Madereva wa Mwendokasi hawana nidhamu

Inawezekana tatizo lipo kwny mfumo wa Ajira wa kupata hao madereva.

Mifumo ya Ajira imebuniwa na kwa kusimamiwa kwa namna gani kupata Madereva wenye sifa.

Mie binafsi siamini kama Dereva asie na 'Mkubwa' akawa anajua ana kijiji kinamtegemea anaweza akafanya ujinga wanaofanya wale Madereva

anaweza akakuta kituo kinejaa abiria nae akapita bila ya kusimama huku gari ikiwa tupu na nyakati zingine anasimama kupandisha abiria ikiwa hakuna nafasi kabisa na hakuna mfumo wowote wa kufuatilia na kudhibiti uholela huu wa Mwendokasi
 
Sitetei madereva wa mwendokasi ila hawa boda ni Wapuuzi Sana. Ukiangalia ile video ya kisutu kwakweli hata kama sio tu junction ya mwendokasi ule sio mwendo kwa mjini-kati.

Hao wanaodai kuwekwa traffic lights nao ni wapuuzi wengine wasio na akili. Traffic lights ngapi ziko mjini na bado boda hawazifuati?

Tena bora hata barabara isiyo na traffic lights kidogo afadhali kwenye traffic lights ndo wanakuwa wehu. Atakayebisha aende ubungo, tazara akajionee maajabu.

Kila mtu afuate sheria full stop sio mara matuta mara taa za trafiki kila eneo.

Usiku huu tu kwenye saa 1 hapo shekilango gari zimesimama kupisha raia kuvuka katika zebra boda katoka huko honii kama zote nusu agonge watu wakiwemo watoto.
Hakuna wa kuchukua hatua ila ipo kuna jambo litatokea nchi itasimama kwa huu ujinga WA boda.
 
kuna dereva mmoja mzee wa kudeshi.

anafanya kama anasimama mlango wa kwanza wa kituo,woote mnakimbilia kule,mkikaribia anatoa basi alafu anasimama mlango wa kati.,,mkikimbilia tena mlango wa kati,,, anatoa gari anasimama mlango wa mbele,,mkikaribia mlango wa mbele anatoa gari mazima,anaenda tena kuwachezesha kituo kinachofuata.

mwenyewe anafurahi anawafanya watanzania kama vile midoli.
 
Back
Top Bottom