Madhara ya kurithi/kupewa MAJINA YA MABABU/MABIBI!

Madhara ya kurithi/kupewa MAJINA YA MABABU/MABIBI!

jnrs;Marwa mwita chacha rhobi MUSOMA BILA SHAKA, ngoja nikuongezee, wegesa,mairo,khitentani nk! Ila wakuu nijuzeni basi faida na hasara?
 
Mara nyingi inatokea kwa mfano bibi alikuwa na tabia fulani nzuri au mbaya au hata babu yule mtoto utakayempa jina linalofanana na hao watu lazima atarithi zile tabia za yule mwenye jina mimi nina ndugu zangu wengi wamepewa jina la mtu fulani kwenye ukoo wetu basi wale wote waliopewa lile jina ni wakorofi mno yaan ni wagomvi sana kufuatilia historia ya mwenye jina na yeye unaambiwa alikuwa mkorofi sana

Unachosema mdau ni cha kweli kabisa, sasa nini kifanyike? au tupewe tu majina ya kawaida haya ya (wazungu)?

Kwani hao wazungu hawakuwa na tabia mbaya? Au kwa vile hujui story zao?
Ndio maana wakatoliki wanapendekeza majina ya watakatifu na sio ya wazungu. Mfano Kizito (shahidi wa Uganda) au Fransisco wa Sales etc.

So kama kuna babu au bibi alikuwa na maadili, tabia nzuri na mcha Mungu mpe jina mwanao.
 
kupewa majina yasiyo ya asili ni mkakati uliofanywa makusudi na nchi za magharibi dhidi ya watu walio kua wana watawala ukidadisi kwenye vitabu vya historia uta gundua hili mfano ireland, walipinga hili kwa nguvu zao zote, mm sioni sabau ya kumpa mtoto jina la wazungu ndio maana wana rithi tabia za kishoga na usagaji, nasema hivyo sababu kuna mchangiaji mmoja amesema ya kua wata rithi tabia mbaya, ona mfano wa mataifa ya africa ambayo yana wasomi wanaojiatambua na kutaka kutunza asili yao huwezi kuona majina ya kizungu kwa watoto wao
 
Wana JF,

Kuna kasumba ya wazazi kuwapa watoto wanaowazaa majina ya (kiukoo) aidha ya babu ama bibi, ukiachilia mbali majina yetu haya ya kawaida kwa maana majina ya wakristo, kwa walio wakristo, na waislam, kwa walio waislam.

Sasa swali langu ni kwamba: Yapi madhara ya kumpa jina mtoto, mwanao, jina la ukoo?

Maana nilishaskia (some story) huyu mtoto ana tabia kama babu yake, au mlevi, mcheshi, kama bibi yake.

Karibuni tulijadili hili swala wana JF!
Na wewe unapotumia jina ambalo si lako kwenye JF je lina madhara gani?
 
majina kama haya ni hatari, Mjaliwa ,Masumbuko Matatizo, Shida ,Tabu Majuto
 
SiKutishi
KUNA MIMBA ZINGINE.ZIMETUNGWA BAR MKUU SIRI ANAJUANMAMA SASA UKIMPA JINALAMAMA US ISHANGAE AKARITHI

WAPO WALIOPEWA MAJINA YA MAMA AMA BIBI SIKUTISHI BIBI AKAACHIKA MWANAE YAANI MAMA AKAACHIKAPAKA LEI WAJUKUU WENGINR WAMEOGOPA KABISA KUOA AMA KUOLEWA SABABUBU YA JINA.

Yaleyaleee! sikio la kufaa.....!!!
 
sikutishi
kuna mimba zingine.zimetungwa bar mkuu siri anajuanmama sasa ukimpa jinalamama us ishangae akarithi

wapo waliopewa majina ya mama ama bibi sikutishi bibi akaachika mwanae yaani mama akaachikapaka lei wajukuu wenginr wameogopa kabisa kuoa ama kuolewa sababubu ya jina.

we jamaa post zako huwa ngumu sana kuzisoma...utakuwa mkimbizi au hujui kuandika vizuri tu
 
Compare humphrey shitman alfred mothershed. na jina kama Otieno Okoth Ongola Oyoo lipi lenye ladha
 
we jamaa post zako huwa ngumu sana kuzisoma...utakuwa mkimbizi au hujui kuandika vizuri tu

Huyu atakuwa mchina kaoa mbongo yaani hata mi sikuelewa kabisa kaandika nn nafikiri nae mwanae atamtolea CHING LEE POMBE
 
Mbona wataalam wa kuiga majina ya wazungu hamuigi ya wachina ? au hata wahindi ?
tuone Chong Jin Kund.
Jivunie chako uheshimike
 
Huo ndo uafrika halisi bwana..mtu anaitwa Andendekisye Gwalugano Ambonisye Mwaipopo..mtu mmoja huyo!
 
Acheni utmwa wa kifikra, majina ya asili tunayo ya kutosha badala yake mnaita watoto wenu majina yaliyokuja na meli mwisho wake hata nyinyi wenyewe mnashindwa kuyaandika ama kuyatamka sawasawa, hivi tukijiita Mwanamtwa, Mkombozi, Mwaiposa, Chacha, Urio, Rweyongeza, Shemahonge, Malima, Simbachawene, Mwanakulya, Mapesa, Kikwete, Mkapa, Nyerere, Membe, Magufuli......hadi raha kuyatamka majina yenye fleva ya kiafrika.
Hahahhahaaaaaa Ngozi Nyeusiiiiiiiii........Jina Jeupeeeeeeeeee, Wabongo bana, embu cheki Nigeria huko
 
Back
Top Bottom