Hili jambo ni kongwe mno na linaazia pale kwenye bustani ya Eden ibilisi kupitia nyoka alipomhadaa mwanamke na hatimaye kufanya kinyume na maagizo ya Mungu.Ni tangu pale ndio Madhila ya mwanamke yalianza, kwanza aliambiwa atazaa kwa uchungu hii ni laana ambayo haijawahi kutenguliwa popote. Kisha kwenye Maandiko ya Biblia takatifu kitabu cha methali kuna mstari usemao.
Mwana mpumbavu ni mzigo wa *****. Haishii hapo tu, bali hata katika mahusiano... Ni jambo lisilo la kawaida kukuta mwanamke mmoja kaolewa na wanaume wawili kwa wakati mmoja. Mpaka leo hii kuna jamii za imani fulani zenye misimamo mikali kuhusu wanawake, akikutwa na mimba nje ya ndoa hata kama kabakwa au wakikutwa wawili wanafanya ngono kesi yote humuangukia mwanamke na adhabu yake ni kupigwa mawe mpaka kufa, haya yapo na yanatokea. Tumeshuhudia hata katika maisha haya kuanzia majumbani mwetu, ndugu wa kike tunaishi nao, wafanyakazi wa ndani, mashuleni na hata vyuoni maofisini na hata kupata cheo nk.
Tumeshawahi kusikia degree za chupi, tumeona kwa uwazi kabisa mfumo kandamizi mashuleni, binti anapata mimba bila kutafakari anafukuzwa shule na kupewa majina yote mabaya, huku mtenda akisepa au akipeta mitaani, wengi wameombwa rushwa ya ngono ili wapate upendeleo fulani huko makazini nk. Wengi wamekuwa watumwa wa ngono ili waweze kuishi.
Kwenye mahusiano vipigo na manyanyaso mengine ni vitu vinavyoonekana ni vya kawaida kabisa lakini pamoja na hayo yoote bado wameendelea kutupenda kutujali na kutuhudumia bila vinyongo huku wakiwa ni wepesi wa kusamehe na kuonyesha upendo mkuu namchukulia mwanamke Kama alama ya uwepo wa dunia yenye matumaini furaha na tumaini.Bila wanawake sijui dunia ingekuwaje Mungu aliona mbali sana.