Dalili 5 za mahusiano yasiyo na furaha

Peter Mwaihola

JF-Expert Member
Jun 23, 2022
227
333
Mambo vipi mdau wangu wa nguvu, nakushukuru kwa kutenga muda wako na kuwa msomaji mzuri wa makala zangu twende sawa usisahau kufollo ukurasa huu.

Leo tuangazie dalili ambazo huwa zinajitokeza pale ambapo uhusiano kati ya wenza iwe mume na mke au wapenzi unapokosa furaha au kuelekea kuvunjika kabisa.

Dalili ya kwanza ni kupungua kwa mawasiliano, hapa mwenza hupunguza mazungumzo kuhusu maisha ya uhusiano na mazungumzo mengine ya muhimu kuhusu hatma ya uhusiano husika.

Kukosekana kwa urafiki wa karibu ni dalili nyingine ya mahusiano yasiyo na furaha, dalili hii huambatana na tabia kadhaa ikiwemo kutoweka kwa vitendo vyenye kuashiria upendo na urafiki mfano busu, kukumbatiana na vitendo vingine vya kihisia.

Uhusiano usio na furaha haukosi mabishano na taharuki ambavyo kwa pamoja huzua migogoro isiyoisha ikiashiria kutokuridhika na mawasiliano mabovu baina ya wahusika.

Kukosa hisia, hali hii inaweza kuambatana na vitendo kama kunyimwa unyumba na kutokujali hisia za mwingine ambapo mmoja wapo huwa mbali kihisia havutiwi tena na mwenza wake.

Dalili ya tano ni kupungua kwa juhudi za kupenda na kuonyesha upendo baina ya wenza, dalili hii huambatana na mambo kadhaa ikiwemo majuto, kukosekana kwa mipango ya maisha yajayo na kadhalika.

Peter Mwaihola
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom