Baadhi ya vijiji ukifika utadhani unaingia mjini kutokana na umeme.Jamaa wanajenga nyumba za matofali ya kuchoma na bati kila sehemu.Yaani karibu wanafuta nyumba za nyasi.Barabara ya Kigoma - Uvinza- Tabora sasa ni ya lami(daraja la Kikwete kwenye mto Malagarasi ni muujiza).
Waha wanasafirisha ndizi kwenda Tabora kama kazi.Kigoma sasa imo kwenye big 6 katika kuzalisha zao la mahindi.Shule za sekondari za kata kila kona.Kigoma hawajawahi kuomba chakula cha msaada miaka mingi iliyopita kama siyo hapana kabisa.Aidha nimeshuhudia vipaji vikuu vya kuimba sijawahi kutegemea.
Vijamaa vina maumbo madogo lakini vinaimba balaa.Tatizo la hawa Jamaa ni ubishi,japokuwa ukiwasikiliza kwa makini wana hoja.Ukibishana na Muha Hata kama ni darasa la 4 jipange sawa sawa.Kama huamini hudhuria kwenye vikao vyao vya Baraza la .madiwani.
Kimsingi Kigoma nimeshuhudia maendeleo makubwa ambayo sikuyatarajia.Hongera serikali.Jitahidini kumalizia barabara ya Kigoma Nyakanazi.KIGOMA YA SASA YASONGA MBELE.