Madikteta wote duniani hufanana

Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
Wakati huo Mwanakijiji bado anaitwa Mwanakijiji.
 
Mzee Mwanakijiji,

Be honest to your fellow JF Members. Chambuzi zako before current leadership zilikuwa influenced na nini hasa?! Au shutuma za FaizaFoxy kwamba ukosoaji wako wa mara kwa mara kwa serikali ya JK ulisukumwa na chuki zako za kidini!!!

Look, threads zako za nyuma zinakuacha uchi wa mnyama tena ukiwa umejianika mbele ya halaiki!!! Yaani ni kiroja cha mwaka kuona thread kama hii kwako ilistahili sana kutolewa wakati wa utawala wa JK lakini hivi sasa; HAPANA!!

Kwa aibu, hii post hapa chini umei-delete ambayo ulikuwa unamlinganisha JK na hizo sifa ulizotaja hapo juu lakini eti sio John Pombe Magufuli!!!!!
View attachment 610308

Ni kigezo kipi miongoni mwa hivyo ulivyotaja ambavyo Rais Magufuli hana?! Magufuli yule ambae bila aibu mara kwa mara umekuwa ukija hapa kumtetea! Kila uovu ukifanyika lazima uje hapa ku-justify uovu wa utawala wake kwa kutumia maneno kama "...jambo kama hili si mara ya kwanza kutokea!" Maneno kama "....hata huko nyuma, so and so....!" Ben Saanane hafahamiki alipo and presumably dead!!! Tundu Lissu ameponea kwenye tundu la sindano na si ajabu akarudi akiwa kwenye wheelchair!!!

Lakini bila aibu kuna siku ulikuja ku-justify ushenzi kama huo kwa hoja kwamba "...hii si mara ya kwanza kutokea jambo kama hili!"

Narudia, uchambuzi wako miaka ya nyuma ulikuwa upo influenced na nini hasa?! Was really political anaylysis au ndo kama ambavyo FaizaFoxy alivyokuwa anasema??!!

Juzi ulilia lia kwamba eti natumia lugha kali! Kwa kawaida, ulimu ukiniteleza baadae huwa najutia kauli zangu lakini kwa kukutolea kauli juzi katu sijawahi kujutia kwa sababu, you deserved something more harsh kuliko lugha kali!!! Kama nilivyosema juzi, narudia tena hapa kwamba watu kama nyinyi ni watu hatari kwa ustawi wa jamii!! Ni watu ambao hamna tofauti yoyote na righthand men wa madikteta wote duniani!!! Ni watu mlioapa kutetea uovu bila uovu!!!

Maandishi yanaishi! In the next 15 years, yule mtoto wako ambae ulitutangazia hapa JF kwamba amezaliwa na kisha ukampatia jina la Kinyakyusa, wakati huo atakuwa old enough kusoma maandiko ya babake!!! Very sorry to that kid manake ataanza kuwa na ufahamu wakati babake akikazana kutetea uovu unaofanyika serikalini!!!

It's a matter of time ipo siku utakuja hapa na hoja zinazofanana na akina Mkamia cuz' that's what you're good at!!!
Kiukweli, katika wanafiki wanaoweza kubeba ngao/tuzo za unafiki, Mzee Mwanakijiji ni miongoni mwao. Na hili jambo ndiyo linatuumiza sana Watz, kwamba mtu anajipambanua kuwa na sifa Fulani kwa kipindi fulana na jamii inamwamini, kumbe ni koti la inafiki kavaa. Mara anajipambanua tena ktk uhalisia wake, na hataki kuelezwa kuwa zamani kidogo alikuwaje.
Lakini tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kutfunulia haya maana ni historia inaandikwa.
 
Kumekuwepo na ama maneno maneno au tuhuma mbalimbali ambazo zimekuwa zikielekezwa kwa viongozi mbalimbali wa Afrika na dunia kwa ujmla kuwa wanaongoza nchi katika mfumo wa kidikiteta au ni madikiteta kwa ujmla
Lakini Mimi ningependa kabla hatujamtuhumu kiongozi yeyote yule awe Wa Tanzania, Afrika au wa nchi za ulaya kuwa ni dikiteta, tupitie hapa sifa za dikiteta ndipo tuje tufanye hitimisho kuwa hpkiongozi huyo ni dikiteta au
Sifa zenyewe ni hizi hapa chini;
Udikteta ni mfumo wa utawala wa nchi ambapo mtu mmoja asiyebanwa nasheria wala katiba anashika madaraka ya serikali na ana uwezo wa kuyatumia jinsi anavyoamua mwenyewe.

1.Sheria na Haki za binadamu

Kila nchi inahitaji sheria na pia udikteta hauwezi kuongoza bila sheria. Lakini tabia muhimu ya udikteta ni ya kwamba dikteta ana nafasi au uwezo wa kupuuza sheria au kufanya maazimio nje ya sheria na hakuna njia ya kumlazimisha kutii sheria. Katika udikteta serikali inateua mahakimu na kuingilia kati katika maazimio ya kesi. Kama kesi inaangaliwa na serikali ni kawaida ya kwamba hukumu huamuliwa nje ya mahakama. Polisi inapewa nafasi ya kuwatesa watu na hii ni aina ya adhabu bila sheria wala mahakama.

2. Uchaguzi bandia
Utaratibu wa uchaguzi huru haufuatwi. Katika nchi kadhaa uchaguzi hufutwa kabisa kwa miaka mingi. Lakini mara nyingi kuna uchaguzi bandia badala ya uchaguzi huru. Kati ya njia mbalimbali za kuathiri matokeo ya uchaguzi ni. kutawala usimamizi wa uchaguzi na kutangaza matokeo kufuatana na mipango ya uongozi si kutokana na kura.

3. Uhuru wa maoni
Uhuru wa maoni unabanwa au hata kupigwa marufuku kabisa. Serikali inasimamia vyombo vya habari kama magazeti, redio na televisheni. Kutolewa kwa maoni yasiyopendwa na serikali ni vigumu.
Jambo la kawaida ni uteuzi wa habari zitakazoonekana kwenye vyombo vya habari.

4. Hakuna makosa

5. Sheria inakuwa upande wake ama kundi lake na anawataka watu wafanye bila kuuliza maswali chini ya mamlaka yake

6. Anawataka watu wafanye kwa ubora nyakati zote, hakuna kukosea, ukikosea kidogo tu hauna kazi tena

7. Hakuna Uhuru wa watu kusema au kukosoa
8. Dikteta anajua kuna nguvu katika maarifa ndio maana atafanya juhudi zote kuhakikisha watu anaowaongoza wanakosa maarifa Chama kimoja

Kwa kutathimini sifa hizo halo juu sasa unaweza kuja na majibu fasaha juu ya kiongozi Fulani wa nchi Fulani mbaye kwa namna moja ama nyingine umekuwa ukimuweka katika kundi LA madikiteta kubuhu au uchwara
Nawasilisha
Kama unazo sifa zingine ongezea ili tusaidiane kuwatambua madikteta
 
Wadau,hao madikteta niliowataja licha ya kufanya ukatili wa kila aina kwa raia wao, bado kuna watu ndani ya nchi zao waliwatetea kwa hali na mali na kujaribu kuaminisha umma kuwa wako sahihi kwa wanayofanyia wananchi wao.

Kuna waliokuwa wanawateta kwasababu tu walikuwa wamepewa vyeo na madikteta hawa,wengine kwasababu walikuwa wanalipwa na wengine kwasababu tu walikuwa na chuki binafsi na waathirika wa matendo ya watawala hawa.

Hivyo hata katika dunia ya leo haya mambo yatakuwepo tu kwasababu wenye chuki binafsi bado wapo,wenye kulipwa bado wapo,waliopewa vyeo bado wapo,n.k.

Hata hivyo,mambo yalipogeuka na kupelekea watawala hawa kupoteza dola,vibaraka hawa wengi wao waliwageuka na kujifanya ni sehemu ya wananchi waliokuwa wakifurahia anguko lao wakiwemo na wanajeshi waliokuwa wamekula kiapo cha kuwalinda na kuwatii na ambao waliokuwa wakipiga na kuua raia waliokuwa wakiandamana kupinga tawala hizi za kimabavu.

Msisahau hata utawala wa makaburu uliotesa na kuua raia wengi weusi wa Afrika kusini ulikuwa na support ya baadhi ya wazungu wenzao nje ya nchi hiyo lakini ni wazungu hao hao walikuja kupongeza kuisha kwa ubaguzi wa rangi na ni wazungu hao hao kutoka mataifa yaleyale waliomwagia sifa kedede Mzee Mandela aliewekwa jela na utawala wa makaburu.

Kwa kifupi,madikteta huwa hawana rafiki wa kweli wa kuwatetea bali huwa wana marafiki masilahi tu wa kuwaunga mkono wawapo madarakani na si vinginevyo.
 
Sifa yao ingine ni kwamba huhakikisha watu wote wenye uwezo hawapati nafasi katika fursa za uongozi wowote wala kupata kazi ya maana. Wakishindwa kabisa kuwakwamisha, huwafunga na/au kuwaua!
Huu ni uthibitisho kuwa Rais Magufuli sio miongoni mwao, kwa sababu yeye katoa nafasi, kawapa fursa.

Ila hili la kuwafunga watu au kuwaua, ukilifafanua, utatusaidia sana.
P
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)
Haya uliyoaandika na yanayoyokea hapa nchini kwa sasa yana mfanano pakubwa sana
 
Inaonekana watu hawashindwi kuwatambua madikteta; Kitila umesema point moja muhimu sana. Madikteta wanahofia sana intellectuals vile vile. Lakini upande mwingine kundi la wasomi hujitengeneza kama watetezi wa madikteta hao.
Mzee Mwanakijiji,

Maandiko haya uliandika wakati uleee..., akili yako ikiwa ktk hali njema sana ya afya...

Tazama sasa maandishi haya yanavyokuokoa leo hii UDIKTETA ukiwa umesha shika kasi..
 
Madikteta wote wanafanana; wawe ni wale ambao ni mtu mmoja mmoja au wawe wa chama kimoja; kufanana kwao kunatabiri vitendo vyao. Hufanana katika mambo makubwa matano:

a. Huamini kuwa wao ndio pekee wenye uwezo wa kutawala (Katika fikra zao hawaamini kama kuna mtu au chama kingine kinachoweza kutawala vizuri kuliko wao). Baadhi yao (kama ni mtu mmoja au chama) hujiaminisha kabisa kuwa ni wateule wa Mungu kutawala nchi zao.

b. Huamini kuwa wanapendwa sana kupita kiasi (hili kuelezea kwanini picha, sanamu, n.k zao huenezwa kila kona ya nchi) Hupenda kuimbiwa nyimbo za kusifiwa na kupeperushiwa maua kila wapitapo kama ishara ya "upendo" huu.

c. Hawako tayari kuamini wanaweza kukataliwa; Mara zote inapotokea mtu anawapinga au kuwakataa hutafutiwa sababu ya kuoneshwa kuwa haiwezekani awakate wao kwani (b) wao wanapendwa sana!

d. Hata siku moja hawajawahi kutengeneza mifumo itakayowaondoa wao wenyewe madarakani. Hivyo, hutumia mbinu zote kufanya mabadiliko ya kimapambo tu ambayo kwa watu wasiofuatilia huweza kuvutiwa kuwa ni mabadiliko. HIvyo aidha hujikuta wanaondoka kwa kukimbia au kwa kukimbizwa na wananchi wao au mataifa ya nje!

e. Wako tayari kufanya jambo lolote kubakia madarakani - msisitizo hapa uko kwenye neno "LOLOTE".

Kutokana na hayo matatu tabia za madikteta wote huweza kutabirika (wawe ni mtu mmoja au chama kimoja). Na ili kuhakikisha hayo matatu madikteta wote duniani (wanaovaa nguo za kiraia na wale wanaovaa nguo za kijeshi).

1. Hutumia vitisho kulazimisha kupendwa na kukubalika - silaha ya dikteta ni vitisho (terror). Wakikukamata watakasumbua sana hadi uogope. Lengo ni kukushawishi uone ni kwanini wao wanastahli kupendwa! Hupenda kujiona kama wazazi wa wananchi - nani atamchukia mzazi wake?

2. Hutengeneza masimulizi ya sifa na kuyalazimisha yaaminiwe hata kama msingi wake ni uongo. Madikteta ni mabingwa wa kuunda (manufacture) uongo. Uwezo wao mkubwa wa kufanya hivi hutokana na ukweli kuwa wao humiliki vyombo vya habari vyenye kufikia watu wengi zaidi (radio, TVs n.k)

3. Inapofikia mahali kuwa upendo wa wananchi unapungua au wanaanza kuwa na mashaka nao madikteta huanza kupoteza watu. Yaani, pole pole watu huanza kukamatwa na kuwekwa "vizuizini" ili wasimpinge sana dikteta.

4. Kisingizio pekee cha madikteta wote (wawe wa mtu mmoja au chama kimoja) kuhalalisha kuwanyanyasa, kuwanyima wananchi uhuru na hata kuwatia watu nguvuni ni "kwa ajili ya nchi". Yaani, hutumia "taifa" kama kisingizio cha wao kuendelea kutawala.

Kwanini?

Kwa sababu madikteta wote wanataka kupendwa na kukubaliwa!

Ole wao wananchi wanaposema "hapana"!!!

Na. M. M. Mwanakijiji (BGM)

Haya yote yamo ndani ya utawala huu. Watetezi huu utawala waje wapangue moja baada ya nyingine.

Ingawa hii iliandikiwa utawala uliopita. Lakini asilimia kubwa yanatendeka sasa na yanaendelea kutendeka.
 
Kuna wachangiaji wengi wanamshangaa Mzee Mwanakijiji (MM) kwa kubadilisha msimamo wake wa kisiasa. Hii ni kwa sababu labda hawafahamu kuwa kwa MM kushiriki katika uandishi wa kiuharakati katika siasa sio suala la kutoa maoni yake bali ni kazi. (Bila shaka maana ya "kazi" inaeleweka!). Wakati wa uchaguzi wa mwaka 2010 MM alikuwa katika timu ya wanamkakati (strategists) wa uchaguzi wa Chadema na mwaka jana akahamia CCM kwa kazi hiyo hiyo! Katika siasa kuhama chama kimoja na kwenda kingine (crossing the floor) ni jambo la kawaida lakini la kutilia shaka (bizarre) kwa sababu huchagizwa zaidi na maslahi binafsi badala ya masuala ya kiitikadi au kisera. Rais Ronald Reagan wa Marekani (1981-89) alisema haya kuhusiana na kazi ya siasa: "Politics is supposed to be the second oldest profession. I have come to realise that it bears a very close resemblance to the first".

And the first oldest profession is what...?!

MMKJition..?
Prostitution...?!
............... ?!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom