Madiwani Mbeya wapongezwa kwa kuwafuta kazi watumishi wabadhirifu

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Jul 21, 2021
1,126
4,169
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa (Mb) amepongeza uamuzi uliofanywa na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Jiji la Mbeya ambalo ndio Mamlaka ya nidhamu ya Watumishi wa Halmashauri hiyo kwa kuchukua hatua kali ya kuwafukuza kazi watumishi wawili wa Halmashauri hiyo ambao ni Obely Mpamande Yesaya (Afisa Hesabu) na Nyando Christopher Nasson (Mhasibu Msaidizi).

Baraza la Madiwani limechukua hatua hiyo baada ya Timu ya Uchunguzi iliyoundwa kuthibitisha kuwa watumishi hao walihusika katika kukusanya mapato pasipo kuwa na Kibali cha Halmashauri na pasipo kutumia PoS za Halmashauri na kutumia fedha hizo za Serikali kwa manufaa binafsi.

Mhe. Mchengerwa amewaelekeza watumishi wote wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakisha wanafanya kazi kwa weledi na kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu. Aidha, amezielekeza Mamlaka za nidhamu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, kuendelea kusimamia nidhamu za watumishi na kuwachukulia hatua stahiki watumishi wote wabadhirifu wa fedha za Umma.

20231109_080509.jpg
 
Back
Top Bottom