MAFISADI waanzisha Operation Migogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MAFISADI waanzisha Operation Migogoro

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kamende, Nov 29, 2009.

 1. Kamende

  Kamende JF-Expert Member

  #1
  Nov 29, 2009
  Joined: Mar 1, 2008
  Messages: 415
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Habari zisizo rasmi ambazo zimepatikana kwa hisani ya wajanja wanusao habari za ndani za serikali, usalama wa Taifa na zile za Chama Cha Mapinduzi zimeanika kuwa mkakati kamambe umeandaliwa wa kupandikiza migogoro ndani ya kambi zinazopambana na MAFISADI.

  Kundi moja la wabunge wa CCM na wafuasi wao ambao wamebainika kushadadia vita dhidi ya MAFISADI wamewekewa mkakati wa kushambuliwa kwa kuharibiwa haiba zao mbele ya jamii na pia kuwaondolea nguvu za kisiasa katika mikoa yao. Ni lazima wawekewe mazingira ya kutochagulika na pia watanyang'anywa nafasi zozote za ushawishi walizonazo.

  Katika mkakati huo CHADEMA imepangiwa mkakati maalum wa kuiweka busy na hata kuisambaratisha. Hii ni kwa lengo la kuiondolea uwezo wa kujipanga dhidi ya MAFISADI katika uchaguzi ujao. Hapa waheshimiwa hawa wanajiaminisha kuwa watapandikiza migogoro ndani ya CHADEMA kila siku. Media itajaa habari za migogoro ya CHADEMA kila siku. Hatimaye UFISADI pekee utakaokuwa ukijadiliwa ni wa CHADEMA. Viongozi wa CHADEMA watalazimishwa kuwa wakijibu shutuma dhidi yao na dhidi ya chama na hivyo hawatakuwa na muda wa kurusha makombora kwa MAFISADI.

  Mkakati mwingine ambao utaunganisha sana mikakati mingine yote ya kundi hili ni ule wa kutumia vyombo vya habari. Magazeti yatajaa habari enezi za propaganda hizi. Kila siku kutafumuliwa mgogoro mmoja baina ya viongozi wa juu wa CCM, Mawaziri, Vyama vingine vya siasa hasa CUF na CHADEMA na pia biashara za mahasimu wa kundi la MAFISADI zitatengenezewa propaganda ya kuzichafua.

  Wakuu hawa watu wana hela nyingi na wako tayari kuzitumia kuimaliza demokrasia ya nchi yetu. Wanazitumia sasa kwa wingi ili waweke mazingira mazuri ya kuzirudisha baada uchaguzi ujao.
  Tuwe macho sana na yanayotokea na yatakayokuwa yakitokea!!!
   
 2. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #2
  Nov 29, 2009
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  wakijatahidi kuilenga CHADEMA. lakini kwasababu tumewang'amua hawatashinda, mimi hawa jamaa wa Usalama wa T aifa naona kama mijitu fulani isio na akili , maana inapambana na wasio tishia ustawi wa Taifa, kweli siwapendi.
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Nov 29, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Mbona kama operesheni hizi zilishaanza kitambo?
   
 4. b

  bnhai JF-Expert Member

  #4
  Nov 29, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha mafisadi wala nini? Vyama vyenyewe vipo hovyo hovyo. Itachukua muda mrefu kuleta mapinduzi ya ukweli. Angalia hii ya juzi, watu wanaongozwa na hisia au watu wachache katika utendaji wao. Tumekuwa tukijadili anguka la CCm lakini muda si mrefu litajadiliwa la CHADEMA kabla la CCM halijafika.
  CHADEMA kuna watu wanajua kuzungumza saana lakini implementation ni zero. Nadhani kuna haja ya kutazama approach. Angalia nguvu ya CHADEMA kwenye operesheni SANGARA then fananisha na matokea ya kura za serikali za mitaa. Hii inatafsiri nini uchaguzi mkuu. Utaona kuwa KUMBE NI NDOTO WALA SI KWELI kuing'oa serikali.
   
 5. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #5
  Nov 29, 2009
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  Usalama wa Taifa hivi ni kumlinda rais tu?
   
 6. P

  Papa Sam Senior Member

  #6
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 102
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Usalama wa taifa yao nikuwatafuta watu wanaoibua mafisadi wanaohatarisha usalama wa nnchi, hawa jamaa bwana,
   
 7. omarilyas

  omarilyas JF-Expert Member

  #7
  Nov 29, 2009
  Joined: Jan 24, 2007
  Messages: 2,127
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hii haina tofauti na ile mentality ya kudai kuwa ujinga, umasikini, migogoro na hata utumwa wa kimawazo wa nchi zetu za kiafrika ni kwa sababu ya historia ya ukoloni na maslahi ya nchi za magharibi. Makada wa CCM wakitumia maneno kama haya mnawaita wajinga na wanaficha mapungufu ya ndani. Sasa siju ninyi mnaoendelea kujidanganya kwa mtindo huohuo tuwaitaje.

  Amkeni acheni kujidanganya kuwa kila kitu kiko sawa na matatizo ndani ya makundi ya masiha wenu yanatokana na maadui wa nje...

  Watanzania wanaweza kuwa wameelemewa na mapungufu ya CCM lakini kamwe sio watu wa kubahatisha na kukimbilia bora mbadala unaoshindwa hata kukubali mapungufu madogomadogo unaowasibu sasa.

  Its time for self reflection na kuacha kulia foul na kukimbilia kulaumu wachawi wa nje hata katika challenges ndogondogo kama hizi....

  Mnaboaaaaaaaaaa

  omarilyas
   
 8. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #8
  Nov 30, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Mkuu mazingira ya uchaguzi wa mitaa kwa jinsi yalivyo andaliwa hayawezi kuchukuliwa kama kipimo cnja uchaguzo ujao .Serikali na CCM wametumia kila mbibu a uchafu wote kushinda ili kuonyesha kwamba wana nguvu .Mkuu huu si mfano kwa yanap tegemewa. Serikali imejaa uoga na naharibu chaguzi. Kweli uliona uchaguzi mtu anaenda kuandika jina la mtu na hata picha wala nini za wagombea hazikiwepo ?Rudi tena uangalie uhalisia
   
 9. Sir R

  Sir R JF-Expert Member

  #9
  Nov 30, 2009
  Joined: Oct 23, 2009
  Messages: 2,177
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Mkuu uchaguzi wa serikali za mitaa haukufaa kuwa kipimo sahihi kwani kulikuwa na ukiukaji mwingi maeneo mengi. kuna maeneo unashindwa kutengannisha wasimamizi wa uchaguzi na makada wa CCM kwani kila walichokifanya ni kwa maslahi ya chama tawala (CCM)

  Hivyo tusilaumu vyama vya upinzani, tuwaunge mkono ili kuleta mabaliko ya kweli.

  Tafakari.
   
 10. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #10
  Nov 30, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hii kama ni kweli basi vita ni kali. Kama hicho kikundi kinaweza kujipanga na kushambulia vyama vya upinzani na wakati huo huo sehemu ya wabunge wa chama chao basi tuaamini kwamba watu hawa wamejipanga na wanao mtaji wa kutosha, (Mechi moja kucheza na timu mbili sio mchezo).

  Swali la kizalendo linalonisumbua ni kwa nini mitaji mikubwa namna hii isitumike kwa maendeleo ya jamii na badala yake inatumika kwa ajili ya kitu ambacho ni maslahi ya watu wachache tu?

  TANZANIA NCHI YANGU, TATIZO NININI?
   
 11. b

  bnhai JF-Expert Member

  #11
  Nov 30, 2009
  Joined: Jul 12, 2009
  Messages: 2,208
  Likes Received: 1,373
  Trophy Points: 280
  Nini kipimo sahihi cha achievement za Upinzani? Hivi tukifanya analysis na kuchukua performance ya upinzani in aggregate yaani km variable moja tukafanyia tathmini kuanzia 1995 mpaka sasa. Wakati upi kuna mafanikio? Binafsi naona mzoroto mtupu.
   
Loading...