Madini kunani mbona shida kila mwaka?

Karibuni

New Member
Jan 13, 2013
4
0
Wanafunzi wapatao 154 wa chuo cha Madini jumatatu tarehe 07/01/2013 waligoma kufanya mitihani ya Supplementary baada ya wenzao 55 kusemekana kwamba wali Disco katika mitihani yao.

Hatua hii ilifikiwa ikiwa inaonekana kuwa historia ya chuo hicho tangu kuanzishwa kwake haijawahi kutokea wanafunzi katika idadi hiyo Ku- Disco hali ambayo ilionyesha uwepo wa mazingira ya kutotendewa haki kwa wanafunzi hao.
Kufuatia Mgomo huo nilizungumza na Rais wa serikali ya Wanafunzi Bw, ........... ambaye kwa upande wake kwanza alianza kwa kukanusha kwamba ni Mgomo, akaendelea kwa kusema " Kilichofanyika sio Mgomo ila tulikaa sisi kama serikali ya Wanafunzi kujadili hatua ya Mazingira ya kitaaluma ambayo kimsingi yamekuwa sio rafiki kwetu (wanachuo) na kisha tukajaribu kukaa na Management kujadili matatizo hayo lakini mpaka mwisho hatukuweza kufikia muafaka ndipo tuliamua kusitisha zoezi la kufanya mitihani ya Supplementary kwa Baadhi ya wanafunzi chuoni hapa , Hata hivyo tuliamini maamuzi hayo ni sahihi kwa kuhofia hata hao walio kuwa wanaingia kufanya supp wangeweza kudisco pia kutokana na mazingira ya mitihani ambayo imekuwa ikitungwa ,Mfano Mwalimu anayefundisha ni tofauti na yule anayetunga Mitihani , hivyo hali hii inapunguza nia ya mwanafunzi kusoma na kumnyima haki ya msingi ya kutimiza kile kilicho mleta hapa chuoni" Alisema Rais huyo.



Hata hivyo ikumbukwe kwamba Chuo cha madini kilifungwa Tarehe 13/12/2012 baada ya mitihani kumalizika na kutoa fursa kwa wanachuo hao kwenda likizo kwa mategemeo ya kurejea chuoni (kufungua chuo) tarehe 12/01/2013. Kufuatia mlolongo huo baada ya matokeo kutoka wanafunzi walitakiwa kufanya mitihani ya supp tarehe 07/01/2013 mpaka 11/01/2013.
Baada ya tarehe 07/01/2013 wanafunzi kugoma kufanya mitihani ya Supp waliomba kukutana na Mwenyekiti wa Bodi ya chuo hicho Prof. Mruma, Ambaye alikuja na kukutana na wanafunzi hao kisha kukutana na management ambapo maamuzi yaliyofikiwa ilikuwa ni kufanya uchunguzi dhidi ya Madai ya msingi ya wanachuo hao ,hatua iliyopelekea tarehe ya kufungua chuo kusogezwa mbele mpaka tarehe 29/01/2013 ambapo kuna uwezekano wa Mitihani ya supp kuanza tarehe 20/01/2013 mpaka 25/01/2013 baada ya uchunguzi wa madai ya wanafunzi kukamilika mpaka itakapofikia tarehe 14/01/2013 imefahamika.
Hata hivyo katika hatua nyingine raisi wa Serikali ya wanafunzi (MRISO) Bw. President ameongeza kwa kusema tatizo sio wanafunzi ku-disco au kupata supp , suala la msingi hapa ni kuangalia je huyo mwanafunzi alistahili kupata hiyo supp au ku- Disco? Sasa hapa lazima haki itendeke kwa mwanafunzi . Alisema Bw. President. Alipotakiwa kueleza nini hasa ambacho kinafanyiwa uchunguzi mpaka sasa , Rais huyo alisema "Nadhani wanazo taratibu zao za kuhakikisha wanakidhi madai yetu ingawa naamini watapitia mitihani upya,Mitaala ya chuo na mambo mengine ambayo wao watadhani ni sahihi kwa lengo la kubaini kasoro"


Mwanafunzi mmoja ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema kwa hakika yamekuwepo mazingira kandamizi dhidi yao," Nasikitika baada ya baadhi ya walimu kufikiri jinsi gani watuinue kitaaluma wao wanafikiri jinsi ya kutuangamiza, alisema Mwanafunzi huyo huku akitokwa na machozi.
Licha ya hivyo tuliwasikia watu mbalimbali akiwepo raisi wa nchi anasifu wataalamu wa mafuta ila cha kushangaza hakuna wataalamu wtakoa toka palekwani mitaala mibovu na hata waalimu wa kufundisha hakuna.

Mimi Kibwetere Maji, Tukuyu- Mbeya. Past student wa MRI.
 
Muhongo yupo bize na kuwadhihaki wananchi wa mtwara wakati haelewi madudu yaliyopo katika chuo kilicho chini ya wizara yake.

Kheri yako wewe uliyeleta mada hii hapa, wanafunzi wanapata sana tabu kile chuo. Muhongo wacha porojo kakisafishe kile chuo la sivyo itageuka kampuni muda si mrefu.
 
Acha kupotosha umma wa Watanzania chuo kinaandaa watalamu si wahuni, waliofeli ni halali yao.
 
Back
Top Bottom