Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,595
- 215,298
Maendeleo ya sayansi na tekinolojia yameua mahusiano ya kijamii. Leo hii kila mtu anatembea na simu. Akiwa anasubiri huduma iwe mahakamani au hospitali anaingia Instagram au Facebook. Hakuna muda wa kumsalimia aliyekaa pembeni yako.
Miaka ya nyuma ilikua ni kawaida kugonga mlango katika nyumba iliyo karibu na kuomba maji ya kunywa ukiwa na kiu. Siku hizi kugonga nyumba ya mtu kuomba maji au kuomba kutumia simu umepatwa na dharura ni jambo la ajabu. Enzi za simu za mezani nyumba zenye simu zilijulikana na kukiwa na dharura mnagonga mlango hata usiku wa manane.
Binadamu ni wanyama wanao tegemeana na hupenda kushirikiana. Kadiri maendeleo yanavyoongezeka binadamu tunazidi kujitenga. Usishangae ukawaeza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa ukiwa peke yako.
Huko tuendako itafikia wakati unafunga ndoa ukiwa na mashahidi wenu tu na baada ya hapo mnakwenda kupata chakula nyumbani au hotelini. Muda wa kualikana kwenye sherehe hautakuwepo.