Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by EMT, Feb 20, 2011.

 1. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #1
  Feb 20, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  [​IMG]

  Sijui kama hapa ni mahali muafaka kwa hii lakini taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa yule mwarabu anayetajwa kuwa ndiye mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Oman, amemaliza mkutano wake na baadhi ya wahariri katika moja ya hoteli katikati ya jiji.

  Taarifa zinaeleza kuwa amesema yupo tayari kujadiliana na serikali kuhusiana na
  1. Fidia iliyoamriwa kulipwa na
  2. matumizi ya mitambo yake iliyopo Ubungo.

  Yupo tayari kuruhusu izalishe umeme kama makubaliano yatafikiwa.

  Anayedaiwa kuwa mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi, anayeishi Oman, ametua nchini na kuzungumza na vyombo vya habari katika hoteli ya Kilimanjaro Kempinski, Dar es Salaam.

  PATA AUDIO YA BBC HAPA - http://get.ge.tt/4h8evZo/Untitled.mp3
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Feb 20, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280
  Mkuu wa nchi kasepa. mwarabu katia timu.

  kweli hii ishu ya dowans ni dili
   
 3. jmushi1

  jmushi1 JF-Expert Member

  #3
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 2, 2007
  Messages: 17,551
  Likes Received: 1,899
  Trophy Points: 280
  Naona amekuja ku bargain,atatembeza kisu mambo yatakuwa mswanu tu...Nani wa kuizuia serikali?
   
 4. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #4
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Akafie mbele ya safari hili neno DOWANS NI kichefuchefu cha taifa.

  Tutailipua mitambo yake kwa mabomu ya GOMS tena bora aondoke mapema sana
   
 5. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #5
  Feb 20, 2011
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,511
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 145
  Huyo unayemuita mwenye mitambo ya Dowans ni nani? Mitambo ya Dowans ni ya Rostam na kundi lake la mafisadi na huyo atakayejitokeza kujidai anaisemea Dowans (huyo mwarabu) ni owner wa kuchonga katika jitihada za kujaribu kutufanya Watanzania ni wajinga!!!

  Tiba
   
 6. L

  LAT JF-Expert Member

  #6
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  Mkuu... ile mitambo siyo ya DOWANS Tanzania tena ... ilishauzwa kwa kampuni ya Cyprus ... sasa sijui ni mitambo ipi tena
   
 7. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #7
  Feb 20, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Aliulizwa hilo swali, amekana kuwa imeuzwa na anasisitiza kuwa bado anaimiliki yeye
   
 8. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #8
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Yapata siku 3 baada ya gongo la mboto kulipuka,hatimaye mmiliki wa dowans ajitokeza hadharani.

  KUNANI BONGO??
   
 9. L

  LAT JF-Expert Member

  #9
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu ...hapo umenena ... sasa i smell something fishy .... huyu jamaa ankuja na staili ya ustaarabu ... kuna kitu anatafuta huyu... yawezekana kuna kitu mbacho labda kimekosewa kwenye hukumu ya tuzo na kinaweza kufanya wasilipwe anatafuta data sasa.... tunapigwa changa la macho sasa hivi ....
   
 10. Kiherehere

  Kiherehere JF-Expert Member

  #10
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 1,804
  Likes Received: 245
  Trophy Points: 160
  Hii nchi imevalishwa CH**I
   
 11. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #11
  Feb 20, 2011
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Holy crap....
   
 12. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #12
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Nijuavyo huyu alishawahi kuikana iweje leo awe mmiliki.

  Nijuavyo mie huyu bwana kawekeza kwenye kiwanda cha kuchambua pamba lakini kikitumika pia ku-finance mambo ya dini fulani.

  Hili kanyaboya coz mmiliki wa Dowans twamjua ni RA. Je, wamemwuliza ilikuwaje wakatoa PoA yenye mamlaka kubwa kiasi hicho kwa RA wakati si mwanahisa wala mkurugenzi wa Dowans.

  Tatizo waandishi wetu wengi wanaenda kwenye press conference pasi maandalizi
   
 13. E

  Elifasi Senior Member

  #13
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....where r u people? When will you learn to learn? Aaaaagggrrr!
   
 14. Remmy

  Remmy JF-Expert Member

  #14
  Feb 20, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 4,718
  Likes Received: 146
  Trophy Points: 160
  Tunawaomba tuu, hawa wahusika watakao husika kfanya maongezi na huyo jamaa, wafanye kwa busara kubwa na umakini mkubwa sana. tusije tukalia sana.
   
 15. D

  Derimto JF-Expert Member

  #15
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kaka umeongea kitu cha maana sana waandishi wetu sidhani kama wanafanya maandalizi ya kutosha wakati wanakwenda kwenye press confrc. Nyeti kama hizi au vinginevyo wanachukua mshiko au kupangiwa maswali ya kuuliza au kubaguliwa baadhi ya waandishi. Ama kweli sisi ni wadanganyika RA amekaa kimya asubiri mafala tuvae huu uongo wa karne.
   
 16. NIKOSTRATOS

  NIKOSTRATOS Member

  #16
  Feb 20, 2011
  Joined: Feb 20, 2011
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wabongo mnachonga sanaa!Hamna kitu mnafanyaa!
   
 17. L

  LAT JF-Expert Member

  #17
  Feb 20, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 4,523
  Likes Received: 86
  Trophy Points: 0
  mkuu.. mwenzetu wewe ni mzalendo wa nchi gani....?
   
 18. Ole

  Ole JF-Expert Member

  #18
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 16, 2006
  Messages: 751
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hivi hakuna watu wa kwenda kuilipua ile mitambo? Mbona inatupa kero sana?
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Feb 20, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hivi ni wa wapi huyu? Oman au Bahrain? Kama ni Bahrain naona sasa anataka kusepa kwani kuna watu wanataka nchi yao. Na kama ni Oman -- sijui huko kama kuna square kubwa pale mjini Muscat pa kuanzishia mambo kama ya Misri.

  Hata hivyo nadhani anataka hela yake. kama mtakumbuka yaliyokuwa yakiandikwa mwaka 2005, alitoa mamilioni ya dola kumsaidia Mkwere kuingia Mjengoni wakati Mkwere hana hata chapa mfukoni. Si mnakumbuka yaliyoandikwa magazetini mwaka 2005? Sasa huyo Mwarabu anaogopa huenda Mnazi Mmoja ikaanza kama Tahriri na Mkwere akatokea mlango wa nyuma, na asipate hela yake. Ni bora akapewa mapema.
   
 20. Ozzie

  Ozzie JF-Expert Member

  #20
  Feb 20, 2011
  Joined: Oct 9, 2007
  Messages: 3,234
  Likes Received: 38
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji unasemaje? Unaamini taarifa ya huyu jamaa?
   
Loading...