Maelezo ya Brig. Gen. Al-Adawi kuhusu Dowans Feb 20/02/2011

Hili domo mnapiga mnapata wapi muda?Hakuna kitu mtafanya!Mnatia huruma sana!Una maana gani kuniuliza hilo swali?
Crap....kama ni mtz, basi una problew kubwa, kama ni shemeji yetu basi usiongee kabisa...matatizo mliyonayo ni mengi mno.
 
Sijui kama hapa ni mahali muafaka kwa hii lakini taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa yule mwarabu anayetajwa kuwa ndiye mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Oman, amemaliza mkutano wake na baadhi ya wahariri katika moja ya hoteli katikati ya jiji.

Taarifa zinaeleza kuwa amesema yupo tayari kujadiliana na serikali kuhusiana na
1. Fidia iliyoamriwa kulipwa na
2. matumizi ya mitambo yake iliyopo Ubungo.

Yupo tayari kuruhusu izalishe umeme kama makubaliano yatafikiwa.

Kwa hali yoyote na kwa namna yoyote na kwa wakati wote.... hatutaki majadiliano na mazimwi wala watu, mashetani wa kuzimu hawa.... wafe waende kuzimu, ndio nyumbani kwao....
 
Am speechless, inaudhi sana. Unaweza kuporomosha matusi hivihivi

Umeona ehh! halafu kuna watu wanadai walalamikaji wote kuhusu yanayojiri ndani ya nchi yetu ni haters! Ukistaajabu ya Mussa....
 
Nijuavyo huyu alishawahi kuikana iweje leo awe mmiliki.

Nijuavyo mie huyu bwana kawekeza kwenye kiwanda cha kuchambua pamba lakini kikitumika pia ku-finance mambo ya dini fulani.

Hili kanyaboya coz mmiliki wa Dowans twamjua ni RA. Je, wamemwuliza ilikuwaje wakatoa PoA yenye mamlaka kubwa kiasi hicho kwa RA wakati si mwanahisa wala mkurugenzi wa Dowans.

Tatizo waandishi wetu wengi wanaenda kwenye press conference pasi maandalizi

sikilizia watakavyoripoti magazetini... na ukizingatia wamepewa kababu na bahasha nene
 
Nijuavyo huyu alishawahi kuikana iweje leo awe mmiliki.

Nijuavyo mie huyu bwana kawekeza kwenye kiwanda cha kuchambua pamba lakini kikitumika pia ku-finance mambo ya dini fulani.

Hili kanyaboya coz mmiliki wa Dowans twamjua ni RA. Je, wamemwuliza ilikuwaje wakatoa PoA yenye mamlaka kubwa kiasi hicho kwa RA wakati si mwanahisa wala mkurugenzi wa Dowans.

Tatizo waandishi wetu wengi wanaenda kwenye press conference pasi maandalizi

Mkuu nchi yetu imeaoza sekta zte zimeaza na watu wote tumeoza . Kuna hitajika refeorm kwenye kila idara. hata JF yenyewe inahitaji reform.

Usishangae ukisika kuna baadhi ya press conference waandshi wanapewa "bahasa za usafiri"
Sasa hizo bahasha wapi watapata guts za kuuliza mswali yenye HOJA.
 
Nijuavyo huyu alishawahi kuikana iweje leo awe mmiliki.

Nijuavyo mie huyu bwana kawekeza kwenye kiwanda cha kuchambua pamba lakini kikitumika pia ku-finance mambo ya dini fulani.

Hili kanyaboya coz mmiliki wa Dowans twamjua ni RA. Je, wamemwuliza ilikuwaje wakatoa PoA yenye mamlaka kubwa kiasi hicho kwa RA wakati si mwanahisa wala mkurugenzi wa Dowans.

Tatizo waandishi wetu wengi wanaenda kwenye press conference pasi maandalizi

This is the place where we dare to talk openly taja tu hiyo mkuu....
 
SERIKALI na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), bado wanaendelea na mazungumzo ya kununua mitambo ya Dowans, MwanaHALISI limegundua.

"Kwa ushahidi uliopo, madai yote ya kujiondoa katika mjadala wa kununua mitambo ya Dowans ni kiini macho; na mjadala mkubwa juu ya ununuzi ndio hasa umepamba moto," kimeeleza chanzo cha habari.

Taarifa za kuaminika kutoka kwa anayedaiwa kuwa "mmiliki" wa kampuni ya Dowans Holding Tanzania Limited, Jenerali Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE), zinasema serikali imemhakikishia kununua mitambo yake......

Kumbe Ngeleja ule mkwara wake wote kuwa tatizo la mgawo litakuwa ndoto akili zake zote kaziweka huku kwenye DOWANS kuwa ndio suluisho.

Mhhhh kazi ipo
 
mi nadhani siku wakitangaza kuilipa hiyo DOWANS, watu tuandamane kuing'oa hii selekari.
 
mi nadhani siku wakitangaza kuilipa hiyo DOWANS, watu tuandamane kuing'oa hii gavumenti.
 
Hapo atakuambia simjui huyu mmliki kwa sababu siku alipokuja sikuwapo nchini nilikuwa Mauritania

Mambo yanavyo kweda itabidi tusome sana kwenye intenet tujue jinsi ya kuhack simu za ikulu maana hawa viongozi wetu wasioaminika inawezekan ikulu walishaongea naye vizuri. Kahakikishiwa usalama na ndio maana yupo na kapata nguvu hata ya kuitisha press conference

Hivi serikali haujui imani ya wanachi wake inavyzidi kupungua siku hadi siku.? kama hwapati som kwenye mambo yaliyotokea za egypt na tunisia shauri yao.

Politics za nchi yetu zinaudhi sana .

On papers tanzania ni nchi ina sera nzuri kuzidi kenya ,uganda za kupeleka umeme mpaka vijijini . teh teh the lakini In reality watanzania walio mjini ni kazi sana kuupta huo umeme . Sasa jiulize utafikaje huko vijijini.
 
Mkuu usidhani kwasababu mimi nimgeni kwa kujiunga hapa basi nilikuwa sisomi hii jf,nimeisoma tokea ikiwa Jambo Forum....Kama yanayozungumzwa humu yangekuwa yanafanya kazi,basi tungekuwa na serikali ya tofauti hivi sasa.Nasema ni upotevu wa muda kwasababu haya yamezungumzwa tokea 2006 na bado wananchi wameiridhia serikali iendelee na madaraka kwasababu wamefurahishwa na mwelekeo wake.Kelele zilianza kupigwa tokea enzi za buzwagi,EPA,Richmond ambayo sasa ndo imegeuzwa imekuwa new topic kama unavyotaka tuelewe?Ama kwasababu tu sasa ni dowans na huyo sijui mmiliki anakuja?whats the difference?Richmond aka dowans ilipokuja wananchi walijua na bado wanajua na bado walimchagua JK na serikali yake kuendeleza maendeleo ya umeme nk.

Mimi nadhani ni bora tujadili kama mngekuwa ni alternative government mngefanya nini nk,mnakuwa kama think tank na si kama sokoni ambapo hakuna anayemsikiliza mwenziye,ni full mikelele isiyo na mpango,yani domo tuu!Hakuna la maana!

Unless kama kuna hatua za kuchukuliwa ambazo wananchi tunaweza kuzitumia ili kudai haki yetu na uwajibikaji wa viongozi,lakini kama demokrasia ilivyo,kama wengi wa wananchi wenzangu ni wajinga,then kupiga kelele hakusaidii,ni bora kutafuta namna ya kuwafuta ujinga huo hao wananchi ili waelewe next time wakipiga kura na kuona uchaguzi haukuwa wa huru ama wa haki,basi wakatae matokeo nk,kupiga domo tu haisadiii na wataendelea kupeta kwasababu kelele hizo kwa wananchi ni kama kupiga gitaa kwa mbuzi kwani majani ataendelea kuyachana tu mbuzi huyo bila woga wala wasiwasi....Sasa kwani sisi kujua kuwa eti huyo "Mmiliki" wa mitambo yuko bongo ni a game changer?

Prove to me kama hampotezi muda,na uje na ushahidi kama nilivyofanya!

Otherwise mibongo ndivyo tulivyo,hakuna jinsi,sana sana tuigeuze JF iwe pahala pa kupeana dili nk,kwenye siasa tunapoteza muda tu.

Mkuu hayo ni maneno ya aliyekata tamaa, vijana wa mitaani wangesema "Kwasababu wamemwaga ugali basi nasi tumwage mboga"!. Hapo nchi itakuwa imefika mwisho......!

Wewe kama ni mtanzania uliyebahatika kuelewa hali ya ufisadi mapema basi ujue unao wajibu wa kuwajulisha wenzio ili kuondokana na taifa lisilo na mwelekeo. Timiza wajibu wako kwa nafasi uliyonayo!

Kumbuka kila kitu kina mwisho. Wananchi wa Misri walikuwa wavumilivu kwa zaidi ya miaka 30 lakin arobain za watawala zimefika na wameondoka!

Sijui kama hapa ni mahali muafaka kwa hii lakini taarifa zilizonifikia hivi punde ni kuwa yule mwarabu anayetajwa kuwa ndiye mmiliki wa Dowans, Brigedia Jenerali (mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi wa Oman, amemaliza mkutano wake na baadhi ya wahariri katika moja ya hoteli katikati ya jiji.

Taarifa zinaeleza kuwa amesema yupo tayari kujadiliana na serikali kuhusiana na
1. Fidia iliyoamriwa kulipwa na
2. matumizi ya mitambo yake iliyopo Ubungo.

Yupo tayari kuruhusu izalishe umeme kama makubaliano yatafikiwa.

Hebu tujikumbushwe haya matukio:
  1. Katika kikao cha wabunge wa ccm na mkuu wa kaya; Wazo linatolewa eti "Au tujadiliane nao (Dowans) kuhusu kupunguzwa kwa fidia"
  2. Huko bungeni; Pendekezo linatolewa na January Makamba eti " Tuzungumze na wamiliki wa Dowans ili tupate mkataba wa muda tuwashe mitambo yao ya Ubungo!
Sitashangaa kusikia makubaliono tayari yamefikiwa!

Hivi sisi watanzania tuna matatizo gani katika akili zetu?
 
kwa wale wajanja enzi zile, mnakumbuka ule mchezo ambao unamakosa shule halafu unaambiwa mlete mzazi wako? unachofana ni kwenda kumlipa mtu anajifanya mzazi wako then unamaliza soo bila ya home kujua.
ndio haya ya rostam, kwake kumlipa mtu ili ajifanya ni mmiliki wa dowans sio dili wala nini.

nawakilisha
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom