kuanza kampeni!

HAWA WATU NI WATUHUMIWA LAKINI HAWAJA HOJIWA!
Mimi niliwahi kuswekwa ndani kwasababu tu kimada wa RPC ameamua!

Na dhamana nikanyimwa ili kukomolewa..na kushinda lock up weekend nzima!
Tena wakaambiwa kwa amri ya mkuu wasipokee hata kitu kidogo!

Kwanini Mungu asitusaidie atokezee hawara wa kiongozi awaambie kuwa mafisadi are yet to be held accountable!
Watuhumiwa gani wasiohitajika kuhojiwa jamani!

Yani wana uhuru baada ya tuhuma za uhujumu uchumi?
Sheria ipi hiyo?
Hivi Jaji Warioba huwa anakuja humu?
Tunahitaji msaada!
 
HAWA WAHISANI WASITULETEE ZA KULETA KWANZA SISI NI MATAJIRI KULIKO WAO!

KASHFA KAMA HII IKITOKEA HUKO KWAO WATUHUMIWA WANAHOJIWA SI TU NA KAMATI..BALI KWANZA NA BUNGE THEN KAMATI YA BUNGE,THEN MAHAKAMA..AND FINALY SHERIA INACHUKUA MKONDO WAKE!

TUMEONA USHAHIDI KAMILI WA WATU KAMA MABILIONEA WA KIKWELI WA MAREKANI KAMA VILE KEN LAY ALIYEAMUA KUJIUA!

RAIS KAMA ANA UWEZO WA KUINGILIA SHUGHULI NA RESPONSIBILITY ZA BUNGE THEN ANASHINDWA VIPI KUAMURU WAHOJIWE?

ET HAWATAKIWI KUHOJIWA!?
WAHISANI WANA USHAHIDI GANI KUWA JUSTICE HAS BEEN SERVED OR AT LEAST IS BEING SERVED?
 
VIZINGITI VYA KUWAZUIA WASIHARIBU USHAHIDI AMA KUPINDISHA HAKI NI VIPI HIVYO?
 
amini msiamini kitakachotokea hapo hawa jamaa watatoroka mmoja mmoja kisha itaundwa kamati itakayotumia mamilioni ya walala hoi kuchunguza hawa jamaa wamekimbilia wapi...

kama ingekuwa nchi inayoongozwa na kiongozi timamu kichwani hawa jamaa wangekuwa wameshapitia katika njia zoote wanazostahili kupita na wangekuwa wameshapandishwa kizimbani, ila kwa kuwa nchi yetu ndo jalala la kila uchafu ishu za mafisadi zitakwenda mwisho zitazimwa.
 
Pata uhondo.....

Balali hana ujanja!

2008-05-09 19:21:02
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Licha ya Serikali kutoa taarifa inayodai kuwa hivi sasa haimtafuti aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Dokta Daudi Balali ambaye inasemekana amejichimbia Marekani, baadhi ya wanasiasa nchini wanasema, msomi huyo hana ujanja na kinachotakiwa ni kumrejeshwa nchini fasta fasta ili aeleze ni vipi mabilioni ya Watanzania yalichotwa na kuliwa hivihivi.

Imeelezwa kuwa kinachotakiwa kufanyika ni uchunguzi kuendelea kufanywa huku mtuhumiwa akiwa tayari ametiwa mikononi mwa dola kama inavyofanyika kwa watuhumiwa wengine wa makosa mbalimbali.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha,CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, amesema sheria ya Tanzania kuhusu makosa ya jinai iko wazi na kamwe haichagui mtu na wala haiangalii hali yake kuwa ni tajiri au maskini.

Akasema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtuhumiwa wa makosa ya jinai anapaswa kukamatwa, kufunguliwa jalada polisi na kisha uchunguzi wake kufanywa wakati mtuhumiwa akiwa nyumbani kwa dhamana au rumande.

Dk. Slaa amesema sheria inasema kesi ambayo hairuhusu mtu kukamatwa au kufungwa ni ya madai pekee.

\"Tuhuma zinazomkabili Dk. Balali ni za wizi wa mabilioni ya fedha... hilo ni kosa la jinai.

Sasa kwanini asitafutwe na kukamatwa? Sasa wanaposema wanachunguza, watafanya hivyo kwa RB ipi?\" akahoji Dk. Slaa.

Amesema kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria ni kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi, kuwafungulia RB polisi na kisha uchunguzi kufanyika wakati watuhumiwa wakiwa rumande au wakiwa nje kwa dhamana.

Jana Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Bw. Balali ametoweka na hajulikani alipo.

Hata hivyo, taarifa zilizotolewa jana kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu Bw. Salva Rweyemamu, zimedai kuwa hivi sasa, Serikali haina shida na Dk. Balali na kwamba itamtafuta wakati utakapowadia baada ya uchunguzi wa sakata lake kukamilika.

Dk. Balali alipigwa chini na Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete baada ya ripoti ya mkaguzi wa hesabu za BOT, kampuni ya ukaguzi ya kimataifa ya Ernst & Young, kubaini kuwa kuna mapesa mengi yametumika visivyo wakati akiiongoza taasisi hiyo.

Kashfa kubwa iliyotikisa nchi na kumfanya Balali apigwe chini na Rais ni ile ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh. Bilioni 133 za BOT, ambazo zililipwa isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.
  • SOURCE: Alasiri
 
takakimbilia mikoani kwani wanajua habari zao hawazijui vizuri....dar kwao ni pachungu,watatembelea magari tu

Sio tu Dar ni chungu...Bali Tanzania itakuwa chungu kwa mafisadi na "sheria ni msumeno" wenye kukata pande zote kupata maana halisi!
 
Hapo ndipo tatizo lilipo, tunaomba hao Takokuu wasikae tu chini wachunguze haya mambo na wahusika washitakiwe, wakishindwa kufanya hivyo siku itafika wananchi watachukua sheria mkononi, mbona hayo ya masaki ni madogo lakini ni dalili! tafadhali msitulazimishe kwenda huko, washitakini.

Wananchi wamesha amua kuizika CCM! Mark ma words kwenye hili!
CCM bye bye!
 
Pata uhondo.....

Balali hana ujanja!

2008-05-09 19:21:02
Na Emmanuel Lengwa, Jijini

Licha ya Serikali kutoa taarifa inayodai kuwa hivi sasa haimtafuti aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Dokta Daudi Balali ambaye inasemekana amejichimbia Marekani, baadhi ya wanasiasa nchini wanasema, msomi huyo hana ujanja na kinachotakiwa ni kumrejeshwa nchini fasta fasta ili aeleze ni vipi mabilioni ya Watanzania yalichotwa na kuliwa hivihivi.

Imeelezwa kuwa kinachotakiwa kufanyika ni uchunguzi kuendelea kufanywa huku mtuhumiwa akiwa tayari ametiwa mikononi mwa dola kama inavyofanyika kwa watuhumiwa wengine wa makosa mbalimbali.

Akizungumza na Alasiri leo asubuhi, Katibu Mkuu wa chama cha upinzani cha,CHADEMA, Dk. Wilbrod Slaa, amesema sheria ya Tanzania kuhusu makosa ya jinai iko wazi na kamwe haichagui mtu na wala haiangalii hali yake kuwa ni tajiri au maskini.

Akasema kwa mujibu wa sheria za nchi, mtuhumiwa wa makosa ya jinai anapaswa kukamatwa, kufunguliwa jalada polisi na kisha uchunguzi wake kufanywa wakati mtuhumiwa akiwa nyumbani kwa dhamana au rumande.

Dk. Slaa amesema sheria inasema kesi ambayo hairuhusu mtu kukamatwa au kufungwa ni ya madai pekee.

\"Tuhuma zinazomkabili Dk. Balali ni za wizi wa mabilioni ya fedha... hilo ni kosa la jinai.

Sasa kwanini asitafutwe na kukamatwa? Sasa wanaposema wanachunguza, watafanya hivyo kwa RB ipi?\" akahoji Dk. Slaa.

Amesema kinachotakiwa kwa mujibu wa sheria ni kuwakamata watuhumiwa wote wa ufisadi, kuwafungulia RB polisi na kisha uchunguzi kufanyika wakati watuhumiwa wakiwa rumande au wakiwa nje kwa dhamana.

Jana Waziri wa Fedha na Uchumi Bw. Mustafa Mkulo alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa aliyekuwa Gavana wa Benki Kuu Bw. Balali ametoweka na hajulikani alipo.

Hata hivyo, taarifa zilizotolewa jana kwa waandishi wa habari na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Ikulu Bw. Salva Rweyemamu, zimedai kuwa hivi sasa, Serikali haina shida na Dk. Balali na kwamba itamtafuta wakati utakapowadia baada ya uchunguzi wa sakata lake kukamilika.

Dk. Balali alipigwa chini na Rais wa Jamhurio ya Muungano wa Tanzania Bw. Jakaya Kikwete baada ya ripoti ya mkaguzi wa hesabu za BOT, kampuni ya ukaguzi ya kimataifa ya Ernst & Young, kubaini kuwa kuna mapesa mengi yametumika visivyo wakati akiiongoza taasisi hiyo.

Kashfa kubwa iliyotikisa nchi na kumfanya Balali apigwe chini na Rais ni ile ya kuchotwa kwa zaidi ya Sh. Bilioni 133 za BOT, ambazo zililipwa isivyo halali kupitia akaunti ya malipo ya madeni ya nje, EPA.
  • SOURCE: Alasiri

Kama hakuna viongozi watakao kuwa upande wa wanchi kwenye hili sakata tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu then miye yangu macho!
 
Back
Top Bottom