Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamebadili tabia zetu kama binadamu

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,597
215,272
Maendeleo ya sayansi na tekinolojia yameua mahusiano ya kijamii. Leo hii kila mtu anatembea na simu. Akiwa anasubiri huduma iwe mahakamani au hospitali anaingia Instagram au Facebook. Hakuna muda wa kumsalimia aliyekaa pembeni yako.

Miaka ya nyuma ilikua ni kawaida kugonga mlango katika nyumba iliyo karibu na kuomba maji ya kunywa ukiwa na kiu. Siku hizi kugonga nyumba ya mtu kuomba maji au kuomba kutumia simu umepatwa na dharura ni jambo la ajabu. Enzi za simu za mezani nyumba zenye simu zilijulikana na kukiwa na dharura mnagonga mlango hata usiku wa manane.

Binadamu ni wanyama wanao tegemeana na hupenda kushirikiana. Kadiri maendeleo yanavyoongezeka binadamu tunazidi kujitenga. Usishangae ukawaeza kusherehekea siku yako ya kuzaliwa ukiwa peke yako.

Huko tuendako itafikia wakati unafunga ndoa ukiwa na mashahidi wenu tu na baada ya hapo mnakwenda kupata chakula nyumbani au hotelini. Muda wa kualikana kwenye sherehe hautakuwepo.
 
Madam! Maisha ya upekee ndio bora, chanya na yenye muendelezo, ukizingatia kanuni za muingiliano na mchanganyiko usiokuwa na maana ndio mwanzo wa maisha ya kimaskini, hali duni, ujinga, maradhi na unafiki.

Kupitia mfumo wangu wa maisha naweza maliza siku 40 sijaonana na mtu yeyote physically and digitally! Ndugu na rafiki wa kweli kwangu ni mfumo wa mapinduzi katika fikra, tafiti, ubunifu, teknolojia na sehemu yangu.

Umegusia suala la kuoa ukiwa mpweke. Moja ya mpango wangu endapo nikibadili mawazo na kuamua kupata mwenza basi makubaliano na mapatano yatakuwa chini ya watu wanne. Siingi katika mahusiano kwa sababu ya watu au jamii, siku yangu ya kuzaliwa ni yangu sio ya watu baki.

Tusifanye vitu kwa ajili ya watu au kuridhisha kundi fulani la watu tufanye vitu kwa tuonavyo ni sahihi au sawa kwa upande wetu. Kuna watu hadi leo hii hawatumii simu janja au mifumo ya tarakilishi sio kwamba hawana uwezo lakini ni maamuzi wanayoamini ni sahihi kwao.

Maendeleo ya sayansi na teknolojia hayajabadili tabia za wanadamu, bali huo ndio uhalisia wa mwanadamu. Usione mtu kawa mwizi, malaya, msaliti, mnafiki and co. ukadhani kabadilika au kubadilishwa lah! hasha huyo ndiye yeye na ni asili yake.
 
Idadi kubwa ya watu pia wanazidi kudharau uchawi na kupuuza mambo mengi ya dini yanayoonekana kutokwenda na wakati.
Wanga wabadili style maana teknolojia imefanya usiku kuwa mchana wakati wote kuna mwanga wa taa.Watu wanakesha kwenye social media au alarm inaita. Mchawi atapata wapi nafasi?

Watu wanatembelea gari mchawi atapata wapi nyayo zako akuloge?

Wanawake wanaweka nywele bandia mchawi akichukuwa unywele kumbe wa mbrazil.
 
Idadi kubwa ya watu pia wanazidi kudharau uchawi na kupuuza mambo mengi ya dini yanayoonekana kutokwenda na wakati.
Hakika mkuu, dini na uchawi vinaanza kukosa nafasi katika jamii yetu, wengi ukiongea nao kuhusu dini wanaweza hata kukupuuza tu!
 
Nadhani tunakubaliana kwa sote kua panapotokea mfumo wa madiliko lazma utuathiri nyendo zetu za zamani. Hata wanyama wanafwata mfumo ya mabadiliko.ila ukweli utabakia pale pale kama ww unao hisia na ankili za " KiBinAdamu" utaendelea kuenshi vyema na watu.
 
Zamani kujijini na mtaani watu walikula pamoja. Hata familia ambazo hazikuwa na kitu siku ile hazikulala bila kula. Siku hizi nyumba zinajengwa na mageti na hatukuweka utaratibu wa kuwasaidia wasio jiweza.
 
Kwa kweli mfumo wa maisha umebadilika sana, nakumbuka miaka ya nyuma sikukuu ya Wakristo basi tunafungasha mapilau kupeleka kwa majirani zetu waislamu lakini hivi sasa mambo yamekuwa kinyume kabisa. Kwa kweli tunapoenda itafika mahala tutakuwa hatusalimiani kabisa.
 
Kwa kweli mfumo wa maisha umebadilika sana, nakumbuka miaka ya nyuma sikukuu ya wakristo Basi tunafungasha mapilau kupeleka kwa majirani zetu waislamu lakini hivi sasa mambo yamekuwa kinyume kabisa. Kwa kweli tunapoenda itafika mahala tutakuwa hatusalimiani kabisa
Tunako kwenda utawajua vizuri marafiki wa Instagram kuliko jirani yako aliyepata kiharusi na anahitaji msaada wako japo kumpa mkewe masaa mawili ya kumpimzika katika kumhudumia mgonjwa.
 
Zamani kujijini na mtaani watu walikula pamoja. Hata familia ambazo hazikuwa na kitu siku ile hazikulala bila kula. Siku hizi nyumba zinajengwa na mageti na hatukuweka utaratibu wa kuwasaidia wasio jiweza.
Zamani ubunge mtu alikuwa anabembelezwa agombee kwa sababu jamii inamkubali siku hizi wabunge wanajipitisha wenyewe bila kupingwa na wengine wanafoji barua za viti maalumu!
 
Tunako kwenda utawajua vizuri marafiki wa Instagram kuliko jirani yako aliyepata kiharusi na anahitaji msaada wako japo kumpa mkewe masaa mawili ya kumpimzika katika kumhudumia mgonjwa.
imenibidi nicheke kwakweli eti utawajua vzur marafiki wa instagram kuliko majirani zako aiseee kabisa maisha yanakwenda kasi sana
 
Zamani kujijini na mtaani watu walikula pamoja. Hata familia ambazo hazikuwa na kitu siku ile hazikulala bila kula. Siku hizi nyumba zinajengwa na mageti na hatukuweka utaratibu wa kuwasaidia wasio jiweza.
Siku hizi hata kula pamoja nyumbani hakuna. Huyu kaenda kuangalia mpira, huyu anaCHAT jikoni mwingine anacheza GAME chumbani. Chakula kipo kwenye hotpot kikipoa mtu anapasha kwa MICROWAVE.
 
Back
Top Bottom