SoC02 Madhara ya kupenda kupita kiasi katika mahusiano

Stories of Change - 2022 Competition

Hosea Ben

Member
Sep 22, 2014
69
15
Mauaji mengi ambayo yanatokea katika jamii zetu yanatokana na wivu wa mapenzi; na wivu wa mapenzi unaweza kusababishwa na kutokuaminiana katika mahusiano au usaliti miongoni mwa wapenzi au wanandoa.

Ni nini maana ya Kupenda katika mahusiano ya kimapenzi au ndoa?
kumpenda mtu maana yake ni kuheshimu mipaka yake; kupenda kupita kiasi kunamaanisha kuwa unaondoa mipaka hiyo na kuacha kujijali mwenyewe, na unafanya kila kitu kwa mwenzi wako ili kumfurahisha.

Tuangalie baadhi ya madhara ambayo yanaweza kusababishwa na kumpenda mwenza wako kupita kiasi; fuatana nami katika makala hii:-

Moja, unaweza kuharibu utu wako na kuweka mapenzi yako kuwa hatarini. Hii inatokana na wivu uliopitiliza miongoni mwa wapenzi.

Pili, kumpenda mwenza wako kupita kiasi kunaweza kumfanya mwenzi wako asifurahie mahusiano yenu maana unamnyima uhuru na nafasi ya kuonyesha upendo kwako, unamnyima muda wa kujifunza nini afanye ili kudumisha mahusiano yenu. Na hii inamfanya mpenzi wako akuchukulie wa kawaida sana na asione upekee ulionao kwake.

Tatu, kukuza utegemezi usiofaa. Unapopenda kupita kiasi kunaweza kumfanya mpenzi wako awe na utegemezi mkubwa sana kwako, kunaweza kutengeneza maamuzi tegemezi yaani kunaondoa kujisimamia na kuweka utegemezi kwa mwenza wako. Na hii inaweza kusababisha kufanya maamzi ya kujidhuru au kumdhuru mwenza wako endapo mahusiano yatavunjika.

Nne, hupunguza muda na kupoteza muda wa kujikita kwenye malengo ya maisha ambayo umejiwekea maana muda mwingi unawekeza kwa mwenza wako ili kumfurahisha na kuhasahau kijikita na malengo yako.

Unapomfanya mwenza wako kuwa kitovu cha ulimwengu wako, huwa unapuuza kila kitu ambacho kilikuwa kinakufurahisha. kwa mfano, unapojikita zaidi katika mahusiano yako ya kimapenzi, huwa unapuuza mambo unayopenda, na hata kupoteza marafiki na kupoteza mahusiano ya kifamilia kwani utakuwa umewekeza zaidi kwenye uhusiano na mwenza wako.

Njia muhimi ambazo zinaweza kumfanya mtu asiwe tegemezi wa kupenda kupita kiasi katika mahusiano.
Kwanza, Tambua mahitaji ya uhusiano wenu na uweke mipaka fulani; inafaa kufikiria kila wakati juu ya wapi hamu hii ya "kupenda kupita kiasi" inatoka. kuweka mipaka itasaidia katika kuboresha upendo wako na kujistahi.

Pili, Acha kupatikana kila mara yaani unatakiwa uwe na majukumu ambayo yanakubana ili kupunguza utegemezi wa kupenda kupita kiasi, hii itakufanya kutomruhusu mwenzi wako atawale hisia zako.

Tatu, Pata muda wa kupumzika na ujifunze kufurahia ukiwa peke yako. Hapa unaweza kuwa na muda wa kufanya tathmini ya mwenendo wa utekelezaji wa malengo yako katika maisha ambayo unatakiwa kuyatimiza.

Nne, Jifunze kumwamini mpenzi wako; ikiwa unaona vigumu kumwamini mpenzi wako, utajenga mazingira na taswira ya kusalitiwa na kufanya moyo wako ukose utulivu. Matatizo mengi katika mahusiano hutokea kutokana na kutoaminiana.

Mwisho, kama jamii zetu zitazingatia na kuweka mbele uaminifu na kuwa na upendo usio kuwa na mashaka katika mahusiano basi mahusiano mengi yasingekuwa yanaishia katika kuleta mauti yanayotokana na wivu wa kimapenzi na kusalitiana.
 
Kuna kiazi kimeleta uzi leo ana watoto 4 na amekolea kuchepuka na kijana. Huyu unafikiri mumewe akijua amfanye nini??😂
 
Back
Top Bottom