Mafanikio ya mwanamuziki Burna Boy, nini tunajifunza?

kamikaze

JF-Expert Member
Jan 25, 2011
422
610
Huyu jamaa kwa kipindi kifupi ameweza kuwa mwanamuziki maarufu na mwenye mafanikio duniani. Kafanya shows nyingi, kajaza watu kwenye show zake na mengineo mengi.

Je, siri ya kufanikiwa kwake ni Kipaji au menejimenti inayojielewa? Miaka kama miwili au mitatu alifanya ngoma na Diamond pamoja na Harmonise lakini kwa sasa ukiwalinganisha unaona kabisa jamaa kawaacha mbali Diamond pamoja na Harmonise.

Na show yake kubwa ijayo ataperform kwenye fainali ya champions league mwaka huu. Je, nini wanamuziki wetu wanatakiwa kukifanya kuweza kupata mafanikio haya? Maana naona wanigeria wako mbali sana. Mwaka jana Davido aliperfom kwenye fainali za world cup, Tems alishinda tuzo ya grammy na wengineo wanafanya vizuri kimataifa. Nadhani mawazo yetu yanaweza kusaidia wasanii wetu kukua zaidi kimataifa.
 
Tatizo ni lugha, hawa jamaa wanaimba sana kiingereza kwa hivyo wanapata wasikilizaji wengi, tofauti na Diamond/Harmonize nyimbo zao nyingi ni kwa kiswahili. Kuna wimbo Diamond aliimba na Davido - number 1, huo hata kwenye ma party ya wa west african ulikuwa unawekwa sana sio shauri ya Davido bali ni shauri ya lugha. Wabadilike sasa waanze kuimba na nyimbo kwa kiingereza sasa.
 
Mafanikio ya Nigeria sio ya mtu mmoja mmoja bali wenzenu wanapendana wasanii wanasaidiana ,hamna majungu chuki na wivu kwa wasanii waliopo juu, mwisho wana SYSTEM nzuri ya kuendesha mziki wao ambao una waunganisha washikadau wote wawe kitu kimoja. Ndio maana leo unamuona Asake,Rema, Fireboy nk wanawika sababu mfumo upo wa kuwabeba.
 
Back
Top Bottom