Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

watu8 hizo taarifa ni za uongo. kwanza zanzibar sio mkoa ni nchi. pili kwa idadi ya watu :
1. dar
2.mwanza
3.mbeya
4.arusha
5.tanga etc
unatumia takwimu za mwaka gani kaka
 
CCM walijua katiba mpya itataka majimbo ya ubunge wa jamuhuri ya muungano yawe mikoa. Hivyo kila kwenye upinzani wanapagawa wapate jimbo ambalo walau watapata kura!
 
WAZO LA KUUGAWA MKOA WA MBEYA NI LA MSINGI NI MKOA MKUBWA SANA.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa wa Mbeya ubaki kuwa na makao makuu mbeya mjini kama ilivyokuwa zamani ukiwa na wilaya za Mbalali, Momba, Chunya na mbeya mjini. Mbeya mjini imekaa katikati ya wilaya hizo kwa kufikaki kirahi ikiwemo miundombinu yake iko tayari kupokea mabadiliko na huduma mpya za mkoa mpya.

Halikadhalika, RUNGWE ina sifa hizo hizo ikiwemo mlima maarufu wa Rungwe ambapo utatangazwa kitaifa na kimataifa. Aidha, Rungwe ndio Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji katika mkoa wa mbeya hasa kwa mazao ya kilimo. Rungwe ni moja ya majina ya kale ya mkoa wa mbeya tangu enzi la ukoloni kutokana na jina hilo kuakisi mlima Rungwe. Tangu enzi la mkoloni Tukuyu kwa jina hilohilo ndio ilikuwa makao makuu ya Rungwe enzi hizo na ndio sababu Tukuyu ikapata maendeleo haraka baada ya mbeya mjini.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe Tukuyu. Mkoa wa Rungwe uwe na wilaya za Rungwe, Kyela, Ireje na Mbozi

Mkoa wa mbeya ndio mkoa mkubwa kuliko yote nchini kwa sasa ndio maana hata Iringa umegawanya na Arusha. kwa wale wanaoifahamu mikoa hiyo naamini wataniunga mkono tofauti na ambao hawajui vizuri jiografia ya mbeya na mikoa mingine ilivyogawanywa.

Hebu dadavua kidogo mgawanyo wa namna hiyo utamletea unafuu vipi mwananchi wa mbeya kama siyo kumubebesha mzigo mkubwa badala ya kumletea unafuu.kwa mfano mkaazi wa wilaya ya Momba kumuacha mkoa wa mbeya ni kumletea unafuu vipi kwa hali iliyopo sasahivi bila hata mkoa kugawanywa mwananchi wa Momba anapohitaji huduma za kimkoa analazimika kupita wilaya ya Mbozi ndipo afike mkoani Mbeya.mkoa utakapogawanywa mkazi wa Momba atalazimika kupita mkoa wa Rungwe wilaya ya Mbozi ndipo afike mkoani kwake.Je huku ndiyo kumpunguzia matatizo au kumuongezea matatizo?.Pia na kwa mwananchi wa Mbozi kabla ya mkoa haujagawanywa kwake yeye kufika mkoani ni rahisi sana kwa sababu wila ya Mbozi inapakana kwa karibu sana na mkoa wa Mbeya kuliko Rungwe.kwa maana hiyo Mbozi ikipelekwa Rungwe ni sawa na kumuongezea mzigo mkubwa mwananchi wa Mbozi atakapohitaji huduma za kimkoa.Atakapolazimika kupata huduma hizo atalazimika kupita mkoa wa Mbeya ndipo aende mkoani kwake Rungwe.Kwa mgao huu nafuu mkoa ukabaki kama hapo awali kuliko hivi sasa ambapo mwananchi anataka kubebeshwa mzigo juu ya mzigo.Halafu hivi Mbeya hakuna majina mengi mpaka muite majina ya milima tu au mna siri gani na milima?.Mbeya ni mlima na wilaya.Rungwe ni mlima na ni wilaya pia. na sasa munataka kuita mkoa Rungwe.
 
Huyu jamaa anagawa mikoa kama njugu.....haya si maendeleo...sikubali hoja ya kugawa mikoa...ni bora kuwa na majimbo kuliko kugawa mikoa
 
Niwape maoni ya mikakati bora ya kusukuma na kuinua maendeleo.
Kama Lengo ni kujenga uchumi miongoni mwa wanajamii lazima tuwe na structures ambazo zitatuwezesha kupata mafanikio tunayoyahitaji. Kuunda mikoa mipya ni kuzidi kutumia rasilimali adimu kwa kujenga mifumo ya utawala inayogharimu fedha nyingi. Hili ni sawa na mtazamo hasi na bapa wa aliyeunda serikali yenye baraza la mawaziri zaidi ya hamsini akidhani ndio jawabu la kupeleka huduma kw wananachi kumbe anaunda ajira za kifahari kwa watu wachache kwa kutumia rasilimali za taifa.
Vyombo mahsusi vya kutumia ni local government structures. Kama vyombo hivi vitaimarishwa na kuwezeshwa kwa dhati (jambo ambalo wengi wenye ufinyu wa utambuzi wanaona ati si sahihi) jawabu la huduma bora na utumishi wenye tija tutaliona. Imagine kuwa na Madaktari lukuki pale wizarani wakati huduma za tiba tunazihitiji wilayani au Mabwana Shamba pale makao makuu Kilimo, Maafisa Ushirika, Maafisa Elimu na kadhalika.
Amkeni - tuzisaidie local authorities tutapata maendeleo tunayoyahitaji
!
 
Kuna watu wanatafutiwa ajira hapo.Badala ya kuanzisha viwanda vingi ili kupanua ajira sisi tunakazana kuzalisha mikoa na wilaya kwa nia ya kuongeza ajira.

great thinker!!!!!!!!!!!?
 
Hapa nahisi ulinogewa...
Kimsingi pamoja na kugawanywa kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Arusha, Rukwa bado mkoa wa Mbeya sio wa kwanza kwa ukubwa hapa Tanzania.
Ukubwa wa mikoa kulingana na maeneo yake upo kama ifuatavyo:
1. Tabora
2. Morogoro
3. Lindi
4. Ruvuma
5. Mbeya

na kuendelea...

Ukubwa wa mikoa kutokana na idadi ya watu:
1. Dar es Salaam
2. Mwanza
3. Zanzibar
4. Arusha
5. Mbeya

Tupe vipimo kwa sq kms Mbeya ni 63,420 sq. kms. inalipa zaidi kuliko maneno matupu.

sikuzungumzia ukubwa kwa kiwango cha ujazo wa watu hicho ni kingine lakini bado naamni mbeya ni mkoa wenye watu wa kutosha kuugawa
 
mbona arusha, shinnyanga, rukwa , isringa zimegawanywa hakuna tatizo. kugawanya mbeya ni tatizo? mwacheni rais agawanye mkoa kulingana na utawala wake. huu ni utaratibu wa kawaida kwani hata rukwa ilitoka mkoa wa mbeya. wanaopinga wana lao jambo. mbona wilaya zimeendelea kugawanywa hampingi? wilaya ya rungwe itakuwa na wilaya za tukuyu, busokelo, kyela, na ileje. mbeya itabaki na mbalali, momba,mbozi, mbeya jiji, mbeya vijijini na chunya.

wilaya ya rungwe au mkoa wa rungwe?
 
Vipi Mkoa wa Tabora na Mkoa wa Mbeya kwa eneo ni mkoa upi una eneo kubwa? Waliosoma jiografia tumieni uzi kupata surface area ya mkoa huo.
 
Tupe vipimo kwa sq kms Mbeya ni 63,420 sq. kms. inalipa zaidi kuliko maneno matupu.

sikuzungumzia ukubwa kwa kiwango cha ujazo wa watu hicho ni kingine lakini bado naamni mbeya ni mkoa wenye watu wa kutosha kuugawa

Mkuu hata ukiangalia kwa macho tu kwenye ramani mpya ya Tanzania hata ile ya zamani, bado utagundua kwa haraka namna Tabora na Lindi zilivyo kubwa kuizidi Mbeya.

Kwa kuwa hukuwa specific kwenye maelezo yako ya ukubwa ndio maana nilikuonesha kwa namna mbili tofauti zitumikazo kuelezea ukubwa wa mji...

Ila kwa kuwa unahitaji kielelezo basi angalia hapa...une nga mundu ghwa inongwa sya bhwilabhwila!!!

List of Tanzanian regions by area - Wikipedia, the free encyclopedia
 
[QUOTE Ukubwa wa mikoa kutokana na idadi ya watu:
1. Dar es Salaam
2. Mwanza
3. Zanzibar
4. Arusha
5. Mbeya[/QUOTE]

In the 2012 Census, Dar es Salaam was found to have a
population of 4.36 million accounting for 10 percent of the total Tanzania
Mainland population. Regions with a population of over 2 million were
Mwanza (2.77 million), Mbeya (2.71 million), Kagera (2.46 million), Tabora
(2.29 million), Morogoro (2.22 million), Kigoma (2.13 million), Dodoma
(2.08 million) and Tanga (2.05 million).
Kwa idadi ya watu DSM Mwanza na Mbeya ziko kwa top 3
 
The area of Tabora is 76,151 km² (approximately 9% of Tanzania). A total of 34,698 km² (46%) is forest reserve, and 17,122 km² (22%) is game reserve.
Ila Tabora mapori ni mengi maana robo tatu ya mkoa ni forest reserve na game reserve
 
Hoja ya kuugawa mkoa wa Mbeya ni mufilisi na ambayo haina tija!! Kuwa na mikoa mingi siyo maendeleo! Isitoshe rasimu ya katiba mpya imependekeza majimbo 25 tu!!

Rasimu inasema kila mkoa utakuwa jimbo la uchaguzi. Maana yake minkoa ikiongezeka majombo pia!
 
[font=&amp]taarifa zifuatazo zitatusaidia kulichambua hili

southern highlands province then in 1963, the southern highlands province was split into two regions ie mbeya and iringa.[/font]

[font=&amp]1974 sumbawanga district was separated from mbeya and accorded full regional status. Bila kuwa na iyo migawanyo kwa sasa tusingekuwa na mkoa wa mbeya wala rukwa wala iringa maana yote iliitwa southern higland province[/font]


[font=&amp]mbeya regional area covers 63,420 sq.kms. Which is 6.4% of the [/font]

[font=&amp]total area of the united republic of tanzania. [/font]

rwanda: Total: 26,338 sq km & burundi total: 27,830 sq km kwa ujumla wao hawaufikii mkoa wa mbeya kila inchi apoinaingia mbeya kama mara 3
the idea to delineate mbeya into two regions is not a new concepts. It started a long time ago. Essentially the idea was to compose the rungwe region whose hq would be tukuyu town. This idea has not died. Some men want to leave legacy against this achievement. So i dont think those who oppose it will be successful, at any rate you are too late. Infact the president whose motive is delineation of administrative into small portion with a relative advantage of favors from the electorate. I hope his next move would be to divide morogoro region into north and southern region. Trust me this is what is going to happen before he steps down
 
Hoja ya kuugawa mkoa wa Mbeya ni mufilisi na ambayo haina tija!! Kuwa na mikoa mingi siyo maendeleo! Isitoshe rasimu ya katiba mpya imependekeza majimbo 25 tu!!

Pole sana ndugu yangu, Ishu ni U - DC, RC, RPC, RCO, n.k Kwani wajomba wamekuwa wengi kuliko idadi iliyopo. Kulilia uongozi pabaya usiombe, Wilayani niliko kuna Kata imegawanywa kutoka vijiji 3 hadi sita. Kila kijiji kina chini ya kaya 300 na eneo la kijiji upana haufiki hata 500m huku urefu ukiwa chini ya 1km. Kisa hiyo kata Imeshikwa na CUF, wanajaribu kugawa wapate walau kijiji kimoja.
 
the idea to delineate mbeya into two regions is not a new concepts. It started a long time ago. Essentially the idea was to compose the rungwe region whose hq would be tukuyu town. This idea has not died. Some men want to leave legacy against this achievement. So i dont think those who oppose it will be successful, at any rate you are too late. Infact the president whose motive is delineation of administrative into small portion with a relative advantage of favors from the electorate. I hope his next move would be to divide morogoro region into north and southern region. Trust me this is what is going to happen before he steps down

...duuuhh!...aisee!
 
Ndugu Watanzania na wazalendo.
Mnamo tarehe 1/5/2015 katika sherehe za Mei Mosi Rais Kikwete alitangaza kuruhusu kugawa Mkowa wa Mbeya. King'anganyiro hiki kimeanza hukuwa Wanyakyusa wakidai Mkoa mpya uitwe Rungwe na Makao Makuu yawe Tukuyu.
Huku Wana Mbozi wakidai Mkoa Mpya uitwe Songwe na Makao yake makuu yawe Mbozi (Vwawa).

mi nadhani wakati umefika sasa kwa wana mbeya kuangalia sababu za msingi na kuancha ukabila na ubwanyenye wa kiu chumi uliojaa ukiritimba.
Moja wapo ya sababu ni hizi:
1. Kusogeza huduma kwa wananchi
2. Uchumi wa eneo husika
3.Jiografia ya Maeneo yanayotarajiwa kuunda mkoa mpya
4. Asili na kasumba ya watu wa maenwotweo tarajali

Na sababu nyingine kedekede ambazo nazitaraji kutoka kwenu wadau mnaoufahamu mko wa mbeya.
Karibuni wote
Una uhakika na hiyo tarehe mkuu au Ndio unaamka!!!!!
 
Back
Top Bottom