Madiwani waliotimuliwa Chadema Arusha waomba radhi, Napendekeza wasamehewe

Inawezekana mawazo yako ni sawa, lakini kumbuka kule Meru kata 17 zote madiwani ni CCM mbona walishindwa kuisaidia ikashinda uchaguzi? Hakuna wa kuzuia nguvu ya umma bwana. Kama ni kuwasamehe wanaweza kusamehewa lakini udiwani sijui sheria imekaaje, maana bado kesi iko mahakamani. Wanaojua sheria zetu watujuze

Pamoja na hayo yote mheshimiwa...nasikia kichefuchefu kwa hawa jamaa..kikubwa wangetakiwa kujiunga na mbunge kutetea maslahi ya wananchi wa Arusha. Mbona wanaomba msamaha wakati mbunge hayupo? Tujue kwamba hata kesi ya mbunge wao wamechangia kufanya maamuzi yawe kama yalivyokuwa....mm siafiki msamaha kwao...waende chama kingine chochote kwani walipewa nafasi na kuombwa na wazee wakawa kichwa ngumu...wanahudhuria vikao vya halmashauri na posho wanakula...Hii busara ya kuomba msamaha wameipata wapi wakati huu?..CDM kuweni macho this people are virus which will destroy the part if allowed to come in...wametukosea wanachadema na si viongozi peke yao...
 
Ninaunga mkono, kusamehe ni sheria mojawapo ya Mungu. Wasamehewe kwa vile wametambua kosa walilolifanya na unafiki wao. Watakuwa watendaji wazuri na wawakilishi wema wa wananchi.

wasamehewe ila hawafai kuwa viongozi ngazi yeyote ile!
 
Ninaunga mkono, kusamehe ni sheria mojawapo ya Mungu. Wasamehewe kwa vile wametambua kosa walilolifanya na unafiki wao. Watakuwa watendaji wazuri na wawakilishi wema wa wananchi.

utawaamini vipi hao watu wazima walishaombwa mpaka watu wakatoka dar kuja kuongea nao nafikiri alikuwa marando lakini hawakusikia kwa sababu walikuwa wanapewa jeuri na ccm sasa nafikiri ccm wameshawasahau,hawakujuwa ccm ina wenyewe ....chadema ni ya woooote

CDM Arusha tusirudi nyuma, walishatimuliwa kwenye chama, kama wanataka kurudi kwenye chama wanatakiwa waombe upya, hapa ndipo tutapata muda wa kuwasaili na kupata mbivu na mbichi. Kukaa bila madiwani hizo kata ni mbinu ya CCM ili watumie kama mtaji 2015. Tuwe macho na hawa madiwani, inawezekana ikawa mbinu ya c. tawala kutupeleka na matukio tukasahau mambo ya msingi, kwani kila baada ya kipindi fulani wanakuja na jipya kabla hatu
jamaliza la awali. They are trying to keep us busy with various events!!
 
hilo nalo neno
Mmmhhh hili ungamo mbona sina imani nalo!

Ukifuatilia mtiririko wa matukio utajiuliza.... KWANINI MSAMAHA SASAHIVI??
Wawekwe kwenye kipindi cha mpito kuwaangalia, haihitaji haraka na hawa watu tunawamudu sana!
 
waitishe kikao cha hadhara na wawambie wananchi ilikuwaje wakarubuniwa na ccm......na waombe msamaha wananchi wa arusha
 
Mimi nadhani wasamehewe na wawarudisha katika udiwani kuepuka gharama nyingine za uchaguzi endapo sheria ina ruhusu. Kama sheria itataka uchaguzi urudiwe basi kuna haja ya kukaa chini na kutafakari upya kwa wao kuwa wagombea tena. Busara itumike zaidi.
 
Wana-ARUSHA hatuwataki hao mfisadi. Wakisamehewa na kurudishiwa udiwani wao sisi wana ARUSHA tupo tayari kuondoka CHADEMA. hata KAMANDA MBOWE analijua hilo. Infct HATUWATAKI TENA. huo ndiyo msimamo wa watu wa ARUSHA majoritly

Source?!!!
 
Wakuu

Mjadala mzuri. Lakini uko nusu. Kuna vitu tunaweza kuviweka hapa kuliweka sawa suala hili la hawa watu waliofukuzwa uanachama kuandika barua wakiomba kusamehewa na kurudishwa kundini. Ni vyema mleta mada akaiweka hiyo stori nzima ili tujue kilichoandikwa, tuchangie vyema na kutoa taarifa iliyo kamili watu waelewe nini hasa wajadili au wajue kinachoendelea. Haya wakubwa
.
 
Wana-ARUSHA hatuwataki hao mfisadi. Wakisamehewa na kurudishiwa udiwani wao sisi wana ARUSHA tupo tayari kuondoka CHADEMA. hata KAMANDA MBOWE analijua hilo. Infct HATUWATAKI TENA. huo ndiyo msimamo wa watu wa ARUSHA majoritly

Hiyo research uliifanya lini mkuu? Halafu inakuwaje unawasemea na wengine? Açha fitina mkuu! Wasamehewe kwa bure!
 
Huyu mwenyekiti wao Mallah alikuwa na ndoto za kutaka kugombea ubunge na hapo ndipo walipotofautiana na G.Lema. Kurudi kwake na kuomba msamaha baada ya Lema kuenguliwa ubunge ni janja ya kutaka kuja kutimiza malengo ya kugombea ubunge. Wanasiasa hawana mshipa wa aibu na hapa naona Mallah bado ana ambition za kugombea ubunge. Nasema wasamehewe na kurudishiwa udiwani kama inawezekana ila Mallah auvue unaibu Meya.
 
Hapa kuna tia shaka kwanini waombe kusamehewa baada ya mbunge kuenguliwa na imekuwaje wote kwa pamoja wawe na mawazo sawa ya kutaka kusamehewa hao wana lao jambo wasubiri chama cha kima Hamad kitafika Arusha.
 
Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi
Walisha omba masamaha siku nyingi tu huku wakifungua kesi mahakamani...hivyo masamaha wao niunafiki mtupu na hawana mapenzi ya dhati na chama ila ni wachumia tumbo....
Napendekeza wasisamehewe yaani wasirudishiwe uanacha wao tena kama vipi wakajiunge na magamba....
 
CCM ni wajanja hii ni mbinu ya kuimaliza chadema endapo uchaguzi wa bunge utarudiwa katika jimbo la Arusha mjini. Hawa madiwani wakisamehewa watasimama kama wako chadema lakini watakuwa mamluki wa CCM katika ngazi ya kata zao kuchakachua ushindi wa chadema.

Tukumbuke nguvu ya madiwani katika ngazi ya kata ni kubwa. Chadema kuweni makini na agenda hii.

Pinda alikuwa Arusha kupanga mbinu mpya ya namna ya kuipa ushindi CCM kama uchaguzi utarudiwa endapo Lema atashindwa Rufaa.

Kaka unazungumza nguvu za madiwani wepi? Kama wameshindwa mpaka wamefikia mahali pa kuomba rafhi hiyo nguvu ya kuichakachua chadema arusha wataitoa wapi? Usihofu chadema arusha everything is under control?
 
waitishe kikao cha hadhara na wawambie wananchi ilikuwaje wakarubuniwa na ccm......na waombe msamaha wananchi wa arusha
Watasthubutu kuitisha mkutano....kwanza waitishe mkutano kama wanachama wa chama gani au kama wasaliti wa chadema....
 
CCM ni wajanja hii ni mbinu ya kuimaliza chadema endapo uchaguzi wa bunge utarudiwa katika jimbo la Arusha mjini. Hawa madiwani wakisamehewa watasimama kama wako chadema lakini watakuwa mamluki wa CCM katika ngazi ya kata zao kuchakachua ushindi wa chadema.

Tukumbuke nguvu ya madiwani katika ngazi ya kata ni kubwa. Chadema kuweni makini na agenda hii.

Pinda alikuwa Arusha kupanga mbinu mpya ya namna ya kuipa ushindi CCM kama uchaguzi utarudiwa endapo Lema atashindwa Rufaa.
Mkuu wengi wao walichaguliwa kwa sifa ya chama na si kwa majina yao ndiyo maana hawana nguvu kwenye kata zao na nguvu waliyo kuwa nayo iliporomoka kwa kasi ya kutisha kiasi kwamba walikuwa hawathubutu haka kwenda baada......
 
Hiyo ni cancer itakitafuna chama ni waachwe moja kwa moja

Hatimaye madiwani waliotimuliwa na Chadema Arusha wameandika barua kwa Mbowe na Dr Slaa kuomba radhi wasamehewe.

Mimi napendekeza wasamehewe kwa sharti la kuondoa kesi mahakamani na pia waukane muafaka bandia. Inavyoelekea kesi itakaa hadi 2015 na wananchi wa Arusha watakosa maendeleo hasa ukizingatia hakuna mbunge.

Source. Mwananchi
 
Mimi nadhani wasamehewe na wawarudisha katika udiwani kuepuka gharama nyingine za uchaguzi endapo sheria ina ruhusu. Kama sheria itataka uchaguzi urudiwe basi kuna haja ya kukaa chini na kutafakari upya kwa wao kuwa wagombea tena. Busara itumike zaidi kuliko ushabiki. Na wao nao ni binadamu kama hao wengine tunaowaamini wanafaa zaidi.
 
Back
Top Bottom