MADIWANI wa Halmashauriya Wilaya Kyela mkoani Mbeya, wamepitisha azimio la kuugawa Mkoa wa Mbeya nakupendekeza mkoa mpya uitwe Rungwe ambao makao makuu yake yatakuwa Tukuyu.Akiwasilisha pendekezo hilo, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya WilayaKyela, Joseph Njau alisema kufuatia agizo la Rais la kuugawa mkoa ili kuwa namikoa miwili, Kamati ya Fedha Uongozi na Mipango katika kikao chakekilichofanyika Juni 7, mwaka huu ilikubaliana na suala hilo.
Alisema katika kikao hicho, kamati hiyo ilijaribu kupitia mapendekezoyaliyotolewa na kamati ya wataalamu ambayo ilizingatia vigezo kadhaa kama vilejiografia ya eneo lenyewe, historia ya wilaya husika, shughuli za kiuchumizilizopo.
Mapendekezo yaliyofikiwa katika baraza hilo, ni kuwa mkoa mpya uitwe Rungwe namakao yake makuu yawe katika mji wa Tukuyu na kuwa mkoa huo mpya utaundwa naWilaya za Kyela, Rungwe na halmashauri ya Busokelo na Ileje sambamba nakuifanya halmashauri ya Busokelo kuwa wilaya kamili, alisema.
Alisema Mkoa Mbeya, utabaki kuwa na Halmashauri ya Jiji, Halmashauri ya WilayaMbeya, Mbozi, Momba, Mbarali na Wilaya Chunya kwa sababu wilaya hizo zinauhusiano wa kijiografia tofauti na hizi za kusini.
Kwa upande wake, Diwani Kata ya Ngonga, Kileo Kabomonga alisema Mkoa wa Mbeyandio uliokuwa umebakia kuwa na ukubwa kati ya mikoa yote nchini.
Katika kikao hicho, madiwani asilimia 99 walikubali kuwa mkoa uwe Rungwa nabaadhi yao walitaka mkoa uitwe Rungwe, jambo ambalo waliliafiki.
Source: Gazeti la Nipashe 10 Juni 2013
My Take: Hivi kwa nini hawasubiri tuandike Katiba ya Tanganyika? Mfumo huu wa utawala unaweza kubadilika. Haraka yao ni ya nini au ndiyo yale kuwa wao walitakalo ndio linakuwa?