Madiwani waliotimuliwa Chadema Arusha waomba radhi, Napendekeza wasamehewe

Nyuma ya hao madiwani kuna ccm, stukeni. Msamaha nawatangazia lakini hakuna kugombea wadhifa wowote kwa miaka 5.
 
ningeshauri watoe shitaka lao mahakamani wenyewe bila ya shuruti ndipo waombe radhi kwa chama na wanachamakwa kuleta mizengwe yenye sura za kifisadi na hatua ya mwisho waahidi kuwa wanachama waaminifu ndani ya chama. cdm kwa upande wake watumie busara ya kuwaweka chini ya uangalizi kwa kupindi chote kilichobaki hadi 2015 bila mamlaka yoyote ndani ya chama.
 
Kwanza ni vema tuone content ya barua yao ya kuomba msamaha.

Humo nataka kuona wameomba radhi kwa kosa gani? kwa nini sasa? nk nk

Msamaha ni matokeo ya toba ya kweli. Tuone hiyo toba kwanza.
 
Hawa madiwani at that time itakuwa walivuta bangi, but cdm itafakari kwa makini na kama itajiridhisha na uamuzi wa kuwasamehe basi wawasamehe but kwa dhambi ya usaliti waloifanya ni mbaya sana kwani hawakujali hata mda na nguvu zilizopotea kwa ajili yao but if pocbo wasamehewe na waongozwe sala ya toba ya kikamanda ili wasirudie tena ule ushetani walowahi kuufanya huko nyuma.
Solidarity forever
toralence gives power.
 
Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi

Wasisamehewe ili waache undumila kuwili na zito ajifunze ktk hili kwani kuna siku utamtokea puani
 
Vipi, kwani wameelewa kosa walilolifanya, na walistahili adhabu gani kwa kola hilo wanaloombea msamaha wake. Kama hilo, wanalifahamu, ninapendekeza wapate kwanza adhabu stahiki, ndo waombe msamaha. Huu utamaduni wa kukimbilia kutoa misamaha kabla ya kutenda haki ndo imelifikisha taifa lilipo, -chota billion 60 unapewa mshamaha. Tutafika kweli, kwenye kilele cha maendeleo kweli kwa mwendo huu!
 
Nawashauri viongozi wa CHADEMA Taifa, watafakari jambo hili kwa kina; kisha watafakari kwa kina na kuangalia uwezekano wa kuwasamehe iwapo wataweka dhambi zao hadharani.
 
Tutawasamehe 2016 kama wanahitaji kusamehewa waendelee kuvumilia
 
Mmmhhh hili ungamo mbona sina imani nalo!

Ukifuatilia mtiririko wa matukio utajiuliza.... KWANINI MSAMAHA SASAHIVI??
Wawekwe kwenye kipindi cha mpito kuwaangalia, haihitaji haraka na hawa watu tunawamudu sana!

Waombe upya kama wanachama wengine wapya, ila wasipewe nafasi ya kugombea nafasi yoyote ndani ya chama kwa kipindi cha miaka mitatu-ili wajuwe CDM siyo kokoro kama CCM!
 
na mnaturudisha nyuma!!....swala la madiwani lilishafungwa wao waliidharau kamati kuu ya Chadema, by the way vyama vya siasa vipo 18 ni kwa nini wasiende kwenye vyama vingine!! why Chadema?.....

Umeona mbali sana mkuu.Hongera kwa hilo
 
na mnaturudisha nyuma!!....swala la madiwani lilishafungwa wao waliidharau kamati kuu ya Chadema, by the way vyama vya siasa vipo 18 ni kwa nini wasiende kwenye vyama vingine!! why Chadema?.....

Umeona mbali sana mkuu.Hawa jamaa kuna mkono wa ccm nyuma yao,ila kwa sasa nahisi aliyekuwa anawapa kiburi kawatelekeza baada ya kufanikisha kumwengua Lema.WASAMEHEWE ILA ADHABU NI KWAMBA WASIRUHUSIWE KUGOMBEA CHEO CHOCHOTE KWA MIAKA MITANO
 
Ni swala gumu sana, linahitaji kuonyesha character, na maturity ya kisiasa
 
pinda hayuko kwa ajil hy yk kwny u mkutan wa wahasib au wakaguz kitu kama hch na leo alienda minjingu .pinda sio mwanasiasa mshawishi hana uwezo huo
 
Patamu hapo, Hali ngumu mtaani. Wasameheni tu wameshajifunza.
 
Chadema wangejitahidi kesi ya madiwani iishe ili uchaguzi utupatie madiwani wageni wawili tuwe wengi kuliko CCM na TLP
 
Jamani hizi ni trick za chama la majoka mbona wazito ninyi kustuka!!! Kumbuka Mh.Lema hakukubaliana nao wakati ule wa muafaka fek mpka wakatimuliwa sasa iweje waje kuomba kusamehewa leo baada ya Lema kutenguliwa??? hebu jiulizeni kwa nini hawakufanya hivi kabla ya lewa bado mbunge?? hawa ni wadiwani maslahi tu waha na kama kweli watasamehewa duuh hii itakuwa kulamba matapishi!! Wanatumika hawa kutugawa wapo kwa ajili ya maslahi tuachane nao plzzz!
 
Back
Top Bottom