Kujitokeza kwa Al Adawi, Mwanakijiji ameshindwa au kaumbuka? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kujitokeza kwa Al Adawi, Mwanakijiji ameshindwa au kaumbuka?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Alfu Lela Ulela, Feb 23, 2011.

 1. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #1
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Brigedia Jenerali mstaafu, Suleman Mohamed Yahya Al Adawi wa Saud Arabia amejitokeza hadharani na kudai kuwa mmiliki wa kampuni ya DOWANS (T) LTD.

  Al Adawi ambaye alifanya mkutano na waandishi wa habari jumapili ya tar.19/02/2011 ktk ukumbi wa Hotel ya Kilimanjaro Kempisk, pamoja na kuwa alitoa maelezo yaliyoacha maswali mengi kwa Watanzania lakini pia maelezo yake hayamuachi salama mwandishi mkongwe na ambaye tumekuwa tukimhesabu kama shujaa ktk jamvi hili MM.MWANAKIJIJI.

  Katika taarifa kupitia vyombo mbalimbali vya habari kwa nyakati tofauti, (hususan gazeti makini la MwanaHALISI) imekuwa ikidaiwa AL ADAWI amewahi kukanusha kuimiliki kampuni ya Dowans (T) Ltd.

  Taarifa za kukanusha umiliki wa kampuni hiyo inadaiwa zinatokana na mahojiano yaliyofanywa kati ya mwandishi huyo aishie Marekani na AL Adawi mwenyewe.

  Lakini AL Adawi amekuja nchini na kudai kuimiliki kampuni hiyo, tofauti na alipohojiwa na Mwanakijiji ambapo alikana.

  Hii ina maana kuwa maelezo ambayo AL Adawi aliyatoa kwa mwandishi huyo wa Marekani, ni tofauti na aliyoyatoa kwa waandishi wa Tanzania.

  Je ukweli ni upi? Je, Mwanakijiji haoni kuwa maelezo ya AL Adawi yanamuweka hatarini kwa kuonekana alitunga story??

  Najua Mwanakijiji atakuwa amesikia taarifa ya Al Adawi kukiri kuimiliki Dowans. Je,amechukua hatua gani kuudhibitishia umma wa watanzania na dunia kwa ujumla kuwa hakutunga story?

  Na je, Mwanakijiji haoni kuwa taarifa ya AL Adawi inamuumbua, na asipochukua juhudi za haraka, imani aliyojijengea miongoni mwa Watanzania wengi itapotea? TAFAKARI!!
   
 2. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #2
  Feb 23, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  we kurupuka tu; nimezungumza naye leo.... na kama nilivyosema nasubiri serikali yenu imlipe kwanza ndio tutawawekeza huo mgongano wa hoja. Nilitunga vipi stori wakati kinyume na maelezo uliyoyasoma sauti yake ilisikika akiikana Dowans? au wewe hukumsikia?
   
 3. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #3
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwanakijiji hao ndio sehemu ya dowans wametumwa Heshima yako iko juu na kazi zako tunazithamini. Asikuvunje moyo huyo.
   
 4. k

  komredi ngosha JF-Expert Member

  #4
  Feb 23, 2011
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 381
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  kaka, mimi naku admire sana. Wewe ni shujaa wa Tanzania.
   
 5. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #5
  Feb 23, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ndugu yangu Mwanakijiji, nimekufahamu kwa muda mrefu kupitia humu jamvini na sehemu nyingine kwa nguvu ya hoja zako zilizojaa ukweli na uhakika . Nakuheshimu sana na naheshimu mawazo yako pia. Ila nadhani umenitafsiri kinyume.

  Sijasema umeumbuka wala siwezi kuthubutu kusema hivyo. Ila nimehoji. Thread yangu ukiisoma vizuri utagundua si taarifa (statement) bali nimehoji. Nia yangu ni kutaka kujua uhalali wa Adawi kuikubali DOWANS wakati alishaikana kwenye interview yako.

  Narudia tena, mimi nimehoji tu. Na sidhani kama nimefanya makosa kuhoji. Im sorry for any incoviniece that happened kama ulinitafsiri tofauti na nilivyokusudia. Ila naamini ilikuwa haki yangu kuhoji na kujibiwa ipasavyo.
   
 6. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #6
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kaka Mashikolo hiyo uliyojijengea ni kasumba na sidhani kama ni nzuri kwa great thinker. Ni vema ukaelewa kuwa kuna tofauti kati ya kuhoji na kutoa taarifa. Mimi nimehoji, na Mwanakijiji alipaswa ajibu hoja ili kuniweka sawa mimi na watanzania wenzangu ambao taarifa hizi zimetukanganya.

  Lakini badala yake umeanza kunishutumu vikali labda kwa kuwa nimemgusa Mwanakijiji. Jamani, we as great thinkers ni vema tukapingana na HOJA na SI MTOA HOJA.

  Ni vema tukajaribu kuzijibu hoja kwa kuzikubali au kuzikataa bila kuangalia mahusiano yetu na mtoa hoja.

  Binafsi namheshimu Manakijiji na wanajamvi wote ambao hoja zao zimekuwa na tija/manufaa kwa taifa. Mwanakijiji is one of my role models. He is my hero,na wakati fulani idea zake zimekuwa zikiongoza maisha yangu.

  Hivyo hoja yako kuwa nimetumwa si sahihi. Mimi ni mwanaharakati kwa asili na kwa akili, hivyo siwezi kutumwa na yeyote.

  Tafadhali ondoa fikra kuwa kila ambaye hukubaliani nae hoja ametumwa. Si kweli. Sisi kama great thinkers ni muhimu tukubali kutokukubaliana.

  Mawazo kuwa kila ambaye hukubaliani nae hoja ametumwa ni mawazo potofu. Wakati fulani mwanafalsafa wa kale John Locke aliwahi kusema ".....kuna mambo ambayo hatukubaliani nayo,lakini hatuna budi kuyaheshimu"
   
 7. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #7
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,362
  Likes Received: 6,393
  Trophy Points: 280
  najua jinsi ya kutumia maneno vizuri sana; hukuhoji bali umeashiria; kwa sababu ingekuwa ni maandishi niliysema "alichosema" basi ningeweza kuwa nimetunga kama ulivyo"hoji". Sasa yeye alisikika akisema kuwa haijui Dowans.. sasa leo anakuja na kusema anaimili.. iweje mimi ndio niumbuke kwa kitu alichokisema yeye? Labda swali lako la kuhoji ungeliweka sawasawa kwanini yeye aliyeikataa Dowans sasa aikubali?
   
 8. A

  Alfu Lela Ulela JF-Expert Member

  #8
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 1,255
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimekuelewa. Nadhani tatizo ni kuwa kichwa cha thread kinaonekana kukudout, tofauti na maelezo ya thread yenyewe.

  Katika hili nikiri kuwa nimekosea na nikubaliane na wewe kuwa heading of the thread ina mapungufu. Labda heading ingekuwa "Al Adawi kuikataa Dowans na baadae kukubali kuimiliki, je ni utashi wake au kuna nguvu nyuma yake??"

  Yamkini kichwa kingekuwa hivyo (bila kubadilisha chochote kwny content) thread isingekuwa na matatizo.

  Therefore Im sory for any incovinience that happened to you knowingly or unknowingly because was not my intention. You are highly appreciated sir. You are my role model!
   
 9. M

  Mutu JF-Expert Member

  #9
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mtoa hojauna hadithinzuri ilaumeshindwakuumba maneno..kichwa cha thread maneno kwenye body na utetezi wa maneno yako zinakidhana .

  Kwanza mwandishi wa habari anaumbuka vp kwa maneno ya aliyemuhoji yakiwa ndivyo sivyo.

  Kwa kifupi kama shutuma si za reporter ni busara ukasoma thread yako na kurekebisha palipo muhimu kurekiebisha.
   
 10. M

  Mutu JF-Expert Member

  #10
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  ok sorry kumbe umeona na ww basi unaweza ignore maneno yangu hapo juu,vinginevyo habari yako nzuri
   
 11. j

  junior2008 JF-Expert Member

  #11
  Feb 24, 2011
  Joined: Apr 27, 2009
  Messages: 528
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo swali alitakiwa aulizwe Al Adawi na waandishi wa habari alipokuja bongo. Sijui kama walifanya hivyo au ndio walipangiwa na maswali ya kuuliza?
   
 12. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #12
  Feb 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,913
  Likes Received: 12,073
  Trophy Points: 280
  Inavyoonekana watu wamefurahi sana kwa ujio wa Al Adawi, tapeli ni tapeli tu kama waliweza kuingia mikataba feki watashindwa kuleta mmiliki feki.
   
 13. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #13
  Feb 24, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Hivi ni kwa nini mmiliki wa Dowans kaondoka in a hurry bila kutatua tatizo lililopo. Je, amelipwa mpunga wake? Je, ameahidiwa nini? Je ilikuwaje aondoke bila kuonana na wanahabari kujibu chokochoko zao? Je, alihofia kuburuzwa na takukuru? Ilikuwaje aonane na makamu wa rais wakati mikataba yake inaonekana ni ya kishikajishikaji zaidi. Hivi matapeli nao wanaweza kwenda Ikulu ili mradi tu pochi yao ni kubwa? Je kwa nini aende Ikulu na sio tanesco ambao ndio wana mkataba naye. Je alionana na kiongozi yeyote wa Tanesco? Vipi TRA wanaidai hii kampuni chochote?
   
 14. Madela Wa- Madilu

  Madela Wa- Madilu JF-Expert Member

  #14
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 24, 2007
  Messages: 3,074
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 135
  Wewe ni NDUMILAKUTATU.
  Na huna haja ya kujitetea kutaka kurekebisha maoni au mtazamo wako.
  Behind the scene kuna jambo unalosherehekea. Tatizo hukujua kwamba maneno yako yatakurudia mwenyewe ndani ya muda mfupi.
  Wewe ni NDUMILAKUTATU.

  Kama usingekuwa na tabia hiyo ungeuliza kwa namna nyingine kabisa kuliko kuamua kuwa upande mmoja.
  Kwa nini kichwa cha habari kisiulize kujiumbua kwa Al Adawi??
  KWa nini usinge hoji au kuuliza "Ukweli ni Upi"

  Lakini umeamua kukaa upande wa MAFISADI na Wahuni toka Serikali ya CCM na kuandika kichwa cha Habari

  "Kujitokeza kwa Al Adawi, Mwanakijiji ameshindwa au kaumbuka?"


  Acha Uhuni wa kuiga.

   
 15. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #15
  Feb 24, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,913
  Likes Received: 12,073
  Trophy Points: 280
  Al Adawi hana tofauti na vishoka wa Tanesco wanaounganisha umeme wa wizi wakiona polisi wanakuwa na wasiwasi nafikiri nayeye kaogopa Interpol, labda tuwaulize wanaomshabikia kwanini kaondoka haraka haraka hivi.
   
 16. Pakawa

  Pakawa JF-Expert Member

  #16
  Feb 24, 2011
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,737
  Likes Received: 3,172
  Trophy Points: 280
  Nimecheka Mwanakijiji ulivyomjibu 'eti we kurupuka tu' hahahh msg.sent natumaini atakuwa amekuelewa mkuu.
   
 17. Gsana

  Gsana JF-Expert Member

  #17
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 4,387
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mi naona mungemuelewa mtoa mada. Tangu mwanzo kila mtu anaweza kuhoji kama mtoa mada alivohoji,japo mtu unahoji ukijua jibu kuwa al aldaiwi ni msanii. Mwanakijiji alitueleza stepu kwa stepu alivokuwa anamhoji na aliweka ushaidi apa jf,kama watawala wamempanga akapangika basi apa tunaona msanii nani. Rejea pia RA aliweka wazi kuwa haijui wala hausiki Dowans, ali alidaiwi anasema alimkabidi power of attoney fisadRA,ujumla wa adithi ya fisadi uyu unampa mwanakijiji umaarufu,tena mkubwa pale ambapo uyu aldaiwi anapojikoroga wakati mwanakijiji ana ushaidi hata wa sauti ya uyu fisadi.
   
 18. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #18
  Feb 24, 2011
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Mwanakijiji,HESHIMA kwako.
  Kwa kweli binafsi nina appreciate sana mchango wako hapa jamvini na jinsi unatumia muda mwingi kutafiti kabla ya kkujenga hoja yoyote.
  Nimewasoma wachangiaji wa thread hii na kwa heshima naona ume overreact unnecessarily.
  Tunaandika wengi humu lakini naamini aliyeanzisha thread hii alikuwa na nia ya ku provoke discussion na ikiwezekana uumwage ushahidi zaidi.
  Niwie radhi mkuu wangu.
   
 19. b

  bulunga JF-Expert Member

  #19
  Feb 24, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 290
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  MK, naomba iweke tena hiyo interview tuweze kusikia na kufupisha malumbano wengine tuli i miss!!
   
 20. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #20
  Feb 24, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,596
  Likes Received: 3,887
  Trophy Points: 280
  Al Adawi yeye ndiye alijichanganya, swala la kuwa mwanakijiji alimuhoji si Mwanakijiji peke yake, nadhani hapa wengi huwa wanakosea hili

  Mwanakiji alimuhoji na akatoa taarifa kama mwandishi wa habari, swala la huyu kibosile kuikana Dowans alilikana kwa watu wengi wakiwemo usalama wa taifa. Al Adawi si mgeni nchi hii! msije mkamuona malaika anaifahamu Tanzania in and out! mapumziko mengi anakuja Tz.

  Amekuja kukiri baada ya kulazimishwa sana hivyo kumuokoa JK na Rostam, JK kalidanganya taifa kuwa hamjui mmiliki wakati ni mfadhili mubwa tu wa CCM. Adawi alichokifanyia nchi hii asingeweza kufanya nchi zingine.

  Aliyeumbuka ni JK na Rostam wake

  aidha mimi personally sijafurahia na vita hii ya Dowans maana inaficha wengi wanaofanya uhalifu, Al Adawi siyo tatizo! tatizo ni system zetu na wengi hawawataji nani alihusika from A to Z kulifanya hili swala liwe..Dowans to me has never been problem, problem ni weusi wenzetu ambao ndio purposefully wamefanya mjadala uwe wa Adawi na Rostam na siyo TANESCO, BRELA n.k we have big problem maana tatizo siyo dowans we have many like dowans WHO IS ENTERTAINING THIS??
   
Loading...