Madudu ya Usangu Logistics, Wizara ya kazi mpo wapi?

Beman

Member
Joined
Aug 1, 2021
Posts
15
Reaction score
26
MADUDU YA USANGU LOGISTICS-WIZARA YA KAZI MPO WAPI

Utangulizi:
Ndg zangu,hii kampuni ni ya usafirishaji na makao ya ofisi ipo Tabata Matumbi.Wamiliki wa kampuni hii ni waburushi (Mwakabanga) ambao walianza wa tatu, kama madereva wakiwa wanaenda masafa marefu hadi kufikisha magari zaidi ya mia mbili leo hii.

Ila kwa masikitiko makubwa kabisa, waajiriwa wa kampuni hii wanapata mateso bila chuki kila kukicha. Wafanyakazi wa kampuni hii wananyanyaswa kwa kukatwa hela bila sababu za msingi kwenye mishahara yao inapokua inaingia, kufanya kazi bila mikataba, kupigwa, kucheleweshewa mishahara (mishahara kuingia tarehe isiojulikana),na pia wamiliki wa kampuni hii hutumia nafasi zao kutembea na wanawake waliowaajiri.

Hivyo basi, nikiwa naamini kuna sheria za kazi zinazomlinda mwajiri na mwajiriwa.

Naombeni vyombo husika kufatilia maswala hayo yaliosemwa hapo juu ili iwasaidie wafanyakazi waliopo katika kampuni hiyo.

Naombeni kuwakilisha.Mjumbe hauwawi!
 
Uzi umekaa kimajungu.

Hao wanawake huwa wanabakwa ? Liko wazi Wanawake wanapenda hela, sasa anaanzaje kumkataa bosi wake mwenye malori 200.

Pili umeweka historia hao jamaa walianza watatu kama madereva malori na wakapambana hadi kufikisha malori zaidi ya 200.

Sasa why na wewe usipambane kupata mali zako.

Why ung'ang'anie ajira ya mtu inayokupa manyanyaso
 
Ustaarabu ni jambo jema sana, elewa wenzako wanateseka wewe unaleta kebehi na dharau!
NI VYEMA UNGEKAA KIMYA WENYE MAMLAKA WALIFANYIE KAZI.
Tofautisha majungu ambayo yako mengi tu sehemu za kazi na katika biashara na ukweli wa mtu anyetaka mambo yake kuyatatua.
Kwanza mtu huyo hajui Ofisi za Kazi?

Mtu anaomgea kimafumbo , ati hawatulipi, wanatembea na dada zetu, walikuwa na magari matatu sasa yako mia mbili!

Huu ni upuuzi mtupu kwa mtu asiyetaka kushirikisha ubonga wake na anategemea kutajirika kwa kuajiriwa.
Ukiwa na mawazo kama ya huyo mtoa mada basi huna toauti na mijitu mbumbumbu ambayo haijui kwa nini inaishi duniani
 
Tofautisha majungu ambayo yako mengi tu sehemu za kazi na katika biashara na ukweli wa mtu anyetaka mambo yake kuyatatua.
Kwanza mtu huyo hajui Ofisi za Kazi?....
Uwezo wako wa kufikiria ni mdogo sana...na hata hivyo sio kosa lako!
 
MADUDU YA USANGU LOGISTICS-WIZARA YA KAZI MPO WAPI

Utangulizi:
Ndg zangu,hii kampuni ni ya usafirishaji na makao ya ofisi ipo Tabata Matumbi.Wamiliki wa kampuni hii ni waburushi(Mwakabanga) ambao walianza wa tatu, kama madereva wakiwa wanaenda masafa marefu hadi kufikisha magari zaidi ya mia mbili leo hii...
wanajihusisha na usafirishaji wa bidhaa gani?
 
MADUDU YA USANGU LOGISTICS-WIZARA YA KAZI MPO WAPI

Utangulizi:
Ndg zangu,hii kampuni ni ya usafirishaji na makao ya ofisi ipo Tabata Matumbi.Wamiliki wa kampuni hii ni waburushi(Mwakabanga) ambao walianza wa tatu, kama madereva wakiwa wanaenda masafa marefu hadi kufikisha magari zaidi ya mia mbili leo hii...
Mtanzania bwana ni shida, sasa kama kampuni sio ya umma mna ng'ang'ania ya nini? Kwani lazima? Kwanini na nyie msianzishe ya kwenu hata kama mko watano? Kama wanawanyanyasa si muwaachie waburushi kampuni yao wabaki wenyewe! Mambo ya kuja kutusumbua hapa na mada zisizotuhusu muache
 
Tatizo watu wanataka watajirike kwa kuajiriwa.
Mentality ya kufiiri kuna hela ya bure mahali!
 
MADUDU YA USANGU LOGISTICS-WIZARA YA KAZI MPO WAPI

Utangulizi:
Ndg zangu,hii kampuni ni ya usafirishaji na makao ya ofisi ipo Tabata Matumbi.Wamiliki wa kampuni hii ni waburushi (Mwakabanga) ambao walianza wa tatu, kama madereva wakiwa wanaenda masafa marefu hadi kufikisha magari zaidi ya mia mbili leo hii.

Ila kwa masikitiko makubwa kabisa, waajiriwa wa kampuni hii wanapata mateso bila chuki kila kukicha. Wafanyakazi wa kampuni hii wananyanyaswa kwa kukatwa hela bila sababu za msingi kwenye mishahara yao inapokua inaingia, kufanya kazi bila mikataba, kupigwa, kucheleweshewa mishahara (mishahara kuingia tarehe isiojulikana),na pia wamiliki wa kampuni hii hutumia nafasi zao kutembea na wanawake waliowaajiri.

Hivyo basi, nikiwa naamini kuna sheria za kazi zinazomlinda mwajiri na mwajiriwa.

Naombeni vyombo husika kufatilia maswala hayo yaliosemwa hapo juu ili iwasaidie wafanyakazi waliopo katika kampuni hiyo.

Naombeni kuwakilisha.Mjumbe hauwawi!
Unawasagia kunguni
 
Back
Top Bottom