Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

Madhara Ya Mapenzi Ya Aina Hii,.

Habari Za Mwanzo Wa Wiki Wana-MMU!!

Ndugu zangu napitia katika wakati mgumu sana katika ulimwengu huu wa mapenzi,..

Takriban miezi nane iliyopita nilikuwa na mahusiano na msichana ambaye tulikuwa tukisoma wote chuo kimoja Jijini Dar,.

Huyu msichana katika mahusiano yetu hatujawahi kushiriki mapenzi kwa muda niliokaa naye kutokana na yeye kunizungusha na kunipiga mizinga ya hapa na pale ukizingatia sisi wote tulikuwa ni wanafunzi hivyo hali ya kiuchumi isingeruhusu mimi kumtimizia mahitaji yake yote hivyo nikaamua kuachana naye,.

Baada ya mwezi mmoja kupita wakati naelekea nyumbani nikiwa katika daladala nikakutana na rafiki wa yule msichana wangu wa zamani ambapo nilifanya naye mazungumzo kidogo maana sijawahi kupata wasaha wa kuwa naye karibu kwa kuhofia kuharibu mahusiano yangu na ya rafiki yake niliyemwacha,.

Mazungumzo yetu yalikuwa ya kufahamiana tu na pia nilifanikiwa kuchukua namba zake za simu na kumlipia nauli tukaahidiana kukutana siku iliyofuata chuoni,.

Wakati huo tulikuwa katika kipindi cha mitihani hivyo tuliamua kupeana muda kwanza wa maandalizi ya kumalizia mitihani ya muhula,.

Baada ya kumaliza mitihani tulipata wasaa zaidi wa kukaa pamoja na kujuana pia kusomana tabia za kila mmoja wetu,..

Katika kipindi cha kusomana tabia huyu msichana aliniuliza swali hili '' Je ushawahi kuwa na mpenzi kabla??'' mimi nilimjibu hapana lakini baadae alikuja kuniuliza mbona rafiki yake alimwambia kwamba mimi nilishamtongoza? Mimi nikamjibu kwamba hapana yule alikuwa rafiki tu sema kaamua kunichafulia tu kwako,.

Huyu msichana alikubaliana na mimi na kumpuuzia yule rafiki yake,.

Katika kipindi cha kuendelea kufahamiana na huyu binti alinismulia kwamba akiwa mdogo alibakwa ingawa mama yake alimuwahisha hospitalini ili apewe kinga endapo aliyembaka alikuwa na maambukizi ili asipate, hali yake ya afya ni njema na alishapima UKIMWI mara kadhaa yupo salama,.

Kwa kipindi kifupi nilichokaa na huyu msichana nimebaini siyo mtu wa makuu na anajali sana tofauti na yule wa mwanzo,.

TATIZO

1.Nimekuja kugundua kwamba huyu msichana niliye nae sasa sikumpenda kutoka moyoni ila ilitokea tu kuwa naye baada ya kukorofishana na rafiki yake niliyekuwa naye mwanzo,.

2.Huyu msichana inaelekea ananipenda kuliko ninavyompenda mimi na kabla sijawa nae ailiniambia kwamba alinipenda kabla hata ya mimi kukutana nae,.

3.Huyu msichana katika mazungumzo yetu tumekuwa tukizungumzia masuala ya kujenga familia siku zijazo,..

Wakuu naombeni mnisaidie ni njia gani sahihi niyaitumia kumuacha huyu msichana bila kumuumiza maana sitaki kumuumiza hata kidogo na mimi sipo tiyari kuwa naye tena!!!
Aisee chalii hizo akili zako umekopa? Wewe ulivyomtongoza huyu dada ulikuwa unategemea nini? Napenda nikuhakikishie kwamba wewe huo mchezo unaotaka kuufanya utakugharimu alafu baadae uje hapa uanze kutuambia una majeraha moyoni na yana plasta. Tulizana na acha mambo ya kizamani.
 
kwa nini umuache anayekupenda? me naamini unampenda na ndiyo maana upo naye, tulia hapo itakula kwako
 
kumbe unasoma MD ndo zenu hamjielewagi
kabisa mnataka nn,kafie mbali
 
Tayari umeshamvuta kihisia kwa ukaribu na story mlizopiga, umeharibu kwa hapo, ila sikushauri uoe mtu ambaye humpendi, unachotakiwa kufanya nikutomuweka karibu kihisia mtu ambaye humpendi.

Hata mimi ilinitokea msichana alinipenda mno kwa ishara zote na maneno ila mimi sikuitikia kabisa hisia zake akaamua kuacha kujikomba kwangu
 
ahsante kwa ushauri mkuu,..
 
Kijana! Mpende akupendaye,asiyekupenda achana naye! Unataka mwanamke gani zaidi ya huyu? Na kama hukuwa na mpango wa kuishi naye kama mkeo, ni bora usimuharibie maisha yake binti huyo makini.Waachie waoaji wajipatie mke mwema.Wewe ukapambane na vicheche!
 
Naona bado haujajua maana ya tatizo.

Sent from my BlackBerry 9780 using JamiiForums
 
Kijana! Mpende akupendaye,asiyekupenda achana naye! Unataka mwanamke gani zaidi ya huyu? Na kama hukuwa na mpango wa kuishi naye kama mkeo, ni bora usimuharibie maisha yake binti huyo makini.Waachie waoaji wajipatie mke mwema.Wewe ukapambane na vicheche!

nashukuru kwa ushauri mkuu,.

Tatizo moyo haujapenda,.
 
nashukuru kwa ushauri mkuu,.

Tatizo moyo haujapenda,.
Kama ni moyo wako huo huo ndio umejiridhisha juu ya tabia hizo njema za huyo mdada ulizozionesha, basi tatizo ni wewe kukataa kupokea maamuzi ya moyo wako.MAUNGU AKUSAIDIA ON HOW TO OVERCOME THAT CHALLENGE! Obey your heart desire!
 
sawa mkuu, mkuu ila umejikita zaidi kunilaumu badala ya kushauri!!
 
acha uboya,usipoteze hyo fursa,watu wanatafta sana fursa za namna hyo,unataka uendelee kupata kama yule wa kwanza sio?we unaonekana bado unampenda yule wa kwanza ambae hakupend,pia bado unajipa matumain kua utarudiana nae,haya bwana,kuna mtu kakwambia mkataa pema...
 
Back
Top Bottom