Mafisadi kumng'oa mbunge Mahiri 2010.... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mafisadi kumng'oa mbunge Mahiri 2010....

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Bill, Apr 16, 2009.

 1. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #1
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  Katika hali inayoonyesha kuwa ni JITIHADA ZA KUFIFISHA MOTO WA VITA YA UFISADI nchini, mafisadi wanajipanga kumng'oa Mbunge wa Kishapu ndugu Fredrick Tungu Mpendazoe. Mpaka sasa Mafisadi wakiongozwa na Kinara wao wao Rostam wameanza jitihada za kumchafua. Jumamosi iliandikwa katika Gazeti la Mtanzania kuwa Mpendazoe anatengeza makundi jimboni, jana Jumatano gazeti la Majira limerudia habari hiyo. Mtu anayeandaliwa na Mafisadi kuchukua nafasi hiyo ni Katibu mkuu wa UVCCM ndugu Shigela ambaye ana baraka zote za Mafisadi ikisemakana na Mkuu mwenyewe Mr Handsome.

  Kwa hatua hii bado vita dhidi ya ufisadi ni ngumu na ndugu wana JF tuchangie kuona ni jinsi gani Mpiganaji mwenzetu ndugu FT Mpendazoe atabaki kuendeleza moto wa ufisadi
   
 2. M

  Mfumwa JF-Expert Member

  #2
  Apr 16, 2009
  Joined: Aug 29, 2008
  Messages: 1,456
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi kupingana na mtu anayepigana na ufisadi ni kuandaliwa na Mafisadi?, Ubunge ni miaka 5, ikimalizika hiyo yoyote yuko na haki ya kugombea. Haimaanishi kuwa mtu akisimama kuwasema mafisadi basi asipingwe. Hakuna mwenye mkataba wa kuwa mbunge maisha. Kweli wengi watakimbilia kujiweka kwa wananchi ili waonewe huruma kwa kusema wanaopambana nao wametumwa na mafisadi.

  Tanzania mgombea binafsi haruhusiwi, wote wanatakiwa kupitia kwa vyama vilivyosajiliwa. Sasa kama mtu ana nia ya kugombea, na ni CCM kwa nini asigombee, aogope kusemwa katumwa na mafisadi. Hiyo ni haki ya mtu yoyote, raia wa Tanzania aliyetimiza masharti ya kugombea. Tusianze kubagua watu kwa kuwaita wametumwa na mafisadi, ni kuwanyima haki zao zilizoainishwa na katiba.
   
 3. Nduka

  Nduka JF-Expert Member

  #3
  Apr 16, 2009
  Joined: Dec 3, 2008
  Messages: 8,483
  Likes Received: 765
  Trophy Points: 280
  huku ni kutafuta huruma za wananchi kwa kuanza kusingizia mafisadi wanataka kuning'oa. wabunge wengi wameshindwa kutekeleza majukumu yao kwa wananchi wakaona wadandia bega la ufisadi wakidhani litawatoa sasa wameona wananchi wamestukia ujanja wao wanaanza visingizio.RA kishapu wapi na wapi bana nenda kamshauri atafute strategy nyingine hakuna kudandia hoja hapa..AAAAGGGGHHHRRRRRRRR
   
 4. M

  Mtanzania JF-Expert Member

  #4
  Apr 16, 2009
  Joined: May 4, 2006
  Messages: 4,818
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kuna wajanja wameanza kutumia vita vya ufisadi kama njia ya kutetea majimbo yao 2010. Miaka mitano ikiisha kila mtu ana haki sawa ya kugombea hayo majimbo. Wakati ukifika wabunge wa sasa wawaeleze wananchi juu ya mafanikio ya ahadi zao mbalimbali.

  Kutumia vita na mafisadi kama njia ya kuonewa huruma na wananchi naona muda ukifika haitawasaidia sana. Kwanza hata wenyewe utakuta wengi wao waliingia kwa ufisadi bungeni baada ya kuhonga wajumbe. Wanachobiashana hapa ni nani fisadi zaidi ya mwingine.

  Kupigana na mafisadi itakuwa sifa moja tu kati ya sifa nyingi au mafanikio mengi ambayo mbunge atatakiwa kuwa amefanya.
   
 5. Fidel80

  Fidel80 JF-Expert Member

  #5
  Apr 16, 2009
  Joined: May 3, 2008
  Messages: 21,976
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 145
  Na mimi najiandaa kumng'oa Yono Kevela kuleeeeeee Njombe sijui mtasema ufisadi....na kuna jamaa angu nae anamdondosha mtu mzima Jackson Makwete hawa wabunge wamekuwa mzigo kwa sisi wananchi hawana chao 2010...
  Msije mkasema nimetumwa na mafisadi kama hawa mmewahi waskia wanapigana vita ya ufisadi basi nitakuwa nimetumwa lakini kama hamjawahi sikia basi ndo hivyo hawa bungeni hawarudi 2010.
   
 6. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #6
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Nadhani serikali iliporidhia uanzishwaji wa COSOTA iliona mbali. Nawashauri wabunge wakasajili majimbo yao pale ili wapate hati za hakimiliki za majimbo yao ya uchaguzi (kudadadeki)
  Huu ujuha wa kulalamika kung'olewa majimboni ni wendawazimu wa kifisadi pia. Kama kazi ni kupiga kelele bila kuleta maendeleo viable basi ni vyema ukakaa pembeni kulinda heshima na kuwapisha wengine. la ingia vitani kama wanavyotaka kuingia vitani wengine.

  Sipendi mafisadi ila pia sivutiwi na viongozi ving'ang'anizi kana kwamba walizaliwa watawale maisha. halafu hawa hawa wanapewa uwaziri baadaye mnadhani atawajibika akivurunda?? angalia kuna wabunge wengi sana pale dar wala hawana habari na majimbo yao na sana sana utakuta wanaenda jimboni pale tu anapoingia fisi mwenzake mwenye nia ya kumpora jimbo. shenzi taipu. ujinga huu, uhuni huu, siungi mkono mia kwa mia
   
 7. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #7
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwaka 2010, Shigela atagombea kupitia CCM na Mpendazoe atagombea kupitia CHADEMA. Mshindi atakuwa nani hapo? Mnaojua siasa za Kishapu hebu tuelezeni chapu chapu. Au wote ni uchafu mtupu?

  SM
   
 8. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #8
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Wakipata ubunge tu wanayakimbia majimbo yao, halafu wanataka kusingizia mafisadi wanatayarisha mtu, nonesense!

  - Ni majimbo mawili tu ambayo ninajua for a fact kwamba mafisadi wanayawinda nayo ni ya Sitta na Mama Makinda, kwa sababu hawa ndio kikwazo chao bungeni, kama unaelewa vizuri siasa za bongo then uanjau wkamba tatizo la mafisadi sio media wala wananchi, ila wanaumizwa bungeni na hawa viongozi wawili tu, na ndio wamewakamia sana, lakini wengine waache magirini hawana record tu sasa wasidanganye umma!


  FMES
   
 9. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #9
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Heheeheheh Jamani na mimi nigombee nini? Masha watch out I am coming....looh!
   
 10. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #10
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Mzee wa sauti ZA umeme heshima mkuu.
  Mimi nadhani kuna haja ya kubehua mfumo mbovu uliopo na kuleta mfumo workable.
  Kwanza mawaziri wasiwe wabunge, pili katiba itamke majina ya wizara ili kuondoa kadhia ya uundwaji holela wa wizara. tatu waziri mkuu awe mtendaji na nafasi ya raisi iwe ni mpepeaji i mean ceremonial, nne posho za wabunge zipunguzwe kulinganisha mfumo wa mishahara ya serikali na walipe kodi kwa kila senti ya posho inayowadondokea. tano ukabila na udini viwekewe penal code zake. sita sheria ya usajili wa vyama iweke ukomo wa wagombea uraisi walioshindwa kupata popular vote ili kutoa nafasi kwa wengine kuingia ktk soko la kura. saba gavana wa benki kuu na wakurugenzi wa idara nyeti za serikali wapitishwe kwa kura bungeni ktk kuunga au kukataliwa uteuzi wao. nane Mahakama isiwe idara ktk wizara ya sheria na katiba, ipewe nafasi yake sawa ya mhimili wa dola pia utafutwe utaratibu muafaka wa kumpata na kumwapisha jaji mkuu. tisa sheria ya maadili ya viongozi wa umma irekebishwe ili kuchechemiza uwajibikaji zaidi. kumi kiongozi yeyote wa serikali ajivue au avuliwe madaraka yake YOTE ktk chama alichotoka ili awajibike na kutoa nguvu ya accountability....
  Nina mengi kichwani ila nimeyawekea hakimiliki ili wasije wakaiga na kudandia hoja kwa nchani.
   
 11. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #11
  Apr 16, 2009
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 69
  Trophy Points: 0
  - Mkuu wangu maneno haya ni mazito sana, lakini wabongo tunashidnwa kuelewa one thing, kwamba CCM na serikali yake hawana sababu yoyote ya kufanya mabadiliko iwapo hakuna political threat ya kuwaondoa kwa kura, unakumbuka wananchi tulipoanza kuwarushia mawe na kuwazomea, we were almost there kwa sababu walianza kuchanganyikiwa na kuanza kupelekana Kisutu, lakini tulipoacha tu na wao wakarudia walipokuwa mwanzoni yaani walipo sasa. Inasikitisha sana!

  - Anyways, sitakuwa na access ya mtandao kwa muda kidogo kwa hiyo tutaonana tena soon!

  Respect.

  FMES!
   
 12. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #12
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Baharia unachochea vurugu hapa, hujui nchi yetu ni ya amani na utulivu....am kidding
   
 13. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #13
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani nani alimuambia huyo Mpendazoe kuwa hilo jimbo ni mali yake? Yaani yeye akwia Mbunge watu wengine hawaruhusiwi kuja kugombea unapofika wakati wa uchaguzi!
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Tuiombee nchi yetu halafu tufe nayo kimya kimya moyoni bila kusema kitu maana WAKIKUSHIKA wenyewe hawachagui pa kupiga
   
 15. TreasureFred

  TreasureFred Member

  #15
  Apr 16, 2009
  Joined: Feb 25, 2008
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wana jf ni jambo la ajabu hii inayoitwa vita dhidi ya ufisadi kuwa chaka la kimbilio la kila mtu na ambao wameshindwa ku perfome wakibanwa mbavu wanakimbilia kuwa mafisadi wanataka kuwa ondoa.

  Wana jf kwanza nashauri hii vita isiwe jambo ambalo lifunge demokrasia nilipata bahati nikatembelea wilaya moja inaitwa nzega nikiwa pale nilienda kikazi ktk halmashauri ya wilaya hiyo kwa siku 15 nilizokaa pale niliweza kuongea na watu zaidi ya 20 watu,swali langu lilkuwa ikiwa leo unaambiwa chagua mbunge wako utamchaguwa nani?

  Nilifika nikiwa najuwa majina mawili lucas selelii na hussein bashe ambae nilisoma hapa jf ikisemekana nae anapelekwa na mafisadi kumuondoa selelii,nikitaka kujiridhisha, kati ya hao 20, 14 walisema watamchagua bashe, watu 3 walisema watamchagua selelii na mmoja alikuwa wazi alisema hategemei kuchagua mtu wa ccm.

  Nikafanya uchunguzi kwa wafanyakazi wa halamshauri ambao nilikuwa nafanya nao kazi ktk idara ya uhasibu 70% walisema selelii hana nafasi.

  Ktk bar n hoteli ukisikiliza mazungumzo huyu mtu ambae anasema mafisadi wanamdhoofisha hana vote,sasa hapa jf tujiulize je kila anaepambana na mafisadi ametekelea wajibu wake ktk eneo lake?.

  Nilifika mwaka jana halamshauri ya kishapu mpendazoe ni kiongozi ambae ktk siasa za kitaifa amefanya kazi,tatizo ni ktk jimbo lake hajafanya jambo lolote,nachoshauri jf tusiruhusu vita hii ya ufisadi ikawa kimbilio la watu walioshindwa kutekeleza majukumu yao
   
 16. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #16
  Apr 16, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ..kwa nini nisikuunge mkono?
   
 17. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #17
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,171
  Likes Received: 1,256
  Trophy Points: 280
  What are the roles of Wabunge? Pamoja na kuwakilisha wananchi Jimboni kwake, what else! Kupeleka maendeleo kwa fedha yao ya mfukoni?
   
 18. O

  Ogah JF-Expert Member

  #18
  Apr 16, 2009
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 6,229
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Hii ni dharau kwa wananchi.....ikimaanisha eti wananchi hawajui namna ya kuchagua mbunge wao!......huo umahiri kaupata wapi au kapewa na nani au alitunukiwa lini?

  Ndio maana kuna umuhimu wa......kuweka term limit ya ubunge....i.e. maximum iwe terms mbili.....maana kuna watu wameshajiona wao ni "Miungu Watu"......halafu wanafikiri wakija hapa JF tutawapa support kichwa kichwa......HAKUNA hiyo......kama mmefanya mliyotumwa na wananchi why worry?.......damn!
   
 19. k

  kela72 Senior Member

  #19
  Apr 16, 2009
  Joined: May 5, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani tusije tukanogewa kuongea lugha moja wooote humu ndani! nadhani mtoa hoja kasema pia bwana Mpendazoe anachafuliwa kuambiwa 'eti' anatengeneza makundi. Gazeti kama mtanzania ambalo mara nyingi limetumiwa na mmliki wake kuendeleza uma-kundi leo hii limekuwa linapinga tabia hii kirahisirahisi tu? Isije tukaingizwa kwenye mkumbo wa kuunga mkono mambo ambayo wengi wetu tumekuwa tukiyapinga kwa nguvuzetu zote! Hebu fikiri, kwa mfano ikawa ni kweli kuna njama hizo,..... sisi tutakuwa tumecheza mechi upande gani?
   
 20. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #20
  Apr 16, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mishahara na posho yao vipunguzwe tu na kuwekwa kima cha chini kabisa tuone kama watakimbilia ,maana kila mtu itambidi athamini kile alichokisomea ,utamkuta mtu serikali imetoa gharama za kumfundisha uinjinia na udakitari na elimu zingine za ufundi akirudi anaenda kutafuta mambo ya siasa na kujiunga huko na ile hela yote aliyofundishiwa inakuwa imepotea bila kuonekana matunda yake ,ni wizi tu.
   
Loading...