Madhara ya kurithi/kupewa MAJINA YA MABABU/MABIBI!

Madhara ya kurithi/kupewa MAJINA YA MABABU/MABIBI!

Nimeguswa na huu Uzi. Kupeana majina ya kizungu ni kutukuza ukoloni na kujiona wastaarab yani assimilation system ni Sawa na kuiga mitindo yao mingine ya maisha kama enzi hizo kuchana nywele na kuacha way. Ndio sababu watu hujichubua au ushoga. Tue kama wakenya, waganda, Nigeria na SA.
 
Ndo maana vitabu vitakatifu vya kizungu tukaitwa uzao wa hamu(tumelaaniwa). Pale bukoba kuna mzee mmoja mtangangazaji anaitwa anasi(anus) jina la mshahara bila shaka kabatizwa na wazazi wake. Waliona matamshi yamekaa njema. Hapo mlalakuwa kuna jamaa angu anaitwa Hussein wakati kwenye mila za kiarabu ni jina la mtoto pacha yaani Dotto lakn wazazi wakaona imekaa njema... nasema hivi kenge kufanana na mamba haimaanishi kawa mamba...

Waafrika wengi wetu nina wasiwasi na utimilifu wa ubinadamu wetu. Tunajikana kila idara ya maisha yetu ya kila siku. Utashangaa hata wasomi wenye ma-phd yao linapokuja suala la imani,mila na desturi unauona udhaifu wao wa kuhoji au kuidadisi jamii inayowazunguka juu ya imani potofu zilizoletwa na mashua za white-pipo.

Ukiwa na nyuzi za kufikirisha ubongo kama akina KIRANGA unaonekana kama chizi.
Yapo mambo kibao ya kuiga kutoka kwa wenzetu hususana SAYANSI NA TEKNOLOJIA lakin sio mila na desturi zitutambulishazo sisi kama waafrika.

Hivi ukiitwa hayo majina nani atajua unatoka wapi?
Lakini ukiitwa rumanyika, manka, ngosha, mwakyembe, marwa...nk haiitaji maelezo yyte kwani jina linajieleza lenyewe.

Wazazi wangu watanisamehe kwa kulikana jina langu la KIARABU mbele ya mahakama ili niuvae UAFRIKA wangu mbele za walimwengu.

MUNGU habadiliki wakati wote na mahala popote. Huitaji lugha wala jina la jirani kuwasiliana naye.

Ndiyo maana hatuna baraka zake na tumeshindwa kuendelea.

Tafakari, chukua hatua.
 
Back
Top Bottom