Madhara ya kufanya mapenzi na wanawake/wanaume wengi

Madhara ya kufanya mapenzi na wanawake/wanaume wengi

Kwa wanaoruhusiwa kuoa wanawake 4 unasemaje kwa hao? Hayo madhara yanawapata pia?
 
nan kasema hamna kitu kama ocho kuna malaya wanajiuza na maisha yao mazur na wanaaman na furaha hayo magonjwa yapo tuuu usipokufa na ukimwi utakufa kwa kansa na kansa ikikuepuka utapata ajali usitutishe matusi yanaruhusiwa kupunguza hasira achaa tuhangaike kila mtu anahatima yakeee
Tulia bibie acha jazba muombe Mungu akusaidie utoke kwenye hayo maisha machafu...

matusi hayatafuta nilichoandika wala hayahalalishi uzinzi ..jitafakari
 
Pointi namba moja ya kuambukizwa "roho" linahitaji ufafanuzi. Ni dhana mpya ninayoisikia sana siku hizi ambayo naiona so fanatic na unfound. Japo nakubaliana na madhara mengine. Mtoa mada ukiieleza nitakushukuru
 
Hosea(aliyekuwa nabii wa Mungu) aliambiwa akaoe mwanamke kahaba. Sasa huyo mwanamke alikuwa amelala na wanaume wangapi kama kazi yake ni kahaba? Na si ingekuwa miroho ya shetani inatransfer kwenda kwa mtu mwingine, Mungu angemwamuru mtumishi wake kuoa kahaba?
 
Wapendwa ktk Bwana habari za shughuli!

Nimeona vyema nishirikiane nanyi ubaya wa kufanya mapenzi na wanaume au wanawake wengi.

Awali ya yote nitoe maelezo kidogo then niendelee na madhara...naomba ifahamike sijamlenga mtu yoyote kama mtu binafsi Bali nalenga kufumbua macho yetu sote juu ya kile tukifanyacho tukidhani ni ujanja au kufaidi dunia.

Kufanya mapenzi kunahusisha mwili, nafsi ,na ufahamu wote..nisema kunahusisha mwili mzima.

Nikisema nafsi nina maana ya roho, mwanadamu ameumbwa kwa mfano wa Mungu, hivyo ana roho na mwili...lkn ndani ya moyo wa mwanadam kama hakuna roho wa Mungu kuna roho za shetani...

Unapofanya mapenzi na wanawake wengi au wanaume wengi upo kwenye hatari ya kukumbana na haya yafuatayo;

1.Unajivika miroho ya shetani ya kila aina....ndiyo..ngoja nikupe mfano..
Ukilala na mwanaume au mwanamke mwenye roho ya uzinzi maana yake anakuambukiza ile roho...

2.Unaharibu mahusiano yako na Mungu.

3.Unaharibu mahusiano yako na mwenza wako.

4.Unajiondolea uaminifu.

5.Thamani yako inapungua.

6.Unajizeesha kabla ya wakati wako.

7. Unaongeza idadi ya watoto wa mitaani.

8.unajiweka kwenye hatari ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa ikiwepo ukimwi.

9.unajiingiza kwenye mitego ya kufumaniwa.

10.kwa wanaume unajiingiza kwenye wimbi la umasikini.

11.Unajivika mikosi na mabalaaa.

Hayo ni baadhi ya madhara ya kuwa na idadi kubwa ya wanawake/wanaume.

Tulia na mwanamke/mwanaume mmoja ndoa ni baradiso.

HAKUNA JAMBO JIPYA CHINI YA JUA
No. 8 ni kweli ila yaliyobaki yote ni ya kusadikika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
wanawake wanafilisi asikwambie mtu!mtu unakuta analisha mke na watoto makande huku kwa dem anapeleka kuku na madikodiko ya kila aina!hapo lazma laana ikuandame na ufilisike na dem akukimbie urudi kuomba msamaha kwa mkeo eti upepo mchafu ulikufikia!mazafanta wewe

my game,my rules
 
Uasherati ni dhambi inayofanyika ndani ya mwili wa binadamu, inakuunganisha na mtu mwingine ndo maana tunabeba miroho mingine ambayo hatukuwa nayo.... Ukiiweza kudumu na mmoja hakika utaziona baraka katika maisha yako....

Asante Mtumishi kwa kutukumbusha
 
nan kasema hamna kitu kama ocho kuna malaya wanajiuza na maisha yao mazur na wanaaman na furaha hayo magonjwa yapo tuuu usipokufa na ukimwi utakufa kwa kansa na kansa ikikuepuka utapata ajali usitutishe matusi yanaruhusiwa kupunguza hasira achaa tuhangaike kila mtu anahatima yakeee
Binti umejuaje hao wanaojiuza wana maisha mazuri? usipende kutazama muonekano wa nje wengi wanateketea nafsini mwao kimyakimya.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom