Uchaguzi 2020 Hongera Dkt. Magufuli kwa ushindi wa kishindo. Tuliyoyaona kwenye kampeni tujifunze

Team JPM

JF-Expert Member
Nov 11, 2018
1,074
1,608
Nichukue Fursa Hii kukupongeza Dokta John Joseph Pombe Magufuli kwa ushindi wa Kishindo wa 84% ya kura zote. Nikupe pole kwa uchovu wa hekaheka za kampeni kwa Siku 60 wakati pia ukitekeleza majukumu ya Urais.

Niwashukuru pia wananchi kwa kukuamini na kukupatia awamu ya pili ya miaka mitano, ahsanteni sana. Katika kipindi chote cha kampeni tumeweza kupita kuomba kura katika makundi mbalimbali, kila kundi liliahidi kukupigia kura kwa matumaini ya kutatuliwa kero zao ambazo ni pamoja na:

1. Tulipopita nyumba kwa nyumba Wananchi walisema wanahitaji huduma bora za afya, usafiri, maji na Elimu. Mfano kule Kigoma tumeona kuna tatizo la usafiri wa Meli, na barabara zao sio nzuri. Rorya huduma ya maji safi na salama sio nzuri, sawa na Dodoma. Tunahitaji msukumo mkubwa katika maji. Kwa upande wa afya, wananchi wengi hawana bima za afya.

2. Tulipoomba kura kwa wakulima, Wakulima walituambia hawana masoko ya uhakika kwa mazao yao ya chakula na biashara na wengi wanapunjwa na vyama vya ushirika katika bei za mazao. Jicho Kali linahitajika kumkomboa mkulima mfano katika zao la korosho, pamba na mbaazi.

3. Tulipoomba kura kwa Watumishi wote wa umma, kilio chao kilikuwa maslahi duni. Tulipowaendea watumishi sekta binafsi nao walihitaji nyongeza ya mshahara, malimbikizo na kupandishwa vyeo. Ukiwaneemesha watumishi wa umma kama ulivyoahidi, uweke utaratibu kwa sekta binafsi hasa Elimu, afya na ujenzi ili nako waboreshewe maslahi.

4. Tulipoomba kura kwa wanavyuo, walilalamikia Makato ya bodi ya mikopo 15% kwamba ni makubwa mno hivyo sheria irekebishwe ili marejesho yawe 5-7% na retention fee ifutwe maana ni janga kwa wakopaji.

5. Tuliwaendea wafanyabiashara watupatie kura, wao walisema bei ya vifaa vya ujenzi zipo juu kutokana na utitiri wa kodi. Kodi hizo zikiangaliwa upya, vifaa vitashuka bei.

6. Vijijini tulikuta umeme na maji safi sehemu nyingi ni tatizo.

7. Tukaongea na madereva wa daladala, mabasi na maloli, wao kilio chao ni mikataba ya ajira, tochi barabarani ambazo zimegeuzwa mtaji na vitega uchumi vya trafiki.

8. Tukaongea na wadada wa kazi pamoja na shamba boys, wao wanalilia kutumikishwa masaa mengi, ujira mdogo na kukosa mikataba ya ajira.

10. Tulikutana na makundi ya vijana wahitimu katika vyuo vikuu, vya kati na sekondari. Vijana hao wanalilia ajira. Tulibaini wahitimu wengi wamesoma kozi ambazo huwezi kujiajiri. Katika hili kuna haja ya kuifanya Elimu ya ufundi kuwa ya lazima na kufuta mitaala ya masomo ya ujanja ujanja, tulibaini kozi za VETA ni muhimu kuliko shahada za sociology, psychology, public administration, political science, procurement n.k. kozi ambazo zina utitiri wa wanafunzi ambao hawaajiliki.

Hapa kuna haja ya kuupitia upya mfumo wa Elimu maana vyuo vingi chini ya Baraza la vyuo vya Ufundi havifundishi kozi za ufundi.
Makundi yote hayo yalikubali kukupatia Kura na ushindi wa kishindo kwa matumaini kwamba utaboresha hali zao.

Nimeamua kukufikishia kama walivyosema kwakuwa niliwaahidi kwamba nitakufikishia. Wito wangu, katika awamu hii ya pili, watendaji wanapaswa kuwajibika zaidi kwa kuwatumikia wananchi maana uzembe wa watendaji ni mzigo kwa Chama na Serikali.

Uwepo pia utaratibu wa kuwadhibiti madiwani na wabunge ili wawatumikie wapiga kura wao badala ya kuhamia mijini Mara baada ya kuchaguliwa.

Namaliza kwa kukupongeza sana kwa Ushindi wa Kishindo
 
Hongera sana kwa CCM, wapinzani watulize mshono, watanzani walifanya maamuzi sahihi.. Wasilazimishe matokeo wanayotaka. Mjipange upya kwa 2025.
 
Kwa kero zote hizo bado waichague CCM!?

Mbona itakuwa ni ujinga wa hali ya juu? Yote uliyoyaandika hapo na mengine mengi ni kero kubwa kwa wananchi wa Tanzania ambao waliahidi kumuondoa jiwe.

Sasa nawe unasaidia wapinzani kuthibitisha ushindi alioupata jiwe si wa wapiga kura bali ni wa tume.
 
Nadhani umesahau kuwa kibaraka wa mabeberu hakuwa na suluhisho lolote la kutatua hizo kero, na hakuzigusia kabisa kwenye kampeni.

Badala yake yeye alikuja na personal interest zake na kuzifanya ndizo kero za wananchi, as a result wananchi wakaona JPM ambaye ameonyesha uthubutu mkubwa zaidi wa kushughulikia hizo kero ni bora zaidi kuliko kamanda msaliti.
 
Hongera sana kwa CCM, wapinzani watulize mshono, watanzani walifanya maamuzi sahihi.. Wasilazimishe matokeo wanayotaka. Mjipange upya kwa 2025.
Baada ya kiapo Leo, kazi inaendelea Phase II, watanzania tuiunge mkono serikali ili tupate maendeleo ya Haraka, Maendeo Hayana Chama
 
Kwa kero zote hizo bado waichague CCM!?

Mbona itakuwa ni ujinga wa hali ya juu? Yote uliyoyaandika hapo na mengine mengi ni kero kubwa kwa wananchi wa Tanzania ambao waliahidi kumuondoa jiwe.

Sasa nawe unasaidia wapinzani kuthibitisha ushindi alioupata jiwe si wa wapiga kura bali ni wa tume.
Hakuna nchi isiyokuwa na kero, hakuna serikali yenye kuweza kuondoa kero zote, maana utatuzi wa kero moja, huibua nyingine.
 
Hakuna uchaguzi umefanyika Tanzania zaidi ya CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi kwa njia haramu za kishetani
 
Hakuna uchaguzi umefanyika Tanzania zaidi ya CCM kuulawiti kuubaka kuunajisi uchaguzi kwa njia haramu za kishetani
Uchaguzi wetu ni bora kuliko wa Marekani, Huku waliochagua Rais ni wapiga Kura 15 mil, Marekani watu 58 ndio wanaochagua Rais
 
Hongera sana kwa CCM, wapinzani watulize mshono, watanzani walifanya maamuzi sahihi.. Wasilazimishe matokeo wanayotaka. Mjipange upya kwa 2025.
Safi sana, hata wewe Hautauepuka mlo mmoja kwa siku/Viazi vitamu na maji kwa kisima.
 
Back
Top Bottom