Elias Msuya
Senior Member
- Dec 23, 2011
- 173
- 671
Chama cha Madereva wa Malori Tanzania, (TATAMATA) kimetoa siku mbili kwa Serikali kushirikiana nao kumtafuta aliyekuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Godlove Materu , la sivyo madereva wote wa chama hicho hawatafanya kazi kuanzia Februari 10, 2026 mpaka apatikane.
Kwa mujibu wa viongozi wa chama hicho, Februari 5, Materu alichukuliwa na watu wasiojulikana waliofika dukani kwake Tunduma Mkoani Songwe wakiwa na gari jeupe aina ya Toyota Land Cruiser.
Wakizungumza na waandishi wa habari leo Februari 8, 2026 jijini Dar es Salaam, viongoi wa chama hicho, wamesema kuchukuliwa kwa Materu ni mwendelezo wa manyanyaso kwao, wakiiomba Serikali isikilize kilio chao.
Baada ya mkutano wa madereva hao na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Songwe alitoa taarifa akikiri jeshi hilo kumshikilia Godlove Materu.
Makamu Mwenyekiti wa TATAMATA, Yohana Mwanyaga
Wakili Aloyce Komba
Katibu wa kamati ya Madereva, Mbuka Mwakitwile
Polisi wawajibu