Mi mwenyewe niko mpakani hiyo asilimia 60 unayoisema umeipata wapi? Tz ni nchi huru ya kidemokrasia yenye Katiba na utawala,ukitaka kujitenga nenda kawaulize Bokoharam waambie wakupe eneo huko!!
Mbona kwa Boko haram ni mbali saana......hapahapa jirani Kenya.anagalia hiyo 60% nilivyoipata...Wadigo wapo Kenya na TZ...WAKURYA wako kote....Wamasai kote....Wasomali kote....Wajaluo kote....Wahaya....kote upande wa Uganda...Wachagga....usiseme nusu ya Mombasa ni wachagga .
Huu mchakato upo na tuna kamati ya vijana wapiganaji tunakutana tena next Monday then tutaandaa press conference kuwaeleza waandishi wa habari nia yetu na jinsi tutakavyoifanikisha.
Ni wazo chanya....lakini bado nina wasiwasi kama mtakubaliwa.Hebu angalia walioteuliwa kutoa elimu kwenye TV pamoja na kushiriki kwenye Bunge la katiba,mafunzo yao ni kwamba katiba imesheheni vitu vingi na imetaja makundi yote...ki vipi....hawatuelezi na itafanyaje kazi hawatuelezi.
Mukikubaliwa munaweza kuondoa huu mpasuko uliopo sasa hivi.
Ha ha ha ha rudi kwenye lugha ya nyumbani tu maana naona unachanganya madesa!Tanzania imejengwa kwenye misingi imara,usilolijua wewe ni nafasi yako katika kuendelea kufanikisha mafanikio yaliyopo!jipange sawasawa kupokea mabadiliko ya nchi yako,usipaniki na kukata tamaa!
If the country was built on the sound foundations, why do you demand a new constitution?
hacha kulilia mabadiliko huku umelala nyumbani jitokeze
Kwa kweli wenzetu waliofanikiwa kushinikiza kuwepo kwa katiba muafaka wako na nafuu kubwa. Wao kama wananchi wayatakayo yanakuwa na serikali zao zinawajibika kwao. Ununda uliokuwapo unaelekea kuwa historia.
Kwa wenzetu katiba zinawalazimisha Polisi kuwa walinzi wa umma. Polisi anawajibika kulinda waandamanaji. Polisi anakuwa vetted na wananchi. Asiye faa anatupwa pembeni.
Mahakama zao zawajibika kwa wananchi -- hizi zetu zinazoongelea dhamana (si kesi) wakati uko ndani kwa siku lukuki zinatia mashaka. Tukimbilie wapi siye? Haiyumkiniki ni katika kudai katiba mpya yenye kutuweka sote sawa mbele za haki.
Yawezekana hawajafika wanako tarajia kufika lakini wako na nafuu na wanapiga hatua mbele. Tujifunze kwa wenzetu. Maana mazingira yao na yetu hayako na tofauti kubwa hali wenzetu angalau wana sauti za kusemea. Sisi Je?
Source: Dismissal of 127 officers hits traffic police hard
Tunahitaji katiba mpya iseme nini ambacho hakijasemwa katika katiba iliyopo?
Kama ni uhuru wa mahakama katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa mahakama zitakuwa huru..
Tume ya uchaguzi? Katiba iliyopo sasa imeweka wazi kabisa kwamba tume ya uchaguzi itakuwa huru..
Sidhani kama tatizo ni katiba..
Sijasahau pia tulikwenda katika bunge la katiba badala ya kupigania mambo ya muhimu tukaenda kugombania madaraka(serikali tatu)