Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,862
5,797
HABARI

Na Godfrey Kahango, Mbarali. (email the author)

Posted Ijumaa,Mei24 2013 saa 21:56 PM

KWA UFUPI

  • Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wametoa mapendekezo yao juu ya mchakato wa kuugawa Mkoa wa Mbeya, ili kupata mikoa miwili kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya, wametoa mapendekezo yao juu ya mchakato wa kuugawa Mkoa wa Mbeya, ili kupata mikoa miwili kwa lengo la kusogeza huduma kwa wananchi.

Mchakato huo unakuja baada Serikali ya Mkoa wa Mbeya, kumwomba Rais Jakaya Kikwete kuugawa mkoa huo, ili kutoa unafuu kwa watendaji wa Serikali katika kuwahudumia wananchi.

Habari zilisema tayari Rais Kikwete ameridhia maombi hayo na kuagiza kufanyika kwa mchakato huo.

Kw upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, amewataka madiwani wa hamashauri zote kuketi na kuanza mchakato wa mapendekezo kuhusu namna ya kuugawa mkoa huo.

Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali walitoa mapendekezo yao juzi katika kikao chao.

Akisoma taarifa ya mapendekezo hayo katibu wa baraza hilo, Brown Mwakibete, alisema timu

ya wataalamu iliketi na kutafakari kwa kina namna ya kuugawa mkoa huo kwa kuzingatia maagizo ya mkuu wa mkoa.

Diwani Mwakibete, alisema madiwani wa halmashauri hyo wamependekeza jina la mkoa mpya liwe Rungwe ukiwa na Wilaya za Kyela, Rungwe,

Ileje na Mbozi na makao makuu ya yawe Tukuyu.

Alisema pia wametaka jina la mkoa wa zamani libaki kuwa Mbeya ukiwa na Wilaya za Momba, Chunya, Mbeya na Mbarali na Makao makuu yakiwa Mbeya.

Alisema kamati hiyo haikuona haja yaa kuanzisha wilaya mpya kutokana na sababu za kijiografia.
 
Kuwa na MIKOA MINGI sio UFANISI... ni UFISADI ndani ya CHAMA TAWALA; Wanaitajika VIONGOZI IMARA; Wanaopenda NCHI yao; Sio Wanafiki - Wanaimba KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI; Nyuma yake ni MABEPARI wa kupindukia na Wanakana hilo...

CCM ni Chama cha KIPEBARI lakini kinadanganya Wananchi; Hakitaki kusema ndani ya NCHI itikadi zake ni NINI...
Ndio maana Maendeleo Mengi Yanashindikana... UNAFIKI sio NGUZO ya MAENDELEO!!!

Sasa Wanataka kuigawa nchi kuwa na MIKOA 100 ili??? UKABILA ushamiri????
 
Mkuu waache, wenyewe wataikubali sera ya majimbo ya Chadema
 
Hao madiwani wanatumiwa na hawajui walifanyalo; wengi wao hapo ni ndio MZEE, ukizingatia wengi wao elimu zao ziko mashakani.

Nani aliye waambia ati wananchi wana shida ya kumuona mkuu wa mkoa ?
By ze way Mkuu wa Mkoa anafanya kazi gani kama siyo kuongeza kasi ya ufisadi ?
 
Huku ni kuongeza matumizi ya fedha,UWEPO WA MKOA HUO MPYA HAUTAKUWA NA MANUFAA,..Magamba wanawaza machimbo mapya
 
Siyo mbaya wakigawa ila sera ya majimbo bado lipo pale pale hapa ndipo huduma zitakaposogezwa karibu na wananchi.
 
Hakuna kuwa na mkoa kama Pwani ndani ya Dar. Hakuna kiungo cha Rungwe na Mbozi kupitia Ileje lazma utokee Mbeya. Labda makao makuu yawe katka Wilaya ya Ileje na kuchukua baadhi kata za Mbeya Vijijini
 
Hao madiwani wanatumiwa na hawajui walifanyalo; wengi wao hapo ni ndio MZEE, ukizingatia wengi wao elimu zao ziko mashakani.

Nani aliye waambia ati wananchi wana shida ya kumuona mkuu wa mkoa ?
By ze way Mkuu wa Mkoa anafanya kazi gani kama siyo kuongeza kasi ya ufisadi ?

kuhusu elimu umenena mkuu madiwani wengi mbarali ni darasa la saba na ndio mzee sana na wanapenda sana warembo mimi ni mzaliwa wa huko na nimekulia hukohuko
 
HABARI

Na Godfrey Kahango, Mbarali. (email the author)

....
wataalamu iliketi na kutafakari kwa kina namna ya kuugawa mkoa huo kwa kuzingatia maagizo ya mkuu wa mkoa.

Diwani Mwakibete, alisema madiwani wa halmashauri hyo wamependekeza jina la mkoa mpya liwe Rungwe ukiwa na Wilaya za Kyela, Rungwe,Ileje na Mbozi na makao makuu ya yawe Tukuyu.

Alisema pia wametaka jina la mkoa wa zamani libaki kuwa Mbeya ukiwa na Wilaya za Momba, Chunya, Mbeya na Mbarali na Makao makuu yakiwa Mbeya.

Alisema kamati hiyo haikuona haja yaa kuanzisha wilaya mpya kutokana na sababu za kijiografia.

Hao madiwani watakuwa walivuta bange kwenye full councel yao.
Yaani mtu atoke Vwawa aende Tukuyu kufuata Huduma za Serikali ya Mkoa? Sio uchizi huo?

Na huyo Kandoro wenu na Kikwete wana haraka gani na hilo? Gaweni mkoa wa Pwani kwa kuanzia.
Wilaya ya Rufiji iunganishwe na Bagamoyo na Makao makuu yawe Ikwiriri. So stupid! Anzeni ha hilo....
 
Fikra mfu za viongozi wa ccm hizo, mbona nchi nyingine wana mikoa mikubwa zaidi ya hii wanayotaka kuigawa na maendeleo yapo tena ya kutosha. Hapa nakuwa na wasi wasi na uwezo wa rais na washauri wake
 
Hayo magamba yanataka kutugawa wanaMbeya.Kamwe ss hatutakubali upuuzi wa ccm.Njia pekee ya kusogeza huduma kwa wananchi ni kuanzisha sera ya majimbo.Vinginevyo magamba hapa mmegonga mwamba.Na nyie madiwani mnaotumika vibaya,jiandaeni kung'oka 2015
 
Katiba yetu mpya tunayoindika ni lazima itamke wazi kuwa nchi yetu itakuwa na wilaya na mikoa [ FIXED] mingapi otherwise nchi yetu itagawiwa vipande vpande kutokana na utashi na uroho wa madaraka wa wanansiasa at the detriment of the people's development.Haiwezekani kila kiongozi anataka sehemu anayotoka iwe mkoa kwani ni mzigo kwa walipa kodi masikini wa nchi hii; kwa kasi tunayokwenda sintashangaa kabla ya kutoka madarakani kusikia kuwa Kikwete nae anataka Msoga nako kuwe na mkoa wake , kwani inaelekea kuna ushindani wa kutengeneza wilaya na mikoa mipya kati ya wanasiasa!!!
 
Dah hii kali, ko wilaya ya BUSOKELO itakuwa katika mkoa upi katika hayo mapendekezo yao.walikula kitu cha MWAKALELI hao.
 
sasa wameshinda kufanya kazi wanadani dawa ni kugawa mikoa tu, huo ndi uroho wa madaraka, sioni haja ya kuugawa mkoa wa mbeya ni kongeza gharama tu
 
Hao madiwani watakuwa walivuta bange kwenye full councel yao.
Yaani mtu atoke Vwawa aende Tukuyu kufuata Huduma za Serikali ya Mkoa? Sio uchizi huo?

Na huyo Kandoro wenu na Kikwete wana haraka gani na hilo? Gaweni mkoa wa Pwani kwa kuanzia.
Wilaya ya Rufiji iunganishwe na Bagamoyo na Makao makuu yawe Ikwiriri. So stupid! Anzeni ha hilo....

Kha, umenifurahisha sana, hawa jamaaa vikao wanakaa Dar es salaam kugawa mikoa ya watu, maana sasa wanaongeza mamatatizo tupu...........
 
Hao madiwani watakuwa walivuta bange kwenye full councel yao.
Yaani mtu atoke Vwawa aende Tukuyu kufuata Huduma za Serikali ya Mkoa? Sio uchizi huo?

Na huyo Kandoro wenu na Kikwete wana haraka gani na hilo? Gaweni mkoa wa Pwani kwa kuanzia.
Wilaya ya Rufiji iunganishwe na Bagamoyo na Makao makuu yawe Ikwiriri. So stupid! Anzeni ha hilo....

Kha, umenifurahisha sana, hawa jamaaa vikao wanakaa Dar es salaam kugawa mikoa ya watu, maana sasa wanaongeza mamatatizo tupu...........
 
Hakuna kuwa na mkoa kama Pwani ndani ya Dar. Hakuna kiungo cha Rungwe na Mbozi kupitia Ileje lazma utokee Mbeya. Labda makao makuu yawe katka Wilaya ya Ileje na kuchukua baadhi kata za Mbeya Vijijini

Mkuu umesahau yale ya mgawanyo wa Arusha? Mtu anatoka mererani kwenda babati (mkoani) lazima apitie Arusha akitaka kufika haraka. Viongozi hawajifunzi kutokana na historia, badala ya kusogeza huduma kwa wananchi inakuwa kuwakomesha wananchi.

Dhana nzima ya kuigawa mikoa mimi naona kama ni kuwagawa watanzania kwa makabila yao na kutengenezeana ulaji zaidi. Tunahatarisha umoja wetu na hakuna tofauti na lile lingine la udini, waasisi wakiwa wale wale.
 
Hao madiwani watakuwa walivuta bange kwenye full councel yao.
Yaani mtu atoke Vwawa aende Tukuyu kufuata Huduma za Serikali ya Mkoa? Sio uchizi huo?

Na huyo Kandoro wenu na Kikwete wana haraka gani na hilo? Gaweni mkoa wa Pwani kwa kuanzia.
Wilaya ya Rufiji iunganishwe na Bagamoyo na Makao makuu yawe Ikwiriri. So stupid! Anzeni ha hilo....

mkuu wakati mwingine me natamani nisiwe mtanzania tena! Yani bila matumaini 2015 ningezamia hata Zambia hawana upuuzi aina hii!
 
Huu ni upuuzi uliopitiliza kuamini kuwa kuongeza idadi ya mikoa kwa kuigawanya iliyopo ndio suluhu ya matatizo tuliyonayo.
Ni wazi kuwa nchi hii tumeamua kwa makusudi kabisa kuwaacha wapuuzi wachache kutuburuza na kutuletea mikakati mfu, huku tukiendelea kuwapigia makofi.
Hivi hawajui kuwa kuzidi kuongeza mikoa ni kuzidi kuongeza mzigo kwa nchi yetu?
Kama tunaamini kwenye kama ndio njia sahihi ya kusogeza na kurahisisha upatikanaji wa maendeleo kwa wananchi na taifa, KWANINI SASA TUNAHANGAIKA KUZIUNGANISHA NCHI ZETU ZA EAST AFRICA? Kwanini tunahubiri tofauti na tunachotenda nchini mwetu?

Hii ndugu zangu ni ishara ya kuishiwa na mbinu, mikakati, na uunifu wa kutatua matatizo yetu...VIONGOZI TULIONAO WAMESHINDWA KABISA, HAWATUFAI!
 
Back
Top Bottom