Maeneo ya makaburi yamefurika...

Maeneo ya makaburi yamefurika...

Wazo zuri sana mkuu

Hata Mimi huwa nafikilia hivyo

Makaburi ya kinondoni yameshikilia eneo kubwa ambalo lingefanyiwa masuala ya msingi

Wajenge trade center ya kibabe or ma malls or flats za kutosha



Sent using Jamii Forums mobile app
Itabidi eneo litakaswe kwanza maana itakuwa pamejengwa juu ya yalipokuwa makazi ya wafu. Mshanajr tufafanulie kuhusu ujenzi unaotabiriwa. Hautaleta vurugu?
 
Tuhamie kwenye cremation (kuchoma moto), ni salama zaidi kiafya na mazishi hayachukui nafasi kubwa. Pia unaweza ukamwaka majivu mtoni au baharini bila kujenga kaburi lolote.
Umetoa wazo zuri lakini kwa sasa bado hatujafikia hapo, tanzania kuna aridhi ya kutosha hatujakosa pa kuzika watu hadi tuwachome yaani hata tukifa wote kwa siku moja bado aridhi itabaki kubwa sana, pia si utamaduni wa waafrika kuchoma maiti kama njia ya kuzika

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wazo zuri sana la kuchoma miili. Tatizo hapa Tz mbunge wa upande mmoja akisema "sasa miili iwe inachomwa", upande mwingine watasema ni aibu, tamaduni haziruhusu mpaka itaanzishwa Umoja wa Kupinga Uchomaji Maiti(tafadhari usiweke initials) Siasa kila sehemu.
 
Sisi wachaga ata ufie wapi home nazikwa pale nyumba kaburi linajengewa vizuri shamba akuna wakulisumbua kaburi wala kuamisha mifupa yangu huku mjini kila siku mifupa inaamishwa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilikuwa Kinondoni hivi karibuni kwa ajili ya MAZISHI ya rafiki yangu Seth hakika hali sio nzuri...hakuna nafasi kabisa hata sehem walipomzika huyu rafiki yangu ni finyu mno...Serikali inabidi ifanye uamuzi wa Busara kutenga maeneo mengine kwa ajili ya shughuli hii nyeti kwetu sisi binadamu..

Sent using Jamii Forums mobile app
Tena pale ni makaburi ya familia walipanunua muda mrefu sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwenye master plan ya jiji inaonesha kuwa eneo jipya la makaburi liko Mabwepande. Wawalipe fidia watu wahame ili tuanze kuzikwa huko!
Au wachukue eneo walilomnyang'anya Sumaye ligeuzwe kuwa makaburi mapya...
 
Back
Top Bottom