Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

mkuu. n00b
heshima kwako kwa kuutendea haki huu uzi.ni ombi langu kwako kuwa sasa umefika wakati tuweke tena uzi. mwningine stiky unaohusu biashara ya pembe za ndovu
 
Last edited by a moderator:
wanaokamatwa wanatumwa tu kama unavyoweza kumbebesha punda mzigo, unfortunately wanabeba pia "risks" zinazoambatana na kukamatwa wakati wenye mzigo wametulia kwenye kiyoyozi wakiangalia luninga!! tamaa ya pesa za haraka - Big Results Now
 
Ukipita katika mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam na katika miji mingine mikuwa utawakuta vijana na baadhi ya watu wazima wamekaa katika makundi wakivuta bangi na kutumia dawa nyingine ya kulevya bila wasiwasi wowote. Hili hutokea zaidi nyakati za jioni na usiku lakini pia sio nadra kukuta makundi ya namna hii yamechanua nyakati za asubuhi au mchana. Ifikapo jioni hewa ya vichochoro na vijiwe vya wavuta bangi hujaa harufu ya bangi. Watoto wanaocheza katika hii mitaa pamoja na wapita njia wengine hujikuta wakivutishwa bangi kwa lazima bila ridhaa yao kwani hewa yote inakuwa imejaa moshi na harufu kali itokanayo na moshi wa bangi.

Suala la uvutaji bangi kwa vijana wa rika mbalimbali limekuwa kama fasheni. Vijana wa kada zote—waliopo shuleni na mitaani—wamejikuta wakitumbukia kwenye ulevi huu wenye madhara makubwa kiafya. Na kibaya zaidi jamii nayo imeacha vitendo hivi viendelee huku madhara yake yakiwa yanafahamika hata kwa viongozi wa mitaa wanakoketi hawa wahalifu.

Jitihada za serikali kupambana na dawa za kulevya zinaonekana kama zimeshindwa kuzaa matunda. Pamoja na juhudi zote za kuzuia uingizaji wa dawa ya kulevya na ulimaji wa bangi, mirungi na dawa nyingine kama hizo, bado tatizo limezidi kuwa kubwa na kila kukicha vijana wetu hugeuka kuwa machizi, hivyo kupunguza nguvu kazi, kuchochea uhalifu na kupunguza uzalishaji mali. Na idadi ya walemavu wa akili watokanao na utumiaji wa dawa za kulevya inazidi kuongezeka kila siku. Sio rahisi kukatiza mitaa miwili bila kukutana na muokota makopo. Idadi hii kwa kweli inatisha. Serikali isipofanya jambo kuzuia uingizaji na utumiaji wa dawa za kulevya, kizazi cha vijana kitaangamia.

Katika jitihada za kukabiliana na tatizo hili suala la uadilifu miongoni mwa watumishi katika jeshi la polisi sharti lizingatiwe. Ni bahati mbaya kwamba baadhi ya askari polisi wamefanya vita dhidi ya bangi na dawa nyingine za kulevya kama kitega uchumi. Ni mara nyingi tumeshuhudia polisi wakiwakamata wauzaji na watumiaji wa dawa za kulevya na kuishia kuwaachia kwa kukubali kupokea rushwa uchwara kutoka kwa wahalifu hawa. Nadhani ingekuwa rahisi sana kuwapata wauzaji wakubwa wa madawa ya kulevya kwa kuwahoji wauzaji wadogo na watumiaji ni wapi wanakozipata hizi dawa. Halafu kuanzia hapo tunaweza kuwapata waagizaji mapapa na nyangumi wa dawa za kulevya. Kwa bahati mbaya, hali haiko hivyo. Ndio maana suala zima la upambanaji dhidi biashara ya dawa za kulevya wakati mwingine linaonekana kama mchezo wa kuigiza au ‘kombolela’ ya watoto wadogo.

Tuhuma kwa wanasiasa na watu wenye uwezo mkubwa kiuchumi kuwa nyuma ya biashara hii, nalo haliwezi kupuuzwa. Kama isingekuwa hivyo, basi vita dhidi ya dawa za kulevya ingeweza kupata mafanikio haraka. Lakini kwa kuwa tunaowategemea kuchukua hatua ndio hao wamo kwenye biashara hii, itakuwa ni ndoto kufanikiwa katika mapambano haya. Nakumbuka kuna mwanasiasa mmoja hivi karibuni alihusika kwenye ubakaji na amekuwa akimtishia mbakwaji kwamba hawezi kumfanya chochote kwa kuwa watoto wao (wanasiasa) ndio wauzaji wakubwa wa dawa ya kulevya na hakuna wa kuwakamata! Kwa hali hii itakuwa ni ndoto kufanikiwa kutokomeza au kupunguza tatizo la dawa za kulevya katika nchi hii ya Tanzania.

Hivyo basi, ni juu ya kila mzazi/mlezi kuhakikisha kwamba anawalea wanaye katika maadili yanayofaa na kuwakinga wasitumbukie kwenye utumiaji wa madawa ya kulevya kwani kuacha suala hili kwa wanasiasa pekee yao ni sawa na kumuachia kima aamue kesi inayomhusu ngedere. Wazazi wanatakiwa kuchunguza na kudhibiti mienendo ya watoto wao na kuhakikisha kwamba hawajiungi kwenye magenge ya wavuta bangi. Kufanya hivyo kutasaidia kupunguza idadi ya vijana wanaoharibiwa akili kwa bangi na madawa mengine ya kulevya. Kamwe tusiitegemee serikali katika vita hii kwani serikali ni siko la kufa.
 
157fs837411.gif
 
Back
Top Bottom