Maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa

Maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa

Ukishindwa kusoma tazama picha,au ndo macho yako kilakitu yanaona ni kijani na njano.GAMBA CHAKAVU WE!

Hujajibu swali, ndio nini hiki?

quote_icon.png
By democratic

kwa maana hiyo unauhalarisha mwisho wa hiki chama cha magamba & Co
 
Mleta mada nakuunga mkono ndiyo maana TANU ikasambaratishwa na walioanzia kushika madaraka waliiwacha hii nchi kubaya sana. Bora CCM ya kuanzia kwa Kikwete kuwa kiongozi tunaona maendeleo ambayo hayajawahi kutokea kabla.
 
Mzee vyama vya nama hiyo vipo vingi tu; jitahidi uwe unafanya utafiti kidogo kujua mambo kabla hujayaandika maoni yako.

(a) TANU, chama hiki kilieta sana maendeleo Tanganyika ambayo baadaye yaliharibiwa na CCM; kumbuka kuwa CCM siyo TANU.
(b)ASP, chama hiki kilieta sana maendeleo Zanzibar ambayo baadaye yaliharibiwa na CCM; kumbuka kuwa CCM siyo ASP.
(c) BDP (Botswana Democratic Party,) chama hiki kimeleta maendelo sana huko Botswana, ndiyo maana kulikuwa na wabongo wengi wakikimbilia huko.
(d) PAP (Peoples Action Party), hiki ni chama kilicholeta maendeleo ya ajabu huko Singapore; nadhani hakuna haja ya kuambiwa zaidi.
(e) CCP ( Chinese Communist Party), ni chama pekee kilichotawala china tangu kilipoikomboa nchi hiyo mwaka 1949, na leo hata wewe unajua kuwa China imeendelea kwa kasi sana.

Hiyo ni mifano michache tu, lakini kuna nchi nyingi sana zilizoendelea china ya vyama vyao vya ukombozi. Kwa wale wanaodai kuwa TANu na ASP waliiacha nchi ikiwa na hali mbaya sana ama ni wapiga propaganda tu au hawajui wanalosema. Sana sana huenda hawakuwapo mwaka huo 1977, kwa vile huenda wamezaliwa na kuikuta CCM tu, na wanalofanya ni extrapolation ya CCM waliyokuta na kudhani kuwa TANU na ASP zilikuwa hivyo pia.
 
Inawezekana vipi kuhimiza watu wajitume kwa kufanya kazi bila kuwapa nyenzo na vitendea kazi!!!!???? Huu ni wakati wa kufanya mambo kizalendo na sio kwa Itikadi za chama au mfumo wa siasa.
 
Watanzania wenzangu, kwa muda mrefu naona tunajadili mambo yasio ya msing hasa kusifia vyama na viongozi kwa mitazamo yetu.
Kwa upeo nilionao mimi naomba kwa kipindi hiki tulicho nacho ikiwezekana tujadili katiba ambayo itatusaidia katika kuleta njia nzuri za kupata maendeleo.
Tunahitaji kuweka vipaumbele na taratibu nzuri zitakazotuongoza wote bila kujali vyama. Mfano ni mwelekeo na malengo ya wananchi. Katika hili ingependeza sana kama tutaamua kuweka vitu vya maendeleo vitakavyofuatwa na chama chochote kitakachoingia madarakani
 
Kiongozi makini ni yule anaekubali kukosolewa, Chama makini ni kile ambacho kipo tayari kukosolewa kwa masilahi ya umma, 2015 sio mbali lakini ni watanzania tutakao amua kupiga hatua au kurudi nyuma. tusipokua makini tutaishia wote kuwa wanasiasa.. Nchi hujengwa kwa kuchapa kazi sio kwa porojo na majungu, siasa haijengi nchi, siasa inahamasisha kujenga nchi kama ikitumiwa vizuri.. Tusikubali kuchagua Chama/mtu ambae hayupo tayari kukosolewa kama kweli tunahitaji maendeleo..
 
Wakati umefika kwa watanzania kubadilika katika maendeleo yao wenyewe. Hakuna chama chochote cha siasa kitakachomkomboa mtanzania. Ccm au chadema au cuf haviko kwa ajili ya tanzania wala kiongozi hayuko kwa ajili yako.

Mtanzania mwenyewe yuko kwa ajili ya tanzania. Badilika kifikira,badilisha hatua zako ili kujiletea maendeleo kwanza ndipo nchi yako itakuwa na maendeleo. Huu si wakati wa kuangalia tulikojikwaa ila ni wakati wa kuangalia mbele kwa muktabali wa mbeleni.

"YOU IMAGINE WHAT YOU DESIRE,YOU WILL WHAT YOU IMAGINE AND AT LAST YOU CREATE WHAT YOU WILL"
 
...nasikia harufu ya povu la pombe chafu,dah asubuhi yote hii...???
 
mimi ninaomba mtoa thread hii inijulishe kam amenda shule na kama ameanda shule ni wapi? Hapa nina maana hata shule ya msingi kwani itanisaidia katika kutaka kumsaidia kimawazo pamoja na kumuelewesha. kumbuka hapa jf ni mahali pakueleweshana.
 
Siasa inaweza kuwahamasisha watu wajishughulishe na shughuli za maendeleo. Siasa pia ndio mwangalizi mkuu wa maendeleo yapatikanayo kutokana na watu. Siasa inatunga sheria na kuzilet kwa watu. Siasa safi maendleo bora, lakini siasa chafu maendelo duni
 
Kila kitu kinachoanzishwa hapa duniani huwa na sababu maalum au kuna malengo ambayo yanategemewa.

Vivyo hivyo hata kuanzishwa kwa vyama vya siasa dunia kote vina malengo tofauti tofauti.

Tukichukulia kwa mazingira ya Afrika na hasa hapa kwetu Tanzania, tunaweza kutumia vigezo gani ili kuonyesha vyama ambavyo
viko ndani ya Tanzania vimefanikiwa au kuonyesha chama hicho kimepiga hatua?
 
Nimefuatilia kwa makini sana mwenendo wa siasa za vyama vingi hapa nchini, kiasi cha kuweza kusema kwa hakika kuwa vyama vyote vina
malengo yanayofanana ya kuhakikisha vinalinda maslahi ya vijikundi vidogo vya matajiri ambao wamejipatia utajiri huo kwa njia halali au la, na wala si kusimamia maslahi ya masikini walio wengi.

Matajiri hawa wachache kwa kutumia tamaa za mafanikio au umasikini walionao vijana wengi wamewatumia vijana hao kwenye matukio mbalimbali ya kihalifu ili kufikia malengo yao ya kisiasa kwa gharama yoyote ile. Lakini kama ilivyo kwa mbwa na mwenye mbwa siku zote mbwa ndiye anayepatwa na misukosuko mikubwa ndivyo hivyo ilivyo kwa vijana hawa wanaotumika na hawa mafisadi wachache huishia aidha kupigwa, kuteswa vibaya na wakati mwingine kupoteza maisha kabisa.

Kwa kuwa tumepoteza muelekeo sisi kama nchi, napenda kuwaasa wananchi wenzangu hasa vijana kwamba kwa sasa tuna machaguo mawili tu ya au kukubaliana na hali iende kama ilivyo na sisi tujikite kwenye shughuli zetu za kujiletea maendeleo bila kujali yanayowakuta majirani zetu au kuamuwa kwa dhati kuachana na ushabiki wa vyama na kuamuwa kuchagua viongozi kwa kuzingatia sifa bora alizonazo mtu katika kusimamia na kutetea ustawi wa wananchi, mtu asiyependa kujilimbikizia mali, anayekerwa na umasikini wa wananchi, anayeheshimu haki za binadamu na kuamini kuwa binadamu wote ni sawa nk.

Kwa ujumla kama tungekuwa tunaijuwa vizuri siasa ya vyama vingi tungenufaika sana lakini kwa kuwa ama hutuijuwi au kwa makusudi ya walioshika hatamu badala ya kufanya siasa ya upinzani wa hoja na mitazamo sasa imekuwa ni uadui, ambao kama hatutaamka mapema tutaingia kwenye matatizo makubwa kuliko haya tunayoyaona sasa.

Nimalizie kwa kusema vyama vyote vinaendeshwa na watu walewale (kimtazamo),wenye malengo yanayofanana (kulinda maslahi ya waongoza vikundi ambao ni matajiri/mafisadi wachache), kama tukichagua watu kwa uzingatia uadilifu wao bila kuangalia vyama vyao tunaweza kufua dafu mbele ya wamiliki wa hivi vyama.

Vijana tumesha tumikishwa vya kutosha na mafisadi wa vyama vyote kupitia the so called green, red or blue whatever sasa tujitambue, nchi iko chumba cha wagonjwa wanaohitaji uangalizi maalumu, Please wake up.
 
sasa mbona hujatoa mfano hata mmoja wa jinsi vyama vyote vinavyofanana kulinda maslahi ya viongozi wao ili tuweze nasi kulinganisha.maana nionavyo mimi tofauti ipo tena kubwa nashangaa mtanzania mwenzangu kutoina hiyo tofauti.naukiitaka mimi nipo tayari kukueleza hizo tofauti.
 
Siasa ni maendeleo,ndo maana magambo bajeti inapitishwa na wanasiasa na viongozi ndio wanaongoza kwa kupitia siasa japo kwa mitizamo tofauti either wa kibinafsi au kijamii hapo ndipo waweza maendeleo ya wachache au ya jamii nzima kutegemeana na chama tawala,sio kwamba chama tawala kikiharibu basi vyama vyote havifai....hiyo sio kweli.
 
porojo za interahamwe hizo! Ccm wamefanya siasa ionekane ni porojo,unafiki na ubabaishaji!
 
Ndugu wananchi maendeleo hayaletwi na vyama vya siasa, maendeleo yanaletwa na watu walioamua kuendelea.

Nchi ikiwa na wananchi walioamua kuendelea itaendelea tu.

Vijana changamkeni tumieni nguvu zenu. Nchi yetu ipo wanasiasa hawataweza hata siku moja kutuletea
maendeleo.
Mkuu usiwalaghai wana Jf vyama vya siasa vinaumuhumumkubwa sana kwa kuktakabali wa maendeleo yetu wananchi wanapo kosea ktk uchaguzi wa vyama uwagharimu daima Ktk swala zima la maendeleo so usipotoshe kabisha..!
 
vyama ndivyo vinavyopanga sera za nchi,maana yake sera mbovu maendeleo mabovu
 
Back
Top Bottom