Madiwani waliotimuliwa Chadema Arusha waomba radhi, Napendekeza wasamehewe

Mimi nadhani wasamehewe na wawarudisha katika udiwani kuepuka gharama nyingine za uchaguzi endapo sheria ina ruhusu. Kama sheria itataka uchaguzi urudiwe basi kuna haja ya kukaa chini na kutafakari upya kwa wao kuwa wagombea tena. Busara itumike zaidi.

Kweli wewe mbuzi! na post zako 14 umetumwa hapa kushauri huu upuuzi wenu! ha ha ha! unatoka maji yanukayo wewe both sides!
 
Mimi naona wanakumbuka shuka pamekucha kama watataka wasamehewe waweke mambo wazi yaliyokuwa nyuma ya pazia na wananchi wawasikie ili waamue kwa yaliyokuwa nyuma yao lakini ni bora zaidi wasiruhusiwe kugombea tena ila wakiweka wazi yaliyokuwa nyuma ya pazia basi wamalizie kipindi chao na hivyo basi itakuwa fundisho kwa watu wenye tabia hiyo
 
Wakuu
Mjadala mzuri. Lakini uko nusu. Kuna vitu tunaweza kuviweka hapa kuliweka sawa suala hili la hawa watu waliofukuzwa uanachama kuandika barua wakiomba kusamehewa na kurudishwa kundini. Ni vyema mleta mada akaiweka hiyo stori nzima ili tujue kilichoandikwa, tuchangie vyema na kutoa taarifa iliyo kamili watu waelewe nini hasa wajadili au wajue kinachoendelea. Haya wakubwa.

Feedback
Nimejaribu kuitafuta habari hii kwenye gazeti la Mwananchi lakini sijaiona.
Hata kama ni habari ya kweli hawa watu si wa kuaminiwa tena. Nakumbuka walipohojiwa Dodoma walisema wanaomba radhi lakini tukasikia tena wamefungua kesi kupinga kufukuzwa. Nafikiri hii imekuja baada ya kujitahidi kukivuruga chama wakishirikiana na CCM (Pinda) bila mafanikio. CCM wameona hata wakiitisha uchaguzi na kuwatumia hao madiwani hawawezi kushinda. Hivyo lililobaki ni wao kujifanya wamejirudi wasamehewe na wapewe udiwani wao kuepusha aibu itakayoipata CCM endapo uchaguzi utarudiwa. So, CDM be careful with this trick.

Ni kweli ilikuwa taabu sana kuipata na kuisoma habari hii kwani iko kwenye latest pages za Mwananchi ya Jumatatu, April 16, 2012, pg. 14. Inasema hivi:

WALIOTIMULIWA CHADEMA ARUSHA WAMPIGIA MBOWE:

Hatimaye madiwani watano wa CHADEMA waliofukuzwa kisha kuvuliwa uanachama na Kamati kuu ya Chama hicho, sasa wameamua kumwangukia M/kiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, wakimwomba awarejeshee uanachama.

Pia, madiwani hao wamemwomba radhi Mbowe kwa kuharakisha hatua ya mwafaka wa utatuzi wa mgogoro wa umeya wa Arusha bain ya CCM na CHADEMA, kwa madai kwamba hawakuwa na nia mbaya wala hawakutarajia hali hiyo kujitokeza.

Kwa mujibu wa vyanzo vya habari vilivyolifikia gazeti hili, vinadai kwamba hivi karibuni madiwani hao waliamua kumwandikia barua Mbowe kuwarejeshea uanachama wao.

Barua hiyo ambayo imesainiwa na madiwani wote watano na nakala yake kupelekwa moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dr. Willibrod Slaa na kwa katibu wa CHADEMA mkoani Arusha, Aman Golugwa, inasema hakuna usaliti waliofanya ndani ya chama wala hawakupokea rushwa bali walichafuliwa.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, sisi tunaomba radhi kwa kuharakisha ile process ya mwafaka na kufikia mwisho, hatukuwa na nia yoyote mbaya dhidi ya chama wala viongozi wake na wala hatukutegemea yaliyojitokeza baada ya mwafaka ule" inasema sehemu ya barua hiyo.

Alipoulizwa Mallah, mmoja wa madiwani hao kuhusu barua hiyo, alikiri kuandika kuomba kurejeshewa uanachama na kwamba uamuzi ulitokana na baada ya wao kutafakari na kushauriana hatima yao kisiasa.

Naye Katibu wa CHADEMA mkoani Arusha, Golungwa alikiri madiwani hao kuandika barua hiyo, lakini alisisitiza kuwa haiwezi kujadiliwa au kushughulikiwa na chama kwa sababu si wanachama wao.
 
Nina uhakika Dr Slaa na mbowe mtakuwa makini na watu wanafki kama hawa, kweli wanaweza kusamehewa lakini lazima muwaweke chini ya uangalizi mkali ili ikigundulika ni magamba tuwatimue moja kwa moja.
 
Wana JF.
Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutafuta muafaka wa kutatua mgogoro uliokuwepo baina yao na madiwani watano wa mkoa wa Arusha.

Jitihada zimeanza kuonekana baada uongozi wa Chadema kuwasihi waufute kesi yao ya msingi waliyofungua katika mahakama kuu kanda ya Arusha ili waweze kurejeshewa uanachama wao na kuumaliza mgogoro huo.

Madiwani watano waliofukuzwa na kamati kuu ya chama hicho ni pamoja na aliyekuwa Diwani wa Kata ya Themi, Ruben Ngowi, Diwani wa Kata ya Kimandolu, Estomi Mallah, Diwani wa Kata ya Kaloleni, Charles Mpanda 'Rasta', Diwani wa Kata ya Elerai, John Bayo Sanjari na Diwani wa Viti maalum, Rehema Mohamed.

Mei 3, Mwenyekiti wa Chadema mkoa wa Arusha Samson Mwigamba aliitisha kikao cha faragha na madiwani hao katika Hoteli ya Sowote Garden kwa lengo la kuwasihi waumalize mgogoro huo kuwataka wafute kesi yao ya msingi.

Hata hivyo madiwani waligoma ombi ilo kwa madai kwamba warejeshewe kwanza uanachama waliofutiwa ndani ya chama hicho.

SOURCE: MWANANCHI MAY 25 2012.
 
walimalize shauri lao hilo ili kuijenga vema CHADEMA Arusha. Migogoro ndani ya chama haijengi zaidi inabomoa tu.
 
Uongozi CDM unadaiwa kutafuta muafaka wa mgogoro uliopo kati yao na madiwani watano wa Arusha, walofukuzwa na kuvuliwa uanachama mwaka jana na Kamati Kuu ya CDM.
Jitihada hizo zimeanza kuonekana kwa kufanya mazungumzo na madiwani hao kwa lengo la kuwasihi wafute kesi yao ya msingi waloifungua ktk mahakama kuu ya kanda ya Arusha ili waweze kurejeshwa uanachama na kumaliza mgogoro.
Muafaka haukutimilika baada ya Madiwani kutaka warudishwe uanachama kwanza ndipo wafute kesi.

My take: M4C table 4 two"
 
ni vizuri kuweka mambo sawa kama wakikubali walipotoka na kuomba radhi wasamehewe tu warudi kutumikia wananchi na kujenga chama hasa wakati huu wa M4C!Busara itumike zaidi kuliko nguvu!
 
Aaaaaaaaa, mi nishachoka sasa na hii migogoro ndani ya vyama ambayo haina kabisa manufaa.
 
Back
Top Bottom