Mafisadi na Wahujumu Uchumi Wasishitakiwe, Wanyongwe

MPadmire

JF-Expert Member
Mar 7, 2006
3,928
3,225
Kuna faida gani kwa Mafisadi na Wahujumu uchumi kushitakiwa?

Watanzania/Wananchi wanapata faida gani kwa mafisadi au wahujumu uchumi kushitakiwa?

Isitoshe kodi za Wananchi zinatumika kuendesha kesi ambazo hatimae serikali hushindwa.

Ushauri wangu ni kuchukua hela zote kwenye akaunti zao na kutaifisha mali zote.
hata kama ameandika mali hizo au hizo akaunti kwa majina ya ndugu na marafiki. Halafu hao wanaomiliki walete maelezo kuwa hizo hela wamepataje, Biashara zipi wamefanya,statements of yearly accounts na kodi zipi wamelipa TRA.

Pia wakati uchunguzi unafanya, inatakiwa wawekwe kuzuizini (detention) ili kutoa mwanga zaidi wa kujua ukweli.

Serikali inajua nani ana shs ngapi kwenye benki ipi ...Through BOT.

Pia kuna usalama wa taifa, kuna Takukuru, mahakama,polisi n.k

Ni usanii mtupu kumfunga watu kama Liyumba au Yona na wengine wakati umewaachie hela zote walizoiba.

Au Kuanzisha tume ya ukweli na upatanishi ili hao wezi warudishe hela kiasi na waachiwe kidogo.

Why was it possible with Sokoine and Son of peasant NOOOO?

Why possible to Kigoma Ali Malima?
 
Fisadi ni nani kwa maana gazeti la Tanzania Daima leo linawatetea sana mapacha watatu je hamuoni kwamba cdm ndio inajichimbia kaburi
 
Mafisadi wote washughulikiwe, wafilisiwe. Hao Mapacha wa 3 hawatetewi na CDM.

CDM ndo walietaja hao mapacha 3 pamoja na wengine hadi list of shame ikafikia 11
 
Tukiwafumbia macho walarushwa, wahujumu nchi na uchumi ipo siku watatutia vidole machoni: wanyongwe!

Tatizo kubwa linalochangia uozo wote huo ulioainisha ni kutokuwa na viongozi wazalendo.

Tuna viongozi wengi ambao wanajali zaidi maendeleo binafsi badala ya maendeleo ya wananchi na taifa kwa jumla.

Wananchi tuna nafasi kubwa ya kuleta mabadiliko wakati wa uchaguzi kwa kutowapigia kura viongozi ambao wameshatuonyesha wazi kuwa hawajali maslahi yetu na ya taifa kwa ujumla!
 
Wanatengeneza NGO za kisiasa kwa kujinadi kuwa wazalendo wa nchii hii na kutangaza kutawala chama milele
 
Tukiwafumbia macho walarushwa, wahujumu nchi na uchumi ipo siku watatutia vidole machoni: wanyongwe!

Mbona wameshaanza kututia vidole!!! Hukumsikiliza Chenge alipokuwa anahitimisha hotuba ya kamati ya bajeti bungeni juzi? Ati serikali isitishe ajira na kodi ya line za simu ni nzuri!!! Huku madini yetu yanachotwa na wanaojiita wawekezaji, malipo ya bill za umeme yakiishia kugharamia capacity charge na misamaha ya kodi kibao
.
 
Nani wa kuanza kumfunga paka kengele, vita ijayo ni baina ya matajiri na masikini, masikin siku zote ndio hukomboa nchi iliyozama
 
Tukiwafumbia macho walarushwa, wahujumu nchi na uchumi ipo siku watatutia vidole machoni: wanyongwe!

Ni matarajio na matamanio ya wengi ,lakini hatujawahi kuona hata fisadi papa mmoja aliefikishwa mahakamani sembuse kunyongwa?.Haya mawazo yako yalitakiwa kuingizwa ktk katiba mpya lakini nayo imeshachakachuliwa kwa baadhi ya mambo kufanywa kinyume na matarajio ya wengi.Jitahidi na ufanye kazi kw bidii ili ujipatie ugali wako wa kila siku,haya mengine achana nayo maana makaburu hawatakawia kukung'oa kucha bila ganzi.
 
Kila uchao tunashuhudia watu wakikamatwa na nyara za serikali,madini yetu, tembo wetu, twiga wetu na kwa ujumla rasilimali zetu. Wanaokamatwa nazo ni majangili wanawauwa wanyama wetu kinyume na sheria. Sasa wachina ndio vinara. Ina maana hawa wachina tuliowakumbatia miaka mingi hivi, hii ndio kazi yao? Kumbe ni urafiki wa kinafki?

Napaza sauti: nasema kwamba, yeyote anayekamatwa na nyara za serikali ipitishwe sheria kali sana ANYONGWE HADI KUFA.
cc.
rais kikwete
spika anne samamba makinda
wizara ya mali asili na utalii
watanzania wote
 
Sijui kukamatwa unamaanisha nini? Ila kwa mapendekezo hayo nadhani Katibu Mkuu angekuwa kwenye usingizi wa milele muda huu. Well, wachina wanaonekana kuwa tatizo kuu nchi hii hasa linapokuja suala la UFISADI - rushwa, ujangili, na mengineyo. Hawa jamaa wanapaswa kutazamwa kwa jicho la tatu.
 
Kila uchao tunashuhudia watu wakikamatwa na nyara za serikali,madini yetu, tembo wetu, twiga wetu na kwa ujumla rasilimali zetu. Wanaokamatwa nazo ni majangili wanawauwa wanyama wetu kinyume na sheria. Sasa wachina ndio vinara. Ina maana hawa wachina tuliowakumbatia miaka mingi hivi, hii ndio kazi yao? Kumbe ni urafiki wa kinafki?

Napaza sauti: nasema kwamba, yeyote anayekamatwa na nyara za serikali ipitishwe sheria kali sana ANYONGWE HADI KUFA.
cc.
rais kikwete
spika anne samamba makinda
wizara ya mali asili na utalii
watanzania wote

We Ifweroo hujui kuwa posho na mshahara wako pale Lumumba inatokana na kuuawa kwa wanyama Tembo na madawa ya kulevya? Mabosi wako wakinyongwa mshahara utapa wapi? fikiria kwanza kabla ya kutokota....
 
We Ifweroo hujui kuwa posho na mshahara wako pale Lumumba inatokana na kuuawa kwa wanyama Tembo na madawa ya kulevya? Mabosi wako wakinyongwa mshahara utapa wapi? fikiria kwanza kabla ya kutokota....
Mkuu, hasira zako ni za ovyo na ni kijinga. Hoja yako ni dhaifu mno. Watu tunazungumzia mambo ya maana
 
Hiyo kazi ya kuwanyonga nitaomba niajiliwe mimi...nikimaliza kunyonga nasaga kabisa na miili yao natupa baharini samaki nao wafaidi.
 
Mkuu, hasira zako ni za ovyo na ni kijinga. Hoja yako ni dhaifu mno. Watu tunazungumzia mambo ya maana
Huna uwezo wa kufikiria umbali wa pua yako! ukizidisha huwezi kuzidi umbali wa tumbo lako! Ndo maana wenzako tunakuona mchumia tumbo! Yaani wewe siku zote umekuwa ukishangilia wananchi kuuawa kwa mabomu, umekuwa ukishanglia madini yetu kumilikiwa na wageni kwa 100%, Umekuwa ukifurahia waananchi kukosa huduma muhimu za kijamii shule, maji, umeme, barabara. umekuwa ukishangilia kupanda kwa gharama za maisha kwa watanzania, umekuwa ukishangilia umeme kupandishwa bei... tukueleweje eti leo hii unajifanya unauchungu na ujangili unaofanywa kwenye Tenbo na wanyama wetu! Limumba wamwepunguza posho au?...
 
Back
Top Bottom