Maendeleo mapya: Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania - Uzalendo

Zakumi

JF-Expert Member
Sep 24, 2008
4,858
2,000
Amani kwenu wazalendo wenzangu:

Baada ya salaam ningependa kusema kuwa uchaguzi uliopita una mapungufu makubwa sana. Mapungufu mengi ni ya masuala ya kikatiba ambayo yamekuwepo kwa muda mrefu kuanzia uchaguzi wa 1995. Mapungufu hayo hayakujionyesha sana katika vipindi vya uchaguzi vilivyopita kwa sababu wagombea wa chama tawala walikuwa hawana upinzani mkubwa. Hivyo kasoro zote za kikatiba zilifunikwa na umaarufu wa kihistoria wa CCM. Kwa kipindi cha uchaguzi cha 2015, Tanzania itakaribisha wapiga kura wapya wapatao 1.5 miloni au waliozaliwa mwaka 1995 na baadaye.

Hatutajitendea haki wenyewe na kizazi kipya iwapo tutaendelea kutumia katiba iliyo sasa kama mwongozo wa kuendeleza nchi. Hivyo kwa maombi yangu binafsi, wazalendo wa Tanzania tuanze kusukuma mabadiliko ya kikatiba. Ninapoita wazalendo, nina maana wananchi bila kujali itikadi zao vyama vya kisiasa, dini au ukabila.

Bila ya kutaja matatizo ya katiba yetu, ningependa kueleza toka tumepata uhuru katiba ya Tanzania imekuwa ni kitu kisichoeleweka wazi kwa wananchi. Tuliosoma shule wakati somo la siasa linafundishwa mashuleni, tulikuwa tunafundishwa katiba ya CCM na miongozi ya chama hicho. Hivyo basi kuna uwezekano mkubwa hata wanasiasa wetu wengi hawajui umuhimu wa kitabu hicho.

Hivyo ningependa kufungua ukumbi kwa kuwakaribisha wenye mawazo na nia ya kubadilisha katiba kutoa mawazo yao.

Na vilevile kama kutakuwa na watu wanaotaka kuanzisha jumuia ya kufanya mabadiliko ya kikatiba, naomba mjitokeze.
 

lukesam

JF-Expert Member
Feb 23, 2015
10,690
2,000
Umesahau madaraka ya kimungu ya Raisi katiaba ya sasa rais ndio alfa na omega

Leo tumepata pombe anavunja iatakavyo siku tunampata mbaya zaid ndio utajua
Mkuu, kikubwa ni watanzania kujitambua.. Mimi sioni sababu ya majaji wetu kutokuufanyia kazi uhuru wao walionao kikatiba..

Ukishamteua hauwezi kumtumbua..na hata ukitaka kumbadilishia nafasi mfano unataka kumpa uwaziri ni lazima akubali.. Kwa maana kwamba anaweza kukataa akabaki na ujaji wake.. Sasa hapa nini kinainyima mahakama kuwa huru?

Kikubwa ni hii nchi wasomi wapunguze kujikombakomba na wafanye kazi kwa mujibu wa sheria..

Tumekuwa taifa la watu wasiojiamini kabisa,mtu licha ya kuwa na elimu kubwa hajiamini hata kidogo..
 

mshunami

JF-Expert Member
Feb 27, 2013
3,911
2,000
Niliandika sana katika uchaguzi uliopita 2015 kuwaasa wapinzani kuwa bila Katiba mpya yenye sheria mpya ya uchaguzi hawawezi kushinda uchaguzi ule. Baada ya Lowasa kuhamia Chadema walidhani kimakosa kuwa amekuja na muujiza wa kushinda sheria ile ya uchaguzi iliyotamalaki wakati wa chama kimoja. Ilikuwa tunachagua kati ya Nyerere na giza. Kipengele kilichokuwa kinasema kuwa atakayetangazwa na Tume ndiye raisi na haitahojiwa mahakamani kilikuwa na mantiki kwa kuwa chama kimoja kilikuwa kimeshika hatamu. Katika siasa ya chama kimoja utafanyaje zaidi ya kukubali hilo! Hii ni lazima ibadilike sasa kabla ya uchaguzi mwingine na Upinzani kama hiyo siyo agenda yake ya msingi unapoteza muda.
Tatizo halikuwa Jecha kule Zenji bali ni Sheria ya uchaguzi, na kama haibadiliki Upinzani usahau kushinda uchaguzi. Kuna haja ya kuacha mambo mengine na kufanya Katiba mpya kuwa agenda ya msingi. Kenya wameonyesha njia.
 

Chabo

JF-Expert Member
Jul 20, 2011
827
500
Tangu niliweke jambo hili kichwani mwangu....huwa sioni haja ya kupanga foleni ili nimchague ninayejua atashinda
 

Mchangila Bakari

New Member
Oct 13, 2017
2
20
suala la kupatikana kwa katiba mpya ya jamhuri ya muungano wa Tanzania ni jambo ambalo limekuwa likisemwa sana kwenye vinywa vya watanzania na kwenye mitandao ya kijamii pia, kuna wengine wanaamini kwamba katiba ya warioba ndio muarobaini wa matatizo au mapungufu yanayotokea na ambayo yataendelea kutokea katika taifa letu. Binafsi mimi pia ni miongoni mwa watu wanaopenda au wanaotaka katiba yetu ifanyiwe marekebisho kwasababu kwanza katiba hii ni katiba ambayo ilipatikana kipindi ambacho kulikuwa na utawala wa chama kimoja, hivyo katiba ambayo ilipatikana kipindi cha utawala wa chama kimoja haiwezi kuendana na mfumo wa siasa za sasa ambao ni mfumo wa siasa za zinazohusisha vyama vingi, licha ya kuwa muumini wa katiba mpya, bado kuna muda nakosa majibu hasa hasa nikijiuliza kwamba "Je katiba mpya ndio muarobaini wa matatizo ya taifa hili". Kila nikitafakari huwa ninajikuta nakuja na majibu ambayo yanapingana na uumini wangu, na muda mwingine huwa nabadilika na kuanza kuamini kwamba katiba mpya(ya warioba) haiwezi kuwa suluhisho la matatizo ya taifa hili na nitatoa sababu zangu ili nawewe kama utakuwa na mawazo tofauti pia utoe sababu zako kwasababu lengo ni kueleweshana.

Licha ya kuwa muumini wa katiba, bado naamini kwamba katiba sio suluhisho la matatizo yetu, badala yake suluhisho litakuwa ni watu ambao tunawachagua kusimamia katiba husika, kwa maana hiyo kitu cha kwanza tunachotakiwa kufanya ni kuchagua viongozi ambao tunaamini kutoka katika sakafu ya nyoyo zetu kwamba wanauwezo na utayari wa kuiongoza nchi kwa kufuata utaratibu au sheria zetu tulizojiwekea katika taifa letu, nitatoa mifano kadhaa kuthibitisha hili,

Mfano wa kwanza; Katiba yetu ya sasa imehalalisha(imeruhusu) maandamano au mikutano ya kisiasa kwa nchi nzima, lakini kwa sasa jeshi la polisi limepiga marufuku mikusanyiko hiyo endapo mtu atakamatwa akiwa anafanya jambo hili anaweza akaambulia kula virungu vya polisi na na kukamatwa na wakati mwingine kuwekwa ndani, sasa hapa watanzania wenzangu nawaomba munisaidie swali langu kwamba je hapa tatizo ni katiba au tatizo ni jeshi la polisi?? maana katiba imeruhusu ila polisi wamekataza, kwa upande wangu mimi naona katiba sio tatizo.

Mfano wa pili; watu wengi wamekuwa wakilalamika kwamba kuna tatizo kwenye mahakama zetu, kwamba haziko huru hivyo tunahitaji katiba mpya ambayo itaziweka mahakama huru, lakini mimi najiuliza kwamba je tatizo liko kwenye mahakama zetu au tatizo ni watu wengine, kwa mfano juzi mahakama ilitoa order ya kusitisha ubomoaji kwenye baadhi ya maeneo lakini wabomoaji walienda kubomoa, ikumbukwe kwamba mahakama ikishatoa order ndio inakuwa imemealiza kazi yake, mahakama haina jukumu la kwenda kuzuia ubomoaji huo, wanachotakiwa wao ni kutoa "notisi" zuio la mahakama lilipaswa kuheshimiwa na kila mtanzania mpaka amiri jeshi mkuu, sasa kama mahakama imeweza kutoa zuio la ubomoaji wa nyumba halafu wabomoaji wakaenda kubomoa ni sahihi kusema kwamba mahakama haiko huru, kwasababu kwa kutoa tu notisi wanakuwa wameshatimiza wajibu wao, je hapa tatizo ni mahakama au wabomoaji?? Lakini pia wapo watu wengi ambao wamewahi kuishtaki serikali na wakaishinda kupitia hizi hizi mahakama zetu, na mahakama ikasema serikali iwalipe fidia, endapo mahakama itasema serikali iwalipe fidia watu hawa halafu serikali ikakaidi kuwalipa fidia hizo, je tatizo litakuwa liko kwa mahakama?? sasa je tunaposema mahakama haziko huru ni sahihi?? gazeti la mwanahalisi liliwahi kufungiwa wakaenda mahakamani na wakashinda, na mahakama ikawaagiza serikali iwalipe fidia, na walishinda kupitia hizi hizi mahakama zetu, sasa tunaposema mahakama haziko huru tunakuwa tunakosea au tuko sahihi??

Kutokana na mifano ambayo nimeieleza hapo juu, na mingine mingi ambayo sijaisema, uumini wangu au imani yangu ya kudai katiba mpya kama suluhisho la matatizo ya taifa hili inazidi kupungua, kwasababu kama kufanya mikutano ya kisiasa ni jambo halali katika katiba yetu lakini leo sehemu hiyo ya katiba inavunjwa, basi ata tukirekebisha hii na tukapata nyingine bora zaidi, mvunjaji akiamua kuvunja ataivunja tu kama anavyoivunja ya sasa.

USHAURI WANGU.

Kwanza ifahamike kwamba katiba sio msaafu, inaweza kubadilishwa kwa wakati wowote, ni suala tu la kupeleka muswada bungeni na kama wabunge wengi wakiridhia bas inabadilishwa, hakuna haja ya kubadilisha katiba leo halafu baada ya mwaka mmoja wabunge wa chama fulani wapeleke muswada bungeni wa kubadilisha kipengele fulani cha sheria tulichokiweka leo na wakafanikiwa kwasababu ya wingi wao, kinachotakiwa kufanyika sasa hivi ni wapinzani wakazane kuongeza idadai ya wabunge bungeni, kwanza wawe wengi ili hata tukipata katiba mpya isiwe rahisi kubadilishwa kwa maslahi ya chama fulani, kama sheria ya kuonyesha bunge live ilivyobadilishwa, ndio hivyo hivyo katiba mpya ambayo tutaipata itawezwa kubadilishwa tena kama wabunge wa chama kimoja watazidi kuwa wengi bungeni kwa maslahi ya chama chao.

Kwasasa hakuna haja ya wapinzani kuwekeza nguvu nyingi kwenye kuurafuta uraisi au kudai kwamba matokeo ya uraisi yaweze kupingwa mahakani, sasa hivi kuna malalamiko kwamba wagombea wa upinzani wa nafasi ya ubunge wengi waliporwa ushindi wao na wakati huo huo matokeo ya ubunge yanaweza kupingwa mahakamani, kwanini wasianze kwa kupigania haki za hawa wabunge walioporwa haki zao katika mahakama, kama wameshindwa kuwapigania hawa wabunge mahakamani na wakapa haki, endapo matokeo ya uraisi yakiruhusiwa kupingwa mahakamani wataweza kuyapinga???

Watuaminishe kwanza kwa wabunge halafu ndio waje waseme wanataka kupinga matokeo ya uraisi mahakamani.

Lakini ni mawazo yangu tu nawewe pia unaweza ukatoa yako.

Na Mchangila Bakari.
 

technically

JF-Expert Member
Jul 3, 2016
9,688
2,000
Tufike sehemu tuwe wakweli kwa serikali za kiafrika hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani sio suluhisho la matatizo yetu hasa kuna watu wanasema .

Tukipata katiba tutaweza kuwa na uchaguzi ulio huru thubutu hakuna kitu kama hicho na hakitakaa kitoke

Matatizo ya uchaguzi ni busara za vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi na utashi wa viongozi waliopo madarakani

Kama mnabisha angalia uchaguzi wa mwaka 2017 nchini kenya Mpaka kijana mmoja mzalendo wa tume ya uchaguzi IEBC alikatwa kiganja ili tu Uhuru Kenyatta aendelee kuwa madarakani

Kenya ndio nchi yenye katiba bora kuliko nchi zote barani africa lakini kilichotokea mwaka 2017 ilikuwa ni ubakaji wa democrasia waziwazi.

angalia Marekani mwaka 2016 Trump alizidiwa popular votes million 3 lakini mpaka sasa eti yupo ikulu sijui anawakilisha wananchi wapi upuuzi mtupu.

tufike sehemu tuwe wakweli hata kama tungetengeneza katiba ya namna gani kama hakuna utashi wa watawala na watu wa usalama kama police na jeshi hawajaamua kuwa wazalendo na kuacha kutumikishwa na wao kuwa na wagombea hasa africa tutaendelea kupiga kelele mpaka kiama ..

Hivi unategemea mtu kama Magufuli akupe katiba mpya halafu akuruhusu kwenda IKULU?
 

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,207
2,000
Mifano yako miwili tu......

Ukitaja nchi Africa zenye kuwa na watu wavumilivu basi uwezi kukosa kuitaja Tanzania. Hivi kwanini usiwe kati ya kijana na kusema Je tukiwa nakatiba bora kwenye jamii yetu tulivu kuna makosa gani?


Tubadilike jamani. Haya mambo ndio maana huyu rais kaingia na kuongeza asilimia ya makato kwa Wale waliolipiwa na serikali wakati wapo chuo, wakati ni tofauti na makubaliano.
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,377
2,000
Ubora wa katiba ya Kenya kuliko nchi zote za Africa ni kwa kuangalia vigezo gani hasa? Facts au Hisia tu?
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
3,054
2,000
Matatizo ya Tanzania ni CCM, si katiba, japo katiba ina mapungufu yake. Ila sio leo wala kesho tutalitambua hilo, nani alaumiwe wakati hakuna kiongozi wa upinzani aliewahi kutawala nchi, kiongozi wa kusukumiwa mpira wa moto aweweseke nao (lawama)????

Mapungufu ya katiba ni madogo, kwa mtazamo wangu. Mfano;

1) Kutoweka/Kuruhusu Tume Huru Ya Uchaguzi.

2) Kwenye issue ya Separation of Powers katika mihimili mitatu ya nchi (Kugawanywa kwa Madaraka). Hapa mgawanyo wa madaraka kikatiba unaojulikana sambamba na madaraka yake ni wa; Judiciary (Mhimili wa Mahakama), Executive (Mhimili wa Serikali) na Legislature (Mhimili wa Bunge).

Hapa tunakuta kitu kinaitwa CHECKS AND BALANCE/UANGALIZI NA BALAMCE (Yaani Haki ya pamoja ya uendeshaji wa nchi pamoja na ushawishi: Rights of Mutual Control and Influence). Kuna sehemu kuna muingiliano ambao unatoa nguvu pande moja kupita mipaka/muingiliano ambao baadhi ya nchi ulishapinga na kuondoa.

#niishie hapo kwa ufupi, nisiumize kichwa kuelezea halafu vichwa maji wanitolee povu
 

Chige

JF-Expert Member
Dec 20, 2008
10,161
2,000
Tufike sehemu tuwe wakweli kwa serikali za kiafrika hata tuwe na katiba nzuri kiasi gani sio suluhisho la matatizo yetu hasa kuna watu wanasema .

Tukipata katiba tutaweza kuwa na uchaguzi ulio huru thubutu hakuna kitu kama hicho na hakitakaa kitoke

Matatizo ya uchaguzi ni busara za vyombo vya ulinzi na usalama wa nchi na utashi wa viongozi waliopo madarakani
Ukiona pamoja na kuwa na katiba "mzuri" bado suala la uchaguzi linategemea busara za vyombo vya ulinzi na usalama basi fahamu hiyo katiba ina mapungufu makubwa! Ina mapungufu kiasi cha kushindwa kuweka mipaka kati ya mihimili kadhaa ya dola na taasisi zake!

Katiba mzuri haiwezi ikatoa loophole ya vyombo vya ulinzi na usalama viwe eti ndio determinant za what next after uchaguzi!!

Umetoa mfano wa Marekani! Unachokejeli kuhusu popular vote ndivyo katiba yao ilivyo! Kinyume chake, hivi umeshawahi kufikiria Trump na uwendawazimu wake ule angekuwa amefanya mambo ya kiuendawazimu mangapi endapo Marekani isingekuwa na katiba bora?

Ni mambo mangapi ambayo yalikuwa initiated na yeye mwenyewe binafsi lakini yakapigwa chini kwa sababu tu, sheria ambazo ni matunda ya katiba zilitupilia mbali mambo yake mbalimbali!!!

Itoshe tu kusema kwamba, katiba bora inaweza kufanya mambo mengi makubwa endapo Watanzania kwa ujumla wao watafahamu wanataka nini hasa! Katiba inayolenga kutatua kero zao za msingi!

The problem kwa Afrika, michakato ya katiba huwa inabakwa na wanasiasa na matokeo yake, muhimu kwao ni yale yenye faida za kisiasa kuliko vinginevyo!
 

amani mushi

Member
Jul 14, 2018
67
125
Duuh,una elimu Gani kama unaipima katiba katka kipengele kimoja cha cha uchaguzi huru na haki tuu?VP uwepo wa serikali tatu,nguvu ya wananchi kuwajibisha viongozi,kupunguzwa kwa madaraka ya mkuu wa nchi,nk
 

mr mkiki

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,207
2,000
Ukiona pamoja na kuwa na katiba "mzuri" na bado suala la uchaguzi linategemea busara za vyombo vya ulinzi na usalama basi fahamu hiyo katiba ina mapungufu makubwa! Ina mapungufu kiasi cha kushindwa kuweka mipaka kati ya mihimili kadhaa ya dola na taasisi zake!

Katiba mzuri haiwezi ikatoa loophole ya vyombo vya ulinzi na usalama viwe eti ndio determinant za what next after uchaguzi!!
Ndugu nimekupa vizuri sana, tambua tuna vijana waajabu sana.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom