Amba Samedi
Senior Member
- Apr 5, 2024
- 193
- 326
Umenena vyema. Sema sio kazi ya mamlaka kukabiliana na ukahaba. Hili ni jambo la kiroho, na jukumu la kujenga maadili hupatikana nyumbani na ibadani.Wakuu kheri ya mwaka mpya.
Naam kwakweli kila maendele yamekuwa na changamoto leo hii Mbagala inakua kwa kasi sana kwa wafanyabiashara kuwekeza pesa zao kutoka na kuongezeka kwa watu na kushamiri kwa biashara.
Mabaa yamejengwa, Nyumba za wageni na za kupanga kupelekea sasa kuongezeka kwa biashara hii ya ukahaba.
Vijana wadogo wanafanya umalaya hadi kwenye makazi ya watu na kutuharibia watoto(wadogo zetu).
Mwanzo ilikuwa maeneo machache tu Pale Masakuu, Sokoni na njia ya Kiburugwa sasa biashara iko Round about ya Charambe kwenye night club maarufu kwa sasa Hotline, Zuen pub, shule ya msingi Rangi 3 uwanjani panapojengwa shule ya sekondari hadi vichochoroni na maeneo mengi kiufupi ukahaba umesambaa kwa kasi sana.
Wenye mamlaka kama wasipothibiti hii hali yumkini miaka michache ijayo mbagala itakuwa Tandika mpya na itapoteza mambo mengi na tayari itakuwa sio salama kuishi na familia zetu.
NB: Najua kuna wadau watakuja kushambulia ila katika jamiii iliyostaarabika ukahaba kufanyika mtaani ni hatari kwa kizazi chetu hasa kutokana na haya magonjwa.