Maelfu ya watu wamuombea dua Rais Samia

Chawa wa lumumbashi

JF-Expert Member
Nov 19, 2022
793
1,749
MAELFU ya wananchi mkoani Kagera, wamejitokeza kwenye Uwanja wa Kaitaba, mkoani Kagera na kushiriki hafla ya kumuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Dua hiyo imefanyika leo (Julai 28,2023) ikifanyika katika kipindi ambacho Rais Dkt. Samia anaungwa mkono na Watanzania wengi kutokana na uongozi wake unaojali maslahi ya wananchi na kutatua matatizo yao.

Mkuu wa Mkoa huo, Fatuma Mwasa aliwaongoza maelfu ya wananchi kushiriki dua hiyo wakimuombea Rais Dkt. Samia maisha marefu kutokana na mchango wake kwa maendeleo ya wananchi na Taifa kwa ujumla.

Baada ya dua hiyo, wananchi walisema wanautambua mchango mkubwa wa Rais Dkt. Samia ambaye uongozi wake umeendelea kuleta mapinduzi makubwa ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Walisema mapinduzi hayo yana manufaa makubwa kwa Watanzania na Taifa hivyo anastahili kufanyiwa maombi ili aweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi zaidi.

“Tuna imani kubwa na Rais Dkt. Samia kutokana na uongozi wake, huyu ni kiongozi anayezijua shida zetu na kuzitatua kwa wakati, tunaunga mkono juhudi zake za kuleta umoja na maendeleo kwa taifa,” alisema Olivia Byabato, mkazi wa Kaitaba jirani na uwanja huo.

Walimpongeza Mkuu wa Mkoa huo (Mwasa) kwa kuwaongoza katika dua hiyo na kuahidi kuiunga mkono Serikali ya Awamu ya Sita ili iendelee kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2020-2025 kwa vitendo, kasi kubwa kama anavyofanya Rais Dkt. Samia.

Rais Dkt. Samia anaendelea kukubalika na Watanzania wengi kutokana na jitihada zake za kuimarisha uchumi, kupambana na rushwa, kutekeleza miradi ya maendeleo inayolenga kuboresha maisha ya wananchi.

Dua hiyo inaonesha jinsi wananchi wanavyothamini na kuzitambua juhudi za Rais Dkt. Samia katika kuliongoza Taifa la Tanzania ili kuboresha maisha yao.
 
IMG_20221017_200817.jpg
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom