Mkuu: Ni kweli kuwa siasa ni moja ya nyanja kuu za maisha, pamoja na tamaduni(kwangu kama msingi mkuu), na uchumi. Vitu hivi havitengani kamwe! Kila mtu ni mwanasiasa, mwanauchumi, na mwanatamaduni katika taifa lake...yaani hizo ni sifa kuu zinazo m-shape binadamu! Tujiulize hapa, ni nani haishi siasa, tamaduni, ama uchumi? Mambo hayo yote hupaswa kusimikiwa mifumo ya kuyaendesha kufikia maendeleo ya watu. Mifumo hiyo ni lazima isadifu (a) MAZINGIRA yaani sura ya nchi na watu wake (b) NYAKATI, yaani mahusiano yaliyopo katika mazingira, yaani baina ya watu na watu, na watu na sura yao ya nchi. ,, Hapo ndipo tunapohoji ufanisi na uzito wa mifumo iliyopo katika kuendesha nyanja hizi za maisha kuleta maendeleo. Je, mifumo hiyo inakidhi haja?
Kisiasa tupo chini ya "demokrasia", kiuchumi tupo chini ya "uchumi huria-free economy" Kitamaduni nako tunasema "uhuru-freedom". Yote hayo yapo chini ya katiba inayoitwa "HAKI ZA BINADAMU-HUMAN RIGHTS"
Tukiruhusu fikra zetu, kufanya upembuzi yakinifu juu ya mifumo iliyopo "HUWEZI KUKATAA KWAMBA, KUAMINI MAENDELEO YATALETWA NA SIASA ILIYOPO NI KUJIDANGANYA"
Ubunifu haujawai kufika mwisho. Tunayo nafasi ya kuutumia!
Mungu wetu anaita!