Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

Madiwani wapendekeza kuigawa Mbeya

Ni upuuzi kugawa gawa ovyo hii nchi, kwani ukubwa ni nini pelekeni maendeleo...
Kikwete amekata kata ovyo hii nchi! Wala hakuna maendeleo yoyote
 
ndugu watanzania na wazalendo.
Mnamo tarehe 1/5/2015 katika sherehe za mei mosi rais kikwete alitangaza kuruhusu kugawa mkowa wa mbeya. King'anganyiro hiki kimeanza hukuwa wanyakyusa wakidai mkoa mpya uitwe rungwe na makao makuu yawe tukuyu.
Huku wana mbozi wakidai mkoa mpya uitwe songwe na makao yake makuu yawe mbozi (vwawa).

Mi nadhani wakati umefika sasa kwa wana mbeya kuangalia sababu za msingi na kuancha ukabila na ubwanyenye wa kiu chumi uliojaa ukiritimba.
Moja wapo ya sababu ni hizi:
1. kusogeza huduma kwa wananchi
2. Uchumi wa eneo husika
3.jiografia ya maeneo yanayotarajiwa kuunda mkoa mpya
4. Asili na kasumba ya watu wa maenwotweo tarajali

na sababu nyingine kedekede ambazo nazitaraji kutoka kwenu wadau mnaoufahamu mko wa mbeya.
Karibuni wote

tafadhali fanya masahahisho mkuu
 
Kugawa nchi hovyo hovyo sii vema!

Tunaharakisha nini kwa nini tusisubiri Katiba Mpya?

Basi hata mikoa ya Morogoro, Lindi, Ruvuma na Pwani ni mikubwa nayo igawanywe!
 
Hofu yangu ni moja tu, mkoa ambao utaitwa Rungwe na wilaya zake 4 ndio eneo la kitegauchumi cha mkoa wa Mbeya kwa sasa hali ambayo itauacha mkoa wa mbeya mpya utafute njia zaidi za kiuchumi ili kubaki juu katika uzalishaji nchini.
Hoja yako ni dhaifu kama jina lako! Nani kakudanganya kuwa wilaya za mkoa wa Mbeya zinaitegemea Rungwe kiuchumi! Kuendelea kugawa mikoa ni kuongeza gharama za utawala badala ya maendeleo na hivyo kuwa mzigo kwa walipa kodi!
 
Mbona kichwa cha habari na maudhui ni tofauti,

acheni mkoa wa mbeya ubaki kama ulivyo.

sio mnagawa mikoa kisiasasiasa.
 
WAZO LA KUUGAWA MKOA WA MBEYA NI LA MSINGI NI MKOA MKUBWA SANA.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa wa Mbeya ubaki kuwa na makao makuu mbeya mjini kama ilivyokuwa zamani ukiwa na wilaya za Mbozi, Zomba, Chunya na mbeya mjini. Mbeya mjini imekaa katikati ya wilaya hizo kwa kufikaki kirahi ikiwemo miundombinu yake iko tayari kupokea mabadiliko na huduma mpya za mkoa mpya.

Halikadhalika, RUNGWE ina sifa hizo hizo ikiwemo mlima maarufu wa Rungwe ambapo utatangazwa kitaifa na kimataifa. Aidha, Rungwe ndio Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji katika mkoa wa mbeya hasa kwa mazao ya kilimo. Rungwe ni moja ya majina ya kale ya mkoa wa mbeya tangu enzi la ukoloni kutokana na jina hilo kuakisi mlima Rungwe. Tangu enzi la mkoloni Tukuyu kwa jina hilohilo ndio ilikuwa makao makuu ya Rungwe enzi hizo na ndio sababu Tukuyu ikapata maendeleo haraka baada ya mbeya mjini.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe Tukuyu. Mkoa wa Rungwe uwe na wilaya za Rungwe, Kyela, Ireje na

Mkoa wa mbeya ndio mkoa mkubwa kuliko yote nchini kwa sasa ndio maana hata Iringa umegawanya na Arusha. kwa wale wanaoifahamu mikoa hiyo naamini wataniunga mkono tofauti na ambao hawajui vizuri jiografia ya mbeya na mikoa mingine ilivyogawanywa.
Mkuu naungana na wewe kwa ulichosema.
 
Ni upuuzi kufikiri kugawa mikoa ni maendeleo. Uhalisia ni kuongeza gharama.
 
Hoja yako ni dhaifu kama jina lako! Nani kakudanganya kuwa wilaya za mkoa wa Mbeya zinaitegemea Rungwe kiuchumi! Kuendelea kugawa mikoa ni kuongeza gharama za utawala badala ya maendeleo na hivyo kuwa mzigo kwa walipa kodi!

Hujaelewa ndugu,

nasema wilaya ya Rungwe, Kyela, Mbozi na Ileje ndizo zinapendekezwa kuunda mkoa wa Rungwe na ndizo zinabeba uchumi mkubwa wa mbeya kwa asilimia kuliko mkoa unaopendekezwa kuwa wa mbeya ukiwa na wilaya za Momba, Chunya, Mbalali na Mbeya mjini.
 
Nionavyo mimi ni upuuzi mtupu kugawanya mikoa na ni kuchochea ukabila.Najua serikali ya CCM inafanya hayo ili kuzima sera ya CHADEMA kuhusu utawala la majimbo ambao kimsingi unawaunganisha wananchi badala ya kuwatenganisha.Mfano, nyanda Iringa ilipogawanywa ikatenganisha wahehe na wabena. Sasa wanataka kuwatenganisha wanyakyusa na makabila mengine.Wananchi wanataka huduma siyo utawala mfano, kama barabara ya Katumba-mwakaleli-Lufilyo-Rwangwa-Ipinda ingekuwa katika kiwango cha lami ingerahisisha kila kitu na kuinua uchumi wa wananchi wa Rungwe kwa kuwa ingerahisisha usafiri na mawasiliano.Mathalani Rungwe kuna gesi na makaa ya mawe, bila kusahau uzalishaji mkubwa wa chai,ndizi,mahindi,viazi mviringo n.k Je, unahitaji kugawa mkoa ili kuwaletea maendeleo na huduma za kijamii kama umeme,maji,barabara,masoko,hospitali,vyuo vya ufundi stadi na viwanda vidogo vidogo? I'm not yet convinced!
 
..Mungu wetu Mwema akunyime kila Kitu lakini akupe BUSARA!
Katika hiyo mikoa ambayo imeishagawanywa, ni ipi ambayo imeonyesha mafanikio na maendeleo makubwa sana kiasi kwamba tuone ni sawa sasa kila mkoa mkubwa hata kwa kilometa kadhaa tu ugawanywe ili...kusogeza maenedeleo karibu na wananchi'!!

Mbeya ilikuwa na Mkuu wa Mkoa Mmoja sasa Itabidi wawe Wawili, MaVX mawili, Ofisi Mbili za Wakuu wa Mikoa, Majengo Mawili ya kuishi ya Wakuu wa Mikoa...
Halafu chukua Idadi ya Wakuu wa Wilaya zidisha mara mbili na gharama kama za hao wakuu wa mikoa.
Bado tutaongeza idadi ya majimbo ya kura na kwa maana hio idadi ya Wabunge ambao watatuzidishia tu Gharama za kuwatunza.
Mwisho wa Siku tunajiuliza, Je Gharama hizi zilizoongezeka kutokana na kugawanywa Mkoa Mmoja Kweli zinaweza kufidiwa kwa hicho kinachoitwa n 'kusogeza maendeleo kwa Wananchi'???
Hivi kweli hatuna Busara kiasi cha kutoona kuwa huu ulikuwa ni muda wa Kupunguza idadi ya Mikoa yetu na sio Kuiongeza??
Hivi tatizo la kuwa na majimbo badala ya Mikoa na kwa maana hiyo kuwa na majimbo/mikoa isiyozidi 15 tu ni Nini????
:suspicious:
 
WAZO LA KUUGAWA MKOA WA MBEYA NI LA MSINGI NI MKOA MKUBWA SANA.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa wa Mbeya ubaki kuwa na makao makuu mbeya mjini kama ilivyokuwa zamani ukiwa na wilaya za Mbalali, Momba, Chunya na mbeya mjini. Mbeya mjini imekaa katikati ya wilaya hizo kwa kufikaki kirahi ikiwemo miundombinu yake iko tayari kupokea mabadiliko na huduma mpya za mkoa mpya.

Halikadhalika, RUNGWE ina sifa hizo hizo ikiwemo mlima maarufu wa Rungwe ambapo utatangazwa kitaifa na kimataifa. Aidha, Rungwe ndio Wilaya inayoongoza kwa uzalishaji katika mkoa wa mbeya hasa kwa mazao ya kilimo. Rungwe ni moja ya majina ya kale ya mkoa wa mbeya tangu enzi la ukoloni kutokana na jina hilo kuakisi mlima Rungwe. Tangu enzi la mkoloni Tukuyu kwa jina hilohilo ndio ilikuwa makao makuu ya Rungwe enzi hizo na ndio sababu Tukuyu ikapata maendeleo haraka baada ya mbeya mjini.

Naunga mkono wale wanaosema mkoa mpya uitwe Rungwe na makao yake makuu yawe Tukuyu. Mkoa wa Rungwe uwe na wilaya za Rungwe, Kyela, Ireje na Mbozi

Mkoa wa mbeya ndio mkoa mkubwa kuliko yote nchini kwa sasa ndio maana hata Iringa umegawanya na Arusha. kwa wale wanaoifahamu mikoa hiyo naamini wataniunga mkono tofauti na ambao hawajui vizuri jiografia ya mbeya na mikoa mingine ilivyogawanywa.
Hapo penye redi ni wapi?
 
Mama Porojo kwenu Rungwe nini?Maana nijuacho ni kuwa mkoa sawa utagawanywa ila MMOJA UTAITWA MBEYA NA MWINGINE KIWIRA kwa mujibu wa vikao vya hapa na pale mkoani sasa ilo la mkoa kuitwa Rungwe na nakusikia wewe.
Usikute ndo umeamua kulipigia chapua na wanaotoka Kyela watakuja sema mkoa uitwe Kyela utawaelewa kweli?
Dhana ya kuugawa mkoa personally ninaiafiki in the sense kwamba huduma zinasogezwa karibu na jamii such that ata management yake inakuwa rahisi.
Pia mkumbuke miaka ya 1980 mkoa wa Rukwa ulimegwa toka Mbeya so ni utaratibu ambao huiva with time.
 
Kumbe ndio maana mnataka kugawa nchi kwasababu ni Kubwa hadi Pemba? Ukubwa si sababu ya kugawanya Mikoa huo ni uvivu wa kufikili pigeni hesabu ya gharama zitakazo ongezeka.
 
TAARIFA ZIFUATAZO ZITATUSAIDIA KULICHAMBUA HILI

Southern Highlands Province then In 1963, the Southern Highlands Province was split into two regions ie Mbeya and Iringa.

1974 Sumbawanga District was separated from Mbeya and accorded full Regional status. Bila kuwa na iyo migawanyo kwa sasa tusingekuwa na mkoa wa mbeya wala rukwa wala iringa maana yote iliitwa Southern Higland Province

Mbeya Regional area covers 63,420 Sq.kms. which is 6.4% of the

Total area of the United Republic of Tanzania.

Rwanda: total: 26,338 sq km & Burundi total: 27,830 sq km kwa ujumla wao hawaufikii mkoa wa Mbeya kila inchi apoinaingia Mbeya kama mara 3
 
Mama Porojo kwenu Rungwe nini?Maana nijuacho ni kuwa mkoa sawa utagawanywa ila MMOJA UTAITWA MBEYA NA MWINGINE KIWIRA kwa mujibu wa vikao vya hapa na pale mkoani sasa ilo la mkoa kuitwa Rungwe na nakusikia wewe.
Usikute ndo umeamua kulipigia chapua na wanaotoka Kyela watakuja sema mkoa uitwe Kyela utawaelewa kweli?
Dhana ya kuugawa mkoa personally ninaiafiki in the sense kwamba huduma zinasogezwa karibu na jamii such that ata management yake inakuwa rahisi.
Pia mkumbuke miaka ya 1980 mkoa wa Rukwa ulimegwa toka Mbeya so ni utaratibu ambao huiva with time.

[h=3]MKOA WA MBEYA KUGAWANYWA[/h]

HATIMAYE Mchakato wa kuugawa mkoa wa Mbeya umeingia katika hatua nyingine , baada ya baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Mbarali kujadili, kutoa maoni na kuridhia mapendekezo kuhusu kugawa mkoa huo kwa lengo la kusogeza huduma za maendeleo kwa wananchi.
Wakijadili hatua hiyo ya pili jana katika kikao cha wataalamu ,waliridhia mapendekezo ya sekretarieti ya mkoa, chini ya Mkuu wa Mkoa Abass Kandoro ya kuzitaka halmashauri zote mkoani hapa kutoa maoni.

Hayo yamebainika wakati wa kikao cha dhadhura cha Baraza la madiwani katika barua ya mapendekezo ya mkoa, iliyotumwa kwa wakurugenzi , ambayo ilisomwa na Katibu wa Kikao cha baraza la madiwani, Bw.Brown Kwakibete alisema kwa pamoja Halmashauri za wilaya zote mkoani hapa zinatakiwa kujadili maeneo makuu manne ambayo yatafanikisha vigezo vya kuugawa mkoa huo.

Maeneo hayo ni namna gani mkoa uweze kugawanywa, upewe jina gani, Makao makuu yake yawe wapi, pamoja na kujadili uwezekano wa kuanzisha wilaya mpya kama kutakuwa na mahitaji ya lazima.

Kufuatia hatua hiyo, madiwani hao kwa pamoja waliridhia mapendekezo hayo ya jopo la wataal;amu lililoketi Mei 22 mwaka huu na kueleza kuwa yatasaidia kuharakisha shughuli za maendeleo.

Hata hivyo madiwani hao wariridhia pia mapendekezo ya kutoigawa wilaya hiyo kutokana na jiografia yake kwa kuwa eneo kubwa linalokaliwa na watu ni pembezoni mwa barabara kuu ya Tanzania -Zambia, huku eneo kubwa likibaki likiwa ni hifadhi za Taifa Ruaha na pori la akiba la Kipengele.

Aidha, madiwani hao walishauri kugawanywa kwa jimbo hilo na kuwa mawili kutokana na kuwepo umbali mkubwa, mfano kutoka kata ya Ilongo hadi Madibila hivyo kufanya mbunge mmoja kushindwa kutoa huduma bora kwa wakati kwa wananchi wake.

Katika mapendekezo hayo ya wataalamu, walipendekeza jina la mkoa mpya utaaozaliwa kutokana na mkoa wa sasa wa Mbeya, upewe jina la Rungwe na Makao yake Makuu yawe mjini Tukuyu.

Wamependekeza kuwa Mkoa huo mpya wa Rungwe uwe na wilaya nne ambazo ni Mbozi, Rungwe, Kyela na Ileje.

Wakati mkoa mwingine uendelee kutumia jina la sasa la Mbeya nao ukiwa na wilaya nne za Mbeya, Mbarali, Chunya, pamoja na wilaya ya Momba na kwamba Makao Makuu yake atabaki kuwa Mbeya Mjini.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauriya Wilaya ya Mbarali Bw. Adam Mgoyi alisema kuwa mgawanyo huo utazingatia rasilimali zilizopo katika wilaya husika .

Mwandishi: ESTA MACHA
Mhariri: JOHNSON JABIR
 
TAARIFA ZIFUATAZO ZITATUSAIDIA KULICHAMBUA HILI

Southern Highlands Province then In 1963, the Southern Highlands Province was split into two regions ie Mbeya and Iringa.

1974 Sumbawanga District was separated from Mbeya and accorded full Regional status. Bila kuwa na iyo migawanyo kwa sasa tusingekuwa na mkoa wa mbeya wala rukwa wala iringa maana yote iliitwa Southern Higland Province

Mbeya Regional area covers 63,420 Sq.kms. which is 6.4% of the

Total area of the United Republic of Tanzania.

Rwanda: total: 26,338 sq km & Burundi total: 27,830 sq km kwa ujumla wao hawaufikii mkoa wa Mbeya kila inchi apoinaingia Mbeya kama mara 3

Kwa takwimu zako ina maana mkoa wa mbeya ni mkubwa mara mbili ya nchi ya Rwanda na Burundi.

tatizo la JF hata wale ambao hawajawahi kufika mbeya watabisha hadi mwisho. Nimefanya kazi mkoa wa mbeya kwa miaka 5 na kuuzunguka mkoa wote hata kuliko baadhi ya wanyakyusa wenyewe. najua ninaongea nini bila hata chembe ya siasa na ndio maana nikaweka kinga kwamba watu wa mbeya naomba waje hapa wanikosoe pengine ndio nitaelewana nao vema. Tatizo hili suala linawekwa kiCCM na KiCHADEMA.

Ukiwauliza watu wa mbeya walio mbali na mbeya mjini wapo wanaokiri kwamba kufikiwa na maendeleo au mgawo wa kitaifa wa fungu la mkoa ni ndoto kutokana na ukubwa wake, hivyo wangependa kupata fungu la mkoa ambao umepunguzwa kidogo ukubwa.
Ni nani asiyejua kuwa fungu la mkoa, wilaya, kata, kijiji lina tofauti kubwa.

Ni nani asiyejua kuwa mtu aliye na watoto wachache ana uwezekano mkubwa wa kuwamudu watoto wake kimaisha kuliko mtu mwenye watoto wengi? ( everything being consitant).
 
Kuna watu wanatafutiwa ajira hapo.Badala ya kuanzisha viwanda vingi ili kupanua ajira sisi tunakazana kuzalisha mikoa na wilaya kwa nia ya kuongeza ajira.
 
Mkoa wa mbeya ndio mkoa mkubwa kuliko yote nchini kwa sasa .....

Hapa nahisi ulinogewa...
Kimsingi pamoja na kugawanywa kwa mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Arusha, Rukwa bado mkoa wa Mbeya sio wa kwanza kwa ukubwa hapa Tanzania.
Ukubwa wa mikoa kulingana na maeneo yake upo kama ifuatavyo:
1. Tabora
2. Morogoro
3. Lindi
4. Ruvuma
5. Mbeya

na kuendelea...

Ukubwa wa mikoa kutokana na idadi ya watu:
1. Dar es Salaam
2. Mwanza
3. Zanzibar
4. Arusha
5. Mbeya
 
mbona arusha, shinnyanga, rukwa , isringa zimegawanywa hakuna tatizo. kugawanya mbeya ni tatizo? mwacheni rais agawanye mkoa kulingana na utawala wake. huu ni utaratibu wa kawaida kwani hata rukwa ilitoka mkoa wa mbeya. wanaopinga wana lao jambo. mbona wilaya zimeendelea kugawanywa hampingi? wilaya ya rungwe itakuwa na wilaya za tukuyu, busokelo, kyela, na ileje. mbeya itabaki na mbalali, momba,mbozi, mbeya jiji, mbeya vijijini na chunya.
 
Back
Top Bottom