Nionyeshe kiongozi au mtumishi hata mmoja aliyewahi kuwajibishwa na utawala wa Rais Samia kwa ubadhilifu, ufisadi au matumizi mabaya ya ofisi

yvegenc prymacov

JF-Expert Member
Jan 22, 2023
1,510
1,901
Salute,

Tangu raisi Samia aingie madarakani katika awamu yake ya sita, baada ya hayati Magufuli kuwa ametangulia mbele ya haki, ni kiongozi gani au mtumishi gani amewahi kuwajibishwa kwa ufisadi?

Uzembe? Uzembe? Au ubadhirifu wa Mali ya umma? Naomba mnionyeshe. HAKUNA. Badala yake mafisadi, wahujumu uchumi na wabadhilifu wa Mali ya umma wanalindwa, na wale waliokuwa wamewajibishwa katika utawala wa Hayati Magufuli wanarudishiwa hela zao na mafisadi yoote wamerudishwa kazini.

Rais wa nchi ndio kila kitu kwenye nchi, ukitaka ujue rais ni mtu wa aina gani tizama watu waliomzunguka.

Tutawalaumu mawaziri, tatizo lipo kwa namba moja.
 
Binafsi, tena kwa utani utani, ni wale wote walioitwa "Stupid" yani wamepigwa kichapo cha kiganja!

Isitoshe wapo wale wanaodai "kutumbuliwa" ulikuwa ni uovu sasa sijui wataita nini haya ya SSH kuita mafisadi "Stupid" inifrontoofu televisheni??(kwa lafudhi fulani)

Hawa majaamaa wanakataa ufisadi,wanakataa panishimenti ya aina yeyote ile!
Nina wasiwasi hawa majamaa ndio hao hao tu, ni mafisadi, na wanaokataa adhabu yeyote juu yao! Hizi na janja janja zao humu mitandaoni, kweli vile, ipo siku.
.....sitegemei waje na....

"HATA MMOJA ALIYEWAHI KUWAJIBISHWA NA UTAWALA WA RAIS SSH KWA UBADHILIFU,UFISADI AU MATUMIZI MABAYA YA OFISI...."​

Hawa ni wa Kunyongwa hadharani tu!
 
Salute,Tangu raisi samia suruhu hassan aingie madarakani ktk awamu yake ya sita,baada ya jpm kuwa ametangulia mbele ya haki,ni kiongozi gn au mtumishi gn amewahi kuwajibishwa kwa ufisadi?, uzembe?, uzembe?,au ubadhirifu wa Mali ya umma?. Naomba mnionyeshe.HAKUNA. badara yake mafisadi,wahujumu uchumi na waadilifu wa Mali ya umma wanalindwa,na wale waliokuwa wamewajibishwa ktk utawala wa jpm wanarudishiwa hela zao.na mafisadi yoote wamerudishwa kazini.

Rais wa nchi ndio kila kitu kwenye nchi,ukitaka ujue rais ni mtu wa aina gn,tizama watu waliomzunguka.

Tutawalaumu mawaziri,tatizo lipo kwa namba moja.
Mada yako ni ya msingi sana; lakini itanilazimu nami nichangie kwa ushahidi ninaoujua.

Tokea mama ashike madaraka ya nchi amewaondoa viongozi mbalimbali katika nyadhifa zao.
Je, tunaweza kuwahesabu hawa kama akina Profesa wa Jalalani, akina Lukuvi, akina Kalemani na wengine kuwa ndio hao hao mama aliopambana nao kwa sababu za ufujaji wa mali za wananchi?

Vinginevyo, basi tuambiwe hawa waliondolewa kwenye nafasi zao kwa sababu zipi?

Hawa na wengine wengi waliokwishaondolewa ndio ushahidi wangu wa kujibu mada yako.

Kama hukubaliani nami, basi nieleze sababu za hawa watu kuondolewa katika nafasi zao.
 
Rais ssh wakati anawaondoa akina kalemani,lukuvi,kabudi,hakutaja ufisadi wowote walioufanya,isipokuwa,alikuwa anapanga tu serikali yake.na alisema watapangiwa kazi nyingine.
 
Rais ssh wakati anawaondoa akina kalemani,lukuvi,kabudi,hakutaja ufisadi wowote walioufanya,isipokuwa,alikuwa anapanga tu serikali yake.na alisema watapangiwa kazi nyingine.
Dah!

Basi elewa kwamba sababu ndiyo hiyo mkuu wangu Yvegenc prymacov.

Kama hakusema sababu za kuwaondoa, basi chukua jibu hilo kwa kujibu mada yako.

Kwa msingi huo, basi, inaelekea mama kapambana sana; maanake amekwishawaondoa watu kadhaa tangia ashike madaraka.

Sasa hawa wanaozuka upya, na bado wanaendelea kuwemo serikalini, inawezekana wao makosa yao ni mepesi sana na hayahusiani kabisa na hujuma ulizozijengea hoja wewe!

Mama anapambana sana. Waliokuwa wanazuiwa na urefu wa kamba zao sasa kawaweka huru bila kamba!
 
Salute,

Tangu raisi Samia aingie madarakani katika awamu yake ya sita, baada ya hayati Magufuli kuwa ametangulia mbele ya haki, ni kiongozi gani au mtumishi gani amewahi kuwajibishwa kwa ufisadi?

Uzembe? Uzembe? Au ubadhirifu wa Mali ya umma? Naomba mnionyeshe. HAKUNA. Badala yake mafisadi, wahujumu uchumi na wabadhilifu wa Mali ya umma wanalindwa, na wale waliokuwa wamewajibishwa katika utawala wa Hayati Magufuli wanarudishiwa hela zao na mafisadi yoote wamerudishwa kazini.

Rais wa nchi ndio kila kitu kwenye nchi, ukitaka ujue rais ni mtu wa aina gani tizama watu waliomzunguka.

Tutawalaumu mawaziri, tatizo lipo kwa namba moja.
Waliowahi kuwajibishwa ni wale mawaziri kwa sababu ya kujipanga 2025
 
Back
Top Bottom