Madereva wa wabunge walia njaa!

Madereva wa wabunge walia njaa!

SirBonge

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2010
Posts
378
Reaction score
436
Huku waheshimiwa wabunge wakiwa wanalipwa sio chini ya 6,000,000/- kwa mwezi na kukiwa na habari za ongezeko la fedha hiyo mpaka 10,000,000/-, madereva wanaowaendesha waheshimiwa hawa wamelalamika kwamba wanapunjwa posho zao na hawana mikataba ya kazi. Kuna wengine wanapewa mpaka 50,000/- kwa wiki nzima....

My take: Enyi waheshimiwa mbona mnakuwa na roho mbaya hivyo?? wafanyakazi wengine mnawabania hata madereva wenu pia???

Source: Michuzi blog (na picha zipo)
 
WAKATI wananchi wengi, wakikabiliwa na ugumu wa maisha, madereva wa wabunge nao wameibua kilio chao wakilalamikia ukali wa maisha. Madereva hao, walilazimika kumwandikia barua Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila wakilalamikia haki zao kukaliwa na wabunge. MTANZANIA imefanikiwa kunasa barua hiyo ya Julai, 2012 ambayo imesainiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva wa Wabunge, Juvenille Joseph.

Pamoja na mambo mengine, barua hiyo inaishutumu Ofisi ya Bunge kushindwa kusimamia maslahi yao, hali inayowafanya waishi kwa shida.

Katika barua hiyo, madereva hao walilamikia suala la ukosefu wa mikataba ya kazi, huku wakitaka posho na mishahara yao itenganishwe kutoka katika akaunti za wabunge.

"Mheshimiwa Katibu wa Bunge, sisi ni madereva wa waheshimiwa wabunge, tunaleta kwako hoja zetu ili ziweze kupatiwa ufumbuzi wa kina katika ofisi yako.

"Kwa kipindi chote, madereva wa wabunge hatukuwa na mikataba ya ajira zaidi ya makubaliano ya mdomo baina ya dereva na mbunge.

"Ndiyo maana kunakuwa na unyanyasaji mkubwa kwa baadhi ya waheshimiwa wabunge dhidi ya madereva wao.

"Tunaomba ofisi yako izingatie kuwa kazi ya ubunge ni ya kipindi cha miaka mitano, bila mkataba ni vigumu kujua suala la haki za kikazi.

"Hivyo basi, tunaomba ofisi yako isimamie kuhakikisha kuwa wabunge wote wanatoa mikataba ya ajira kwa madereva wao," ilisema sehemu ya barua hiyo.

Madereva hao, walisema wamekuwa wakilipwa fedha kidogo na wabunge na wengine kudhulumiwa kabisa, licha ya kuwapo waraka unaoelekeza malipo halisi.

Waraka huo, wenye namba FA.155/206/01/70 wa Novemba, 2008 unaelekeza dereva anatakiwa kulipwa Sh 470,000 kwa mwezi, ikiwa ni mshahara na posho ya siku 10 mbunge akiwa jimboni.

Madereva hao, wamehoji sababu ya Ofisi ya Bunge kuingiza mshahara na posho zao katika akaunti za wabunge na kueleza kuwa huo ni mwanya mojawapo wa manyanyaso.

"Pamoja na maelekezo mazuri ya ofisi yako, lakini wabunge wengi hawalipi mshahara na posho za madereva wao kama waraka unavyoelekeza.

"Kwa msingi huo, tunaomba ofisi yako ichukue jukumu la kuziondoa fedha zote zinazomhusu dereva katika akaunti ya mbunge na kuzipeleka katika akaunti za dereva wa mbunge.

"Hii itapunguza malalamiko yaliyopo na yanayoendelea, kwani kwa sasa mbunge anaona kama anafanya hisani kumlipa dereva, kwa kuwa fedha anatoa kwenye akaunti yake," ilisema barua hiyo.

Madereva hao, pia walilalamikia suala la Ofisi ya Bunge kushindwa kuwatengea mafao na kusema kuwa hali hiyo inawafanya madereva wengi wa wabunge, kukosa mwelekeo wa maisha ya uzeeni.

Akizungumza na MTANZANIA kwa uchungu, mmoja wa madereva wa wabunge ambaye hakutaka jina lake litajwe, alishangaa kuona hadi sasa ofisi ya Bunge imekaa kimya juu la malalamiko yao.

"Kilio chetu hiki kilianza tangu 2007, lakini hakuna juhudi zozote zilizofanywa kubadili hali ya maisha yetu kama madereva wa wabunge.

"Barua yetu kwenda ofisi ya Bunge, tuliipeleka tangu Julai, 2012 hadi leo Katibu wa Bunge hajatujibu hoja zetu.

"Sisi tunashindwa kuelewa kwanini wabunge wanashindwa kuzungumzia na kutetea maslahi yetu, wakati wao wanajiita ni watetezi wa wananchi.

"Waraka huu wa malipo kila mbunge alipewa, lakini wanachofanya hawa jamaa kila wanapopata waraka unaohusu stahili za madereva, wanachana ili kupoteza ushahidi waendelee kutulipa jinsi wanavyotaka wao," alisema.

MTANZANIA ilifanya jitihada za kumtafuta Katibu wa Bunge, Dk. Thomas Kashilila ili aweze kuzungumzia malalamiko hayo, lakini hazikufanikiwa baada ya simu yake ya kiganjani kuita muda mwingi bila kupokewa.

Hata hivyo Ofisa Habari wa Bunge, Owen Mwandumbya alisema: "Siwezi kuzungumza chochote juu ya suala hilo, kwa kuwa hilo ni suala la Katibu wa Bunge.

"Hata hivyo siwezi kujua barua hiyo kama ilimfikia mwenyewe au laa, hilo ni suala lake mwenyewe muulize yeye atakuwa na majibu, mimi sijui lolote kuhusu malalamiko ya madereva wa wabunge," alisema.

Kwa upande wake, Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA), alisema hajui kama kuna kitu kinachoitwa chama cha madereva wa wabunge.

CHANZO:MTANZANIA LA TAREHE 11/03/2013.
 
Hawa wabumge ni wabinafsi sana.mi nashauri madereva wawe wanaajiriwa na bunge kwa mkataba wa kudumu ili miaka mitano ikiisha asubiri uchaguzi na kupewa mbunge mpya.
 
Wabunge,kwa hili hamkwepi lawama!

Msito majibu mepesi kwa maswali magumu!
 
Ukweli ulio wazi huu ni uhuni wa Bunge
kwanini mishahara yao isilipwe Benki
pia wamelalamika sana hawasikilizwi.

Mbunge kwa kifupi ni wabadhirifu sana wa pesa za Umma,wanalipwa pesa za kuwalipa Sekretari,Dereva, n.k lkn ni nani asiyejua kuwa ofisi nyingi za Wabunge ni vumbi tu.

Maana hakuna chochote zaidi ya ujanja ujanja
yaani hao Madereva wako nao muda na wana njaa ila wanafumba macho kama hawaoni.
 
Mimi hapa mbunge wangu prof. Maghembe kaajiri aliyekuwa mhudumu wa ofisi kuwa ndiye katibu wa mbunge. Wakati taratibu zinasema katibu wa mbunge anatakiwa awe msomi ngazi ya digrii. Kwa sababu katibu wa mbunge ndie anayetekeleza kazi za mbunge kama hayupo jimboni. Huyu tulie naye hapa ni balaa tupu kwani yeye hukusanya umbea tu na kumpelekea mbunge. Yote hii ni ili amlipe mshahara wa 40,000/- tu kwa mwezi. Dereva ni wa wizara ya miundombinu.
 
hata mimi siungi mkono mshahara wa mtu mwingine kupitishwa kwa mtu mwingine, ni mkandamizo
 
Hapo sasa ndipo Ugumu wa huo unaoitwa Ukombozi wa pili wa Mtanzania ulipo, Halafu wanashangaa kwa nini Dar watu hawaendi kwenye maandamano yao!
mbona ujielewi wewe..... jibu CCM au CDM basi, wewe unaleta mambo ya maandamano.
 
Back
Top Bottom