Madiwani waliotimuliwa Chadema Arusha waomba radhi, Napendekeza wasamehewe

ibange

JF-Expert Member
Dec 31, 2010
1,545
550
Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi
 
Safi sana,kwa anayejua utaratibu atujuze, kama watasemehewa nini kitajiri, je watarudishiwa udiwani wao
 
kusamehewa kupo kama kweli wameomba radhi lakini sio kupewa dhamana tena.
 
na mnaturudisha nyuma!!....swala la madiwani lilishafungwa wao waliidharau kamati kuu ya Chadema, by the way vyama vya siasa vipo 18 ni kwa nini wasiende kwenye vyama vingine!! why Chadema?.....
 
Mi nina shauri wasamehewe lakini wasirudishwe udiwani wala wasipewe nafasi ya kugombea nafasi yoyote na ikiwezekana waende CCM,kuna wakati Pinda alionyesha nia ya kuwataka.Ukiangalia jinsi Mh.Mbowe na Slaa wanavyojitolea katika chama isingetakiwa wadharau kabisa
 
Wana-ARUSHA hatuwataki hao mfisadi. Wakisamehewa na kurudishiwa udiwani wao sisi wana ARUSHA tupo tayari kuondoka CHADEMA. hata KAMANDA MBOWE analijua hilo. Infct HATUWATAKI TENA. huo ndiyo msimamo wa watu wa ARUSHA majoritly
 
Ninaunga mkono, kusamehe ni sheria mojawapo ya Mungu. Wasamehewe kwa vile wametambua kosa walilolifanya na unafiki wao. Watakuwa watendaji wazuri na wawakilishi wema wa wananchi.
 
Nafasi nyingine ya CDM kuonyesha iko kwa maslahi ya wananchi au la. Maamuzi yoyote yasiangaliwe kichama bali yazingatie je wakisamehewa au wasiposamehewa...... ni wananchi au CDM inaathirika zaidi. Nakubali kama CDM imeathirika sana na tabia hizi za madiwani, hata kikiwasemehe kitaathirika kwa namna fulani.

Lakini kutakuwa na nafuu kwa wananchi kama CDM itaamua kuwasamehe na pia itaonyesha uungwana na moyo wa kusamehe maana kila mtu hukosea- give them another chance wasameheeni na kuwarudhishia udiwani huo ndo msamaha wa ukweli
 
CCM ni wajanja hii ni mbinu ya kuimaliza chadema endapo uchaguzi wa bunge utarudiwa katika jimbo la Arusha mjini. Hawa madiwani wakisamehewa watasimama kama wako chadema lakini watakuwa mamluki wa CCM katika ngazi ya kata zao kuchakachua ushindi wa chadema.

Tukumbuke nguvu ya madiwani katika ngazi ya kata ni kubwa. Chadema kuweni makini na agenda hii.

Pinda alikuwa Arusha kupanga mbinu mpya ya namna ya kuipa ushindi CCM kama uchaguzi utarudiwa endapo Lema atashindwa Rufaa.
 
Kushindwa mahakamamni kwa Lema kumechangiwa sana na madiwani hawa kwani ni waasi nalazimika kuamini kwamba wakati wa kesi hiyo walishiriki kuihujumu chadema chini chini kwa kuwa Lema alikuwa mwiba kwao katika suala la Arusha sasa wanarudi na kuomba radhi pengine wanafahamu kuwa rufaa ya Lema hatashinda.

Chadema mkitaka kupoteza umaarufu Arusha warudishe hawa waasi.

Mgogoro huu wa madiwani umerudisha nyuma wajibu wao kwa wananchi kupitia chadema hawafai hata kidogo.

Kama wana uhakika wa kurudi kwenye udiwani kupitia chama chochote sio lazima warudi CDM vyama viko vingi
 
Kamwe isitokee,chama hakijaathirika kutemwa kwa kina mallah sidhani kama kina slaa watakibakiza salama chama kwa kuwasamehe hawa matumbo.arusha we don want ppl like rasta mallah and bayo
 
walipewa muda wa kuomba msamaha wakajifanya wajuaji kwa kudanganywa na nyan wassiira hatutaki kuona watu wenye upeo mdogo kuongoza chama cha ukombozi wa mtanganyika. Ambaye hana uhakika chadema inafanya nini weka kushoto dereva mwingine endesha gari
 
Mmmhhh hili ungamo mbona sina imani nalo!

Ukifuatilia mtiririko wa matukio utajiuliza.... KWANINI MSAMAHA SASAHIVI??
Wawekwe kwenye kipindi cha mpito kuwaangalia, haihitaji haraka na hawa watu tunawamudu sana!
 
CCM ni wajanja hii ni mbinu ya kuimaliza chadema endapo uchaguzi wa bunge utarudiwa katika jimbo la Arusha mjini. Hawa madiwani wakisamehewa watasimama kama wako chadema lakini watakuwa mamluki wa CCM katika ngazi ya kata zao kuchakachua ushindi wa chadema.

Tukumbuke nguvu ya madiwani katika ngazi ya kata ni kubwa. Chadema kuweni makini na agenda hii.

Pinda alikuwa Arusha kupanga mbinu mpya ya namna ya kuipa ushindi CCM kama uchaguzi utarudiwa endapo Lema atashindwa Rufaa.
Inawezekana mawazo yako ni sawa, lakini kumbuka kule Meru kata 17 zote madiwani ni CCM mbona walishindwa kuisaidia ikashinda uchaguzi? Hakuna wa kuzuia nguvu ya umma bwana. Kama ni kuwasamehe wanaweza kusamehewa lakini udiwani sijui sheria imekaaje, maana bado kesi iko mahakamani. Wanaojua sheria zetu watujuze
 
Mimi wasiwasi wangu ni kwamba kata hizi hazina madiwani hivyo ccm wanajenga kata zao 2015 watasema chadema haijafanya kitu. Pili kesi inachukua muda mrefu na pia wanaweza kushinda wakawa madiwani wa mahakama wakatusumbua sana. Mimi nadhani tuzungumze na wana Arusha kuwa tuwasamehe ila waombe radhi kwa umma wa cghadema na wakae chini ya uangalizi wa katibu mkuu kwa muda wote uliobaki hadi 2015 pamoja na kupewa onyo kali
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom