Madirisha ya aluminium yanaruhusu mbu

Kakati

Senior Member
Apr 11, 2009
167
47
Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi.

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
 
Dah mkuu ilo tatizo hata mimi linanisumbua,haya madirisha yanapitisha mbu sana,Kuna wakati nilimuuliza fundi akaniambia kuna mipira inafungwa kuzuia mbu lkn nikimpigia simu aje anifungie hapokei simu tena,tunahitaji msaada haraka namna ya kuwadhibiti hawa mbu.
 
Aisee yanapitishwa vzr tu.... Labda ufunge yote... N

But ukifungua moja.. Kuna nafas kubwa tu inakuwepo katika zile reli hivo mbu wabapitia hapo... Soln kama Kuna reppelant Za kuweka hapo.

But swala la rubber Za kuweka hapo sidhan Kwan ku a nafas Kat ya ukingo wa dirishamojana kioo cha durisha la pili
 
Hilo tatizo hata mie linanikumba sana inabidi at least kila baada ya siku mbili kupuliza dawa. Kudhibiti hiyo hali lazima usifungue kabisa vioo jambo ambalo haliwezekani kwakweli. Hapo dawa mjitahidi ikifika saa 12 madirisha yafungwe then washa AC pakipoa unaizima ikikaribia muda wa kulala unawasha tena unaizima baada ya muda then mnakula fan tu.
 
Kwani mbu wanazuiwa na aina ya madrisha kwamba ukiweka hayo ya kisasa ndo mbu hawaingii ndani ya jengo lako! Suluhuya adha hiyo ni hakikisha chamber za Maji taka zote hazina upenyo wa mbu kufanya mazalia karibu na mji wako, pia uwe na utaratibu wa kuspray kuta madawa ya kuzuia wadudu kama mbu, nzi, mende, kunguni, utaishi kwa amani sana ukiwa na fumigation ya Mara kwa Mara kwenye kuta za nje zote yaani wadudu hutowasikia kwamwe.
 
Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi!

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
Nenda kwenye maduka yanayuoza vifaa vya madirisha hayo ununue mipira maalum ambayo hubandikwa pembeni ya fremu ya wavu, mimi bibafsi nimefanya hivyo japo si maduka yote wanauza mipira hiyo, nakushauri uende Gerezani Dar es Salaam.
 
K
Hilo tatizo hata mie linanikumba sana inabidi at least kila baada ya siku mbili kupuliza dawa. Kudhibiti hiyo hali lazima usifungue kabisa vioo jambo ambalo haliwezekani kwakweli. Hapo dawa mjitahidi ikifika saa 12 madirisha yafungwe then washa AC pakipoa unaizima ikikaribia muda wa kulala unawasha tena unaizima baada ya muda then mnakula fan tu.
Kama huna a c?
 
Hili tatizo ni sugu mfundi wa siku hizi wanaviwango vya chini

Madirisha yanaingiza mbu na ukija upepo yanagongana

Mim swala la mbu nimekata magodoro madogo nikaweka maana kila nikirudi home nakuita mbu nikawa Sijui kumbe Madirisha
 
Nenda kwenye maduka yanayuoza vifaa vya madirisha hayo ununue mipira maalum ambayo hubandikwa pembeni ya fremu ya wavu, mimi bibafsi nimefanya hivyo japo si maduka yote wanauza mipira hiyo, nakushauri uende Gerezani Dar es Salaam.
Asante kwa ushauri. Nitatafuta hawa jamaa.
 
Habari ndugu zangu.

Mimi nina jambo dogo, madirisha ya alminium, yanayo-slide yana upenyo naona kwenye nyumba yangu yenye wavu wa mbu kwenye madirisha mbu wanapita! Hizi reli zinaacha nafasi!

Hivi tatizo hili wengine mnalo? Au mmelizuiaje? Au mnalikabilije? Nisaidieni jamani.
By default kuna rubber mafundi hawaweki, ila ipo rubber ya kuzuia hyo nafasi ilo mbu wasipite.
 
Hili tatizo ni sugu mfundi wa siku hizi wanaviwango vya chini

Madirisha yanaingiza mbu na ukija upepo yanagongana

Mim swala la mbu nimekata magodoro madogo nikaweka maana kila nikirudi home nakuita mbu nikawa Sijui kumbe Madirisha
Mafundi ndio tatizo
 
Back
Top Bottom