Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

Hakuna kuwa na mkoa kama Pwani ndani ya Dar. Hakuna kiungo cha Rungwe na Mbozi kupitia Ileje lazma utokee Mbeya. Labda makao makuu yawe katka Wilaya ya Ileje na kuchukua baadhi kata za Mbeya Vijijini

huuu ni ujinga ambao ccm wanaufikiria. aafu kwenda huko momba ni lazima upite mbozi, pumbavu sana. si wangependekeza uyole iunganishwe na isyonji, igoma iwe wilaya moja? aafu waongeze na kyela, mbarali, tukuyu na ileje?
 
NDOMYANA ngoja nimtafute m/kiti wa hiyo halmashauri anipe tofauti zake ili nizijue.
 
huuu ni ujinga ambao ccm wanaufikiria. aafu kwenda huko momba ni lazima upite mbozi, pumbavu sana. si wangependekeza uyole iunganishwe na isyonji, igoma iwe wilaya moja? aafu waongeze na kyela, mbarali, tukuyu na ileje?

Yes! Nadhani ni kitu ambacho kinaweza fanya kazi pia. Pia wangekuwa na akili ya kutosha wakati wa kuunda Mkoa wa Njombe, wangechukuwa baadhi ya maeneo ya Mbarali ili kupunguza ukubwa wa Mkoa wa Mbeya.

Tutaendelea kukurupuka mpaka lini?
 
Mkuu Mbugi ee, unajua ukisema hivyo ni kama unakubaliana na dhana ya kuongeza mkoa. Wazo zima ni upuuzi wa kuongeza gharama za uendeshaji wa serikali. Halina maana kabisa.

Hapa kinachotafutwa ni upuuzi wa kuongeza bajeti kwa ajira mpya ya Mkuu wa Mkoa mpya, mashangingi mengine FFU kulinda mkuu wa mkoa mpya na gharama nyingine lukuki ambazo zinahusiana na uendeshaji wa serikali ya Mkoa. Wazo hilo ni economically unreasonable kabisa. Mi hata naliona kama jitihada ya kuwagawa watu wa Mbeya.

Kwa hoja ya kuongeza gharama ya uendeshaji nakubaliana na wewe 100%. na sina hakika kama kuna tafiti yoyote iliyofanywa kuonyesha ni kwa kiasi gani huduma zimekuwa hafifu kwa sababu ya ukuwa wa kijiografia na si ' Zero commitment & abuse of power by those in position of trust' kitu ambacho kinahitajika ni kuja na some control measure kwa watu hawa ambayo nadhani ni pamoja na viongozi wa mikoa na wilaya kuwajibishwa na wananchi
 
jeunafaham mpaka wa tanzania na zambia uma wagawa wanyamwanga ktk nchi mbili wapo zambia na tanzania pili siungi mkono
 
Hakuna kuwa na mkoa kama Pwani ndani ya Dar. Hakuna kiungo cha Rungwe na Mbozi kupitia Ileje lazma utokee Mbeya. Labda makao makuu yawe katka Wilaya ya Ileje na kuchukua baadhi kata za Mbeya Vijijini

Mkuu Gaza, wazo zima la kuigawa Mbeya ni wazo mfu. Ni wazo ambalo klinaweza kutolewa tu na watu wasio makini. Tatizo la kupinga Mbozi kuwa na Rungwe wala hata si ukosefu wa njia. Ni umbali uliopo. Kuna kinjia kinaanzia Kiwira Mjini, pale Rungwe; kinapita kijiji nadhani kinaitwa Swaya kule juu ya Igogwe, unapanda nacho weee....kule mbele unaweza ukachagua kufika Santilya (mbeya vijijini) au hata kuelekea Ilembo ukitaka. Unakuwa umekwepa jiji la Mbeya kabisa kwa upande wa kusini mwa jiji. Upo upenyo wa kushuka Mbalizi sasa unapokuwa maeneo ya Santilya. Lakini pia unaweza ukanyoosha nacho hadi maeneo (kwa Kalondo) na Idunda Mbozi Mashariki. Kutoka Idunda sasa ndo unaanza safari nyingine kuelekea Makao Makuu ya Mbozi. Utapitia Iyula mjini, utaelekea Kijiji cha Ihowa, Ichesa na kuunga Mlowo utapokutana na Lami uliyoiacha Kiwira!!!! Taabu yote hiyo ya nini?

Hivi huduma zinazotakiwa kusogezwa kwa Wananchi ni lazima ziwe ofisi za Mkuu wa Mkoa? Au kusogeza mtawanyo wa huduma za Idara za Elimu, Afya, na Ulinzi? Ee Mungu tusaidie tuondoe hawa watu madarakani kwa amani! I don't like CCM any more... Not one single bit!
 
Mkuu mi sio mtaalamu sana ila katika kufuatilia nliambiwa busokelo sio wilaya ila walichokifanya ni kuigawa tukuyu kua halmashauti mbili ambayo kati ya hizo busokelo nu halmashauri inayojitegemea na rungwe nayo ni halmashauri,. Ila uneza uliza zaidi ukaelekezwa na wataalam

ni kama ilivyo wilaya ya Mbeya Mjini na halmashauri ya Mbeya vijijini. yaani Rungwe ndio yenye office za mkuu wa wilya na DC mwenyewe, lakini Busokelo pale panakuwa na Baraza la madiwani tu (halmashauri bila mkuu wa wilaya). mfano Mbeya mjini na Mbeya vijijini ziko chini ya mkuu wa wilaya mmoja tu Dr Norman Siggala.
 
sawa mkuu nafkiri ukipata jibu utakuja nielekeza zaidi na mie

jibu hili hapa:
ni kama ilivyo wilaya ya Mbeya Mjini na halmashauri ya Mbeya vijijini. yaani Rungwe ndio yenye office za mkuu wa wilya na DC mwenyewe, lakini Busokelo pale panakuwa na Baraza la madiwani tu (halmashauri bila mkuu wa wilaya). mfano Mbeya mjini na Mbeya vijijini ziko chini ya mkuu wa wilaya mmoja tu Dr Norman Siggala.
 
Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya limetoa mapendekezo yake ya Kuugawanya Mkoa wa Mbeya kama ifuatavyo:

A:MKOA WA MBEYA

1.Mbeya Mjini
2.Mbeya Vijijini
3.Mbozi
4.Momba
5.Chunya
6.Mbalali

B.MKOA WA KIWIRA

1.Rungwe
2.Kyela
3.Ileje
4.Busokelo
*Baadhi ya Kata za Mbeya Vijijini zitaenda Mkoa wa Kiwila.

-Pia Halmashauri ya Jiji la Mbeya imeomba kuongezewa Kata za Mbeya Vijijini.

i.Ihango
ii.Utengule
iii.Nsalala
iv.Itewe
v.Ijombe

-Pia Wilaya ya Mbeya Vijijini izae Wilaya ya Tembela.

*HAYA NI MAPENDEKEZO TU YANAYOPELEKWA NGAZI YA JUU YA VIKAO VYA DCC NA RCC.
 
Hii inafanya Huduma za Kijamii kusogezwa karibu.
Tena Mkoa huu wa Mbeya Wilaya zake zote zimejitosheleza sio kama kwetu huku Simiyu!
 
Mh.Mwakyembe nae kupata mkoa!kila waziri sasa atataka mkoa na hii ilianzishwa kwa ubinafsi wa Sumaye kuanzisha manyara
 
Ndugu Watanzania na wazalendo.
Mnamo tarehe 1/5/2015 katika sherehe za Mei Mosi Rais Kikwete alitangaza kuruhusu kugawa Mkowa wa Mbeya. King'anganyiro hiki kimeanza hukuwa Wanyakyusa wakidai Mkoa mpya uitwe Rungwe na Makao Makuu yawe Tukuyu.
Huku Wana Mbozi wakidai Mkoa Mpya uitwe Songwe na Makao yake makuu yawe Mbozi (Vwawa).

mi nadhani wakati umefika sasa kwa wana mbeya kuangalia sababu za msingi na kuancha ukabila na ubwanyenye wa kiu chumi uliojaa ukiritimba.
Moja wapo ya sababu ni hizi:
1. Kusogeza huduma kwa wananchi
2. Uchumi wa eneo husika
3.Jiografia ya Maeneo yanayotarajiwa kuunda mkoa mpya
4. Asili na kasumba ya watu wa maenwotweo tarajali

Na sababu nyingine kedekede ambazo nazitaraji kutoka kwenu wadau mnaoufahamu mko wa mbeya.
Karibuni wote
 
Hoja ya kuugawa mkoa wa Mbeya ni mufilisi na ambayo haina tija!! Kuwa na mikoa mingi siyo maendeleo! Isitoshe rasimu ya katiba mpya imependekeza majimbo 25 tu!!
 
WAZO LA KUUGAWA MKOA WA MBEYA NI LA MSINGI NI MKOA MKUBWA SANA.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa wa Mbeya ubaki kuwa na makao makuu mbeya mjini kama ilivyokuwa zamani ukiwa na wilaya za Mbalali, Momba, Chunya na mbeya mjini. Mbeya mjini imekaa katikati ya wilaya hizo kwa kufikaki kirahi ikiwemo miundombinu yake iko tayari kupokea mabadiliko na huduma mpya za mkoa mpya.

Halikadhalika, RUNGWE ina sifa hizo hizo ikiwemo mlima maarufu wa Rungwe ambapo utatangazwa kitaifa na kimataifa. Aidha, Rungwe ndio Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji katika mkoa wa mbeya hasa kwa mazao ya kilimo. Rungwe ni moja ya majina ya kale ya mkoa wa mbeya tangu enzi la ukoloni kutokana na jina hilo kuakisi mlima Rungwe. Tangu enzi la mkoloni Tukuyu kwa jina hilohilo ndio ilikuwa makao makuu ya Rungwe enzi hizo na ndio sababu Tukuyu ikapata maendeleo haraka baada ya mbeya mjini.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe Tukuyu. Mkoa wa Rungwe uwe na wilaya za Rungwe, Kyela, Ireje na Mbozi

Mkoa wa mbeya ndio mkoa mkubwa kuliko yote nchini kwa sasa ndio maana hata Iringa umegawanya na Arusha. kwa wale wanaoifahamu mikoa hiyo naamini wataniunga mkono tofauti na ambao hawajui vizuri jiografia ya mbeya na mikoa mingine ilivyogawanywa.
 
Hofu yangu ni moja tu, mkoa ambao utaitwa Rungwe na wilaya zake 4 (Kyela, Mbozi, Ileje na Rungwe) ndio eneo la kitegauchumi cha mkoa wa Mbeya kwa sasa hali ambayo itauacha mkoa wa mbeya mpya utafute njia zaidi za kiuchumi ili kubaki juu katika uzalishaji nchini.
 
Back
Top Bottom