Madudu haya ya ajabu ya kisheria yaliweza kufanyika vipi wakati tuna Wanasheria?

Msimila si na wewe umesomea sheria?hata hizo mahakama pia ni batili sababu hazitendi haki.haki ktk nchi hii imeporwa na wenye fedha.upuuzi huu utaendelea mpaka hapo watz watakapojielewa na kuzipindua hizo mahakama pamoja na watendaji wake.
 
Kubwabwaja tu bila kuorodhesha hata hizo sheria mbovu ni zipi, kwa nini ni mbovu na nini kifanyike. Kunadhihirisha wewe ni kundi moja na hao wanasheria uchwara unaowasagia kunguni
 

Umeandika vizuri sana sana, umelalamika kizalendo sana, constitutional rights and freedom as enablers of empowering professional autonomous be it private individuals, groups of individuals, government instructions, etc does not exist, threats is the order of the day. Critics, criticism is never healthy in Tanzania.

Dhana ya unyani, ujima, utumwa, umwinyi, ukoloni, ufalme inafugwa na wapumbavu ambao upumbavu huo msingi wao ni uwoga, ubinafsi na ufedhuli.
 
nimesema suluhisho ni kuzivunja hizo mahakama na watendaji wake be it peacefully or otherwise.mahakimu na majaji wote waondolewe ndo chanzo cha ujinga wote huo unaoendelea ndani ya mhimili huo.vinginevyo haki za wanyonge zitaendelea kuporwa.
 
Katika vitu vinavyokushusha chini Pascal Mayalla !

Ni pamoja ba unafiki wako,kwa kumaanisha kwamba sio muwazi unaeweza kutoka na kusema unachokisimamia na kukiamini.

Machapisho yako yanakunyima nafasi,sababu kila upande huwa unashindwa kuelewa kama uko nao au la!

Mfano mdogo hapa!

Wewe ni mwanasheria na pia mwandishi nguli.
Umeshindwa nini kwenye Makala yako,kwenda direct kwenye kuzitaja hizo sheria zenye mapungufu na ambazo ni batili.

Umetumia muda mwingi na ukurasa mzima kurudia rudia jbo lile lile kwa sababu zako uzijuazo ninafsi.

Na hapo ndio panapofanya usiaminike......

Wewe na Zitto mnaelejea kuwa na unasaba fulani katika mtindo wenu kimaisha,kupitia taaluma zenu.
 
Dalili ya kwanza ya binadamu kukosa akili ni kupenda sheria badala ya haki ....watz wengi hasa wanasheria wanashindwa kutofautisha sheria na haki ...ushahidi ni huu msemo "hakuna haki bila wajibu" ukweli ni kwamba haki ipo hata bila ya wajibu ..mfano ..mfanyakazi asiye taka kufanya kazi haki yake ni kutokulipwa mshahara sasa utasemaje hakuna haki bila wajibu ...ndiyo maana mimi nikisikia mtu ana amini kuwa sheria ndiyo msingi wa maisha mazuri huyo namwona mpumbavu ...utasikia tunataka "utawala wa sheria" ni ujinga kama tundu lissu alivyo jidhihilisha upumbavu wake kwa kusema "tutashitakiwa miga" je alimaanisha tuogope kushitakiwa *** kwanini asiseme tutapatikana na hatia miga maana kushitakiwa siyo kupatikana na hatia.
 
Ukiandika hiki kipande wakati wa utawala wa dictator Jiwe lingekuwa jambo lenye uzito unaostahili
 
Umezungumzia Wana Sheria lakini umewaacha wanasiasa hasa wa upinzani ndio maana nasema marehemu Mtikila alikuwa mpinzani wa aina yake kama angekuwepo angeshaenda mahakamani na kuichallenge serikali na alishafanya hovyo kwenye Sheria ya mgombea binafsi.

Wakati limetolewa tamko la kuzuia mikutano ya kisiasa ccm Bado waliendelea kufanya mikutano lakini vyama vingine vilikuwa vinasubiri hisani ya rais.

Labda nikukumbushe uvunjajwi wa katiba haujaanza Leo kwani mabadiliko yaliyofanyika kuondoa swala la gesi na mafuta halikufanywa Kwa mujibu wa katiba lakini wote wamekaa kimya ila utaona wanavyojiita wasomi lakini wangefanya nusu ya wajibu wao hata misongamano ya mahabusu ingepungua
 
Halafu ajabu kubwa zaidi kupita yote, ni huyu mwandishi anayeuliza kama tuna wanasheria wa kweli, ambaye nae kila siku huwatetea wale wanawake 19 kule bungeni kwa manufaa ya chama chao, lakini chakushangaza, amekuja hapa kutuuliza kama Tanzania tuna wanasheria wa kweli au vibogoyo..

Jibu langu kwake ni fupi tu, tuna wanasheria vibogoyo, na mfano wao ni yeye mwenyewe..
Pascal ni mnafiki sana.
 
Mzee wangu, wakili mwenzangu Pascal Mayalla kuna vitu ama kwa makusudi umevieleza ili kutia chachu wanataaluma ya sheria lakini kuna namna na wewe kama wakili msomi umekuwa mlalamishi.

Kwanini nasema hivyo?
1. Umekwepa kabisa kueleza bayana hayo yaliyofanyika na hili naamini umefanya kwa makusudi, sasa hili linaleta hali ya taharuki, watu watashindwa kupima uliyoyasema na uhalisia.

Nijaribu kufungua hii pandora, kama unazungumzia mabadiliko ya BRADEA yaliyokwenda kubadili kinyemela baadhi ya Ibara za Katiba ya nchi, hakika utakuwa hujamtendea haki mwanataaluma nguli kabisa nchini Profesa Isa Shivji, kwani ameliongelea mara kadhaa swala hili hadi kuandika na makala.

Lakini pia kama utakuwa unaongelea kuhusu suala la haki ya dhamana ambalo nalo Mahakama ilikwishatamka kuwa kile kifungu cha sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kuwa ni batili na kinyume na katiba, basi utakuwa hujamtendea haki mwanataaluma mwingine Mheshimiwa Jaji Mkuu, Profesa Ibrahim Juma, kwani na yeye amekwisha kuwahi kulizungumzia.hili tena kwa kuandika makala kabisa juu ya dhamana kuwa haki kikatiba.

Hapo nimejaribu kufungua pandora kujua ni kipi hasa unachokilalamikia kama sio kukizungumzia, wakili msomi.

2. Umeshindwa kabisa kutenganisha majukumu kwa kila eneo la kiutendaji walipo wanasheria, msomi umeshindwa au.umeacha kabisa kueleza kuwa kazi ya kubadili sheria hizo ipo kwa nani chini ya utaratibu gani ili watu wapime je tatizo lipo kwa nani hasa.

hapa nifafanue mchakato wa kubadili sheria hizo japo kwa ufupi kwa kuwaweka wahusika.

Msomi tutakubaliana kuwa Mahakama inatoa uamuzi wake kisha utekelezaji unafanywa na vyombo vingine kwenye.minajili ya mada hii. Sasa vyombo hivyo vinamjumuisha.wanasheria.Mkuu wa serikali, wizara husika na mpiga chapa mkuu wa bunge (sijui kama ni kiswahili sahihi) au Chief Parliamentary Draftman na mtu mwingine ambaye anajificha sana Wakili wa Bunge.

Sasa hawa wote ukiwaangalia wanatoka mihimili miwili, Serikali na Bunge. Kwa kuwashambulia wanasheria wote ukiwepo pia msomi na kuhoji kama wapo ni kukosea sana na kutupa mzigo kusikotakiwa kwani hata tukisema tuwenge nguvu sisi kama sisi sio watendaji wa hilo swala zaidi tutakuwa ama wahamasishaji au walalamikaji (vitu ambavyo vinafanyika kila siku), sasa tujiulize je misingi ya kitaaluma inatutaka tuwe hivyo?, jibu ni hapana kwani zipo njia sahihi juu ya hayo na huwa zinafuatwa.

Juu ya hili naweza kusema kuwa hoja yako wakili msomi umeielekeza hadi kwa watu ambao kimsingi sio watendaji wa maswala hayo.

Yapo mengi lakini kwa sasa naomba niishie hapa nitaeleza zaidi kadiri mjadala wa uzi huu utakavyoelekea msomi
 

Haya unayongea Paskali ni kama unafurahisha genge tu. Ww ni mfano halisi wa wasomi hewa ndani ya nchi hii.
 
Swali lingine, je tuna bunge makini, linfanya kazi gani?
Pili ndugu unayeleta mada hii leo, ulikuwa unaogopa nini?
 
Anza na nyerere, elewa chama dola na ugonjwa unaitwa "ukondoo wa nyere" na hapa ndio wakazaliwa waoga, watafuta fursa, na wachumia tumbo. Na hao wako kila profession. Na kama haitoshi ongeza chawa na wanafiki. Ukija kwa hao lawyers hayo yote yana apply. Nyeĺrere ingawapo ni mhusika mkuu alituasa juu ya katiba yetu na jpm akahitimisha.
Watanzania wenye ujasiri wa kusimamia haki ni wachache ssana tunawajua na kuwapa majina ya ajabu. Nani atavunja uchama dola na ukondoo wa nyerere?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…