Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

ahsante mkuu ndiyo nahitaji ushauri wa wadau hapa,..

Tafuta muda mchukue mwende sehemu ilipo tulia, kisha anza kumueleza taratibuu vile ww unajisikia juu ya uhusiano wenu
Ongea nae vizuri, kwa upendo pasipo kuonesha lugha chafu au dharau, itamuuma lkn atakuelewa,
 
mkuu mbona kama hujui unachokitaka katika mapenzi?
kwani wewe huitaji kupendwa?Golden chance never come twice ,huyo ndo wife material
 
Iloo! bado unamtaka!!!
Kujishembedua tu! lol!
...
Ebbos! Kwani nitamuambia kama nö umenipa wewe?
Au mi jambazi?
...
Nitajifanya nimekosea namba!
Alah! Wewe haumtaki tupe tunaomtaka ili tumliwaze!
Chezea Mashaxizo weyee!

nipe ya kwako,..
 
we nae ukoje unatongoza kwa kutokupenda vipi wewe? sasa ona unataka kumuumiza binti wa watu tena mwache mapema mtoto wa watu awakubalie wengine wanaomtongoza kuliko kujiaminisha ana mtu kumbe amna mtu.. sawa ....
 
we nae ukoje unatongoza kwa kutokupenda vipi wewe? sasa ona unataka kumuumiza binti wa watu tena mwache mapema mtoto wa watu awakubalie wengine wanaomtongoza kuliko kujiaminisha ana mtu kumbe amna mtu.. sawa ....

ndiyo hivyo nishajikwaa mkuu,..
 
mkuu mbona kama hujui unachokitaka katika mapenzi?
kwani wewe huitaji kupendwa?Golden chance never come twice ,huyo ndo wife material

mwekundu yani unaona amuoe alafu akamtese mtoto wa watu....... mwanaume anapenda ..... ila mwanamke anajifunza kupenda saw,,,,,,,,,,,

shikamoo mwekundu!!!
 
ndiyo hivyo nishajikwaa mkuu,..

sasa fanya maamuzi mapema mwache ...... ili apate mda wa kukubali wengine,.... kwa sababu wewe unamdanganya hadi kumwita mke wangu unamwita .... mtoto wa watu anajua anamume kumbe hana unafanya maigizo...
 
nipe ya kwako,..

Hahahahaaaa! Chakii leo unalo!
...
Sasa nö zangu wewe za nini?
Au wanitaka?
...
Usiseme umpe huyo ke! Sitaki kuunganishiwa! Naunganisha menyewe!
...
Nipe bhana!
 
Hahahahaaaa! Chakii leo unalo!
...
Sasa nö zangu wewe za nini?
Au wanitaka?
...
Usiseme umpe huyo ke! Sitaki kuunganishiwa! Naunganisha menyewe!
...
Nipe bhana!

nipatie ya kwako nimpatie, unahofia nini mkuu,..
 
Iloo! bado unamtaka!!!
Kujishembedua tu! lol!
...
Ebbos! Kwani nitamuambia kama nö umenipa wewe?
Au mi jambazi?
...
Nitajifanya nimekosea namba!
Alah! Wewe haumtaki tupe tunaomtaka ili tumliwaze!
Chezea Mashaxizo weyee!

ati "iloo"...halafu wewe mgomvi
 
unataka kujua ikusaidie nini mkuu,.

Jikite kwenye mada, kama huna cha kuchangia potezea watachangia wengine!!!
Ninayo mengi ya kuchangia, mkuu.. Tatizo langu ni pale mwanafunzi wa MD anapoomba msaada eti ameshindwa kutatua tatizo dogo kama hili. Au wakupeleke kozi ya clinical officer kwanza?
 
mi naona kinachokufanya udai eti hujampenda kutoka moyoni ni hilo suala la kubakwa. Mdogo wangu, kwa kuwa hadi sasa ni kwamba unampotezea muda dada wa watu, na huna mapenzi naye,nadhani hujachelewa sana, muache tu ili usiendelee kumpotezea muda. Mwambie ukweli kwamba HUNA MAPENZI NAYE YA DHATI....ila kumbuka pia what goes around, always comes back around...
 
Ninayo mengi ya kuchangia, mkuu.. Tatizo langu ni pale mwanafunzi wa MD anapoomba msaada eti ameshindwa kutatua tatizo dogo kama hili. Au wakupeleke kozi ya clinical officer kwanza?

maswali yako sijajua yanalenga nini mkuu,..

Ina maana watu tusiombe ushauri humu jamvini kwa sababu zako ulizozisema?

Maswali yako nitayajibu nikiyapatia muda mkuu maana naona unatoka nje ya mada!!!
 
Habari Za Mwanzo Wa Wiki Wana-MMU!!

Ndugu zangu napitia katika wakati mgumu sana katika ulimwengu huu wa mapenzi,..

Takriban miezi nane iliyopita nilikuwa na mahusiano na msichana ambaye tulikuwa tukisoma wote chuo kimoja Jijini Dar,.

Huyu msichana katika mahusiano yetu hatujawahi kushiriki mapenzi kwa muda niliokaa naye kutokana na yeye kunizungusha na kunipiga mizinga ya hapa na pale ukizingatia sisi wote tulikuwa ni wanafunzi hivyo hali ya kiuchumi isingeruhusu mimi kumtimizia mahitaji yake yote hivyo nikaamua kuachana naye,.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati naelekea nyumbani nikiwa katika daladala nikakutana na rafiki wa yule msichana wangu wa zamani ambapo nilifanya naye mazungumzo kidogo maana sijawahi kupata wasaha wa kuwa naye karibu kwa kuhofia kuharibu mahusiano yangu na ya rafiki yake niliyemwacha,.

Mazungumzo yetu yalikuwa ya kufahamiana tu na pia nilifanikiwa kuchukua namba zake za simu na kumlipia nauli tukaahidiana kukutana siku iliyofuata chuoni,.


Wakati huo tulikuwa katika kipindi cha mitihani hivyo tuliamua kupeana muda kwanza wa maandalizi ya kumalizia mitihani ya muhula,.

Baada ya kumaliza mitihani tulipata wasaa zaidi wa kukaa pamoja na kujuana pia kusomana tabia za kila mmoja wetu,..

Katika kipindi cha kusomana tabia huyu msichana aliniuliza swali hili '' Je ushawahi kuwa na mpenzi kabla??'' mimi nilimjibu hapana lakini baadae alikuja kuniuliza mbona rafiki yake alimwambia kwamba mimi nilishamtongoza? Mimi nikamjibu kwamba hapana yule alikuwa rafiki tu sema kaamua kunichafulia tu kwako,.

Huyu msichana alikubaliana na mimi na kumpuuzia yule rafiki yake,.

Katika kipindi cha kuendelea kufahamiana na huyu binti alinismulia kwamba akiwa mdogo alibakwa ingawa mama yake alimuwahisha hospitalini ili apewe kinga endapo aliyembaka alikuwa na maambukizi ili asipate, hali yake ya afya ni njema na alishapima UKIMWI mara kadhaa yupo salama,.

Kwa kipindi kifupi nilichokaa na huyu msichana nimebaini siyo mtu wa makuu na anajali sana tofauti na yule wa mwanzo,.

TATIZO

1.Nimekuja kugundua kwamba huyu msichana niliye nae sasa sikumpenda kutoka moyoni ila ilitokea tu kuwa naye baada ya kukorofishana na rafiki yake niliyekuwa naye mwanzo,.

2.Huyu msichana inaelekea ananipenda kuliko ninavyompenda mimi na kabla sijawa nae ailiniambia kwamba alinipenda kabla hata ya mimi kukutana nae,.

3.Huyu msichana katika mazungumzo yetu tumekuwa tukizungumzia masuala ya kujenga familia siku zijazo,..


Wakuu naombeni mnisaidie ni njia gani sahihi niyaitumia kumuacha huyu msichana bila kumuumiza maana sitaki kumuumiza hata kidogo na mimi sipo tiyari kuwa naye tena!!!

Hebu waza tena na ufikiri usije kuja tena kuomba ushauri wa kurudiana nae.......
 
Back
Top Bottom