Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!

Good Jerry. Anasema kama kuna mtu ambaye ana ndugu yake aliyeathiriwa na dawa za kulevya hawezi kupinga vita hii kwa namna yoyote. Kumbe mdogo wake anavuta ndo maana inamuuma.

Anaongeza kwamba kuna vijana Yanga wameharibiwa na madawa ikiashiria vijana wengi kuharibika kama nguvu ya taifa
 
Good Jerry. Anasema kama kuna mtu ambaye ana ndugu yake aliyeathiriwa na dawa za kulevya hawezi kupinga vita hii kwa namna yoyote. Kumbe mdogo wake anavuta ndo maana inamuuma.

Anaongeza kwamba kuna vijana Yanga wameharibiwa na madawa ikiashiria vijana wengi kuharibika kama nguvu ya taifa
Do ........mwenyekiti wa club.
 
Acheni pumba zenu msijifanye nyie ndio mnajua kila kitu wengine wote hawafai, kazi yenu ni kutetea uhalifu tu katika Nchi hii.
Nashangaa sana umeniquote mimi lakini unazungumzia "msijifanye"..

Haya wewe umemsikiliza huyo jerry kuna kitu cha msingi ameongea zaidi ya kujikombakomba tu??

Hivi kuna sheria gani inampa mamlaka mkuu wa mkoa ya kuwa "rais wa mkoa"..ni sheria ipi inampa mamlaka mkuu wa mkoa ya kumfukuza mwanamchi katika mkoa anaoongaza?..hayo yote ameyazungumza huyo Jerry!

Na sijui umetumia akili gani kusema "tunatetea uhalifu"..sijajua bado!
 
Hivi kuna watu na akili zao timamu wanamsikiliza huyu mpumbavu? Hajui ni kina nani wamemuokoa asifungwe kwenye ile kesi yake ya kuomba rushwa na kutembea na pingu.
 
Duu muda Wangu umepotea bure mada hii channel ten . Saa hili moja ningekuwa nimelala ningekuwa na faida kubwa sana kiafya, siku nyingine wasirudie kuleta mawazo mepesi kwenye mambo mazito tunalipia umeme, cable na ving'amuzi wenyewe wanaleta mzaha
 
Makonda namhurumia sana ningekuwa mimi ningejiuzulu urc
nikarudi zangu kijijini kulima mihogo haiwezekekani unapambana kuwasaidia watu
wasiathirike na madawa ya kulevya hao hao tena wanakupiga vita Ushauri wangu kwa Makonda
fanya mambo mengine suala la madawa ya kulevya acha vijana waendelee kuharibika tukija kushituka tuwe kama Mexico hapo ndiyo kwa unafiki na uzandiki wa watanzania tutaanza kukumbuka Makonda yaache yafe na maunga yao taifa hili wapumbavu wako wengi sana kuanzia wabunge
Kwalweli anayebeza zoezi hili hayajamfika, au kuona mtu wake wa karibu anavyoteseka na hivi vitu. Ndiyo maana Nchi kama China ilichofanya ni kuachana kwanza na sera za haki za Binadamu na kuamua kuwanyonga hadharani wote wanaojihusisha na mihadarati lakini huku watu wanaitwa kiungwana ili wakae round table warekebishe mambo, lakini reaction zao zinavuka viwango wanapiga mayowe na kuwahusisha na wapambe wao ili waonekane wameonewa. kwakweli haya mambo yanatia hasira sana! Lakini makonda aliisha liona hilo mwanzoni ndiyo maana alianza kwa kutoa angalizo na kuahidi kwamba amejitolea kufa na kupona.
 
Vita hii ni ndogo kwa mtazamo wa kiroho ila nikubwa kwa macho ya kawaida na mitazamo ambayo si chanya bali ni hasi katika jamii zetu kama mapambano yangekuwa ya kwetu sote tungeweza kwani katika hali ya umoja kila kitu kinawezekana tukiamua tunaweza .Umeshajiuliza wangapi wanaandika historia mpya katika maisha yao wangapi wanavunja rekodi zilizoweza kuwekwa na wengne kwanini mimi au kwanini wewe ukate tamaa kwanini wewe ushindwe kufanya kitu sababu flan kashindwa kujiweka wa mwisho ni ufinyu wa mawazo na ni umasikini .Nashangaa kuona mpaka viongozi wanakuwa mstari wa mbele kutete na kukatisha tamaa serikali yao wenye kwa kutoa sababu mbalimbali zisizo na msingi kwa kutadhama nchi zingne mnatuaminisha sisi kitu ganiatuwezi sababu ya flan kuzidiwa na mtu darasana aikufanyi wewe kujiaminisha yeye ndiye milele atakiwa anakuongoza tu au yeye ndiye mshindi wa kila siku ukilambana utaweza inanipa mashaka sana .

Tuanze kwa upande wa serikali nafurahi kuona mapambano haya yakifanyika ila tunapaswa kutambua mapambano haya ni ya taifa zima yani yanaanza nyumbani kwako mtaani wilayani mkoani mpaka taifa zima si kwa dar pakee .Kama kweli tumeamua kipambana tufunge mkanda tuingie katika mapambano juu ya hili ila na maswali machache ni kweli tulikaa na kujidhatiti kupambana ninachomanisha tumejipanga kwa hili kukimaliza au tutaishia njiani ? Me nilipendekeza zingeundwa sheria mbalimbali ambazo ni ngumu juu ya madawa yakulevya ila si kwa sasa zilizopo ambazo naona bado zinamlinda muhuzaji na mtumiaji pia kwann nasema zinamlinda kwa sababu sio sheria kali kama nchi zingne zilivyojipanga kupambana kwa swala hili je tumefanya hivyo nilishawai kisoma shairi moja la mwizi lipo katika kitabu cha mashairi chungu tamu utaelewa nini ninachomanisha kwani ukitadhama hilo utaona matabaka mbalimbali yanaguswa kwa kuwaficha na kuwalinda wahalifu.Je mmejipanga kweli kiusalama kuwalinda wanaotoa tarifa kuwalinda mashaidi nimeona kesi nyingi zinaishia njiani sababu ya ushaidi kuwa hafifu tutizame kwanza swala hilo sio ndo tuache mapambano hapana ila tuangalie namna gani linafanyika vilevile Naona kabla atujaenda uko tungeanza na mfumo mzima wa sheria kwanza na amini serikali inawanasheria wazuri tu na washauri wazuri tu kama mfumo wa kisheria na maahakama ukifanya mabadiliko yanawezekana yote tukitaka tunaweza nadhani unatambua nchi ambazo zina sheria kali dhidi ya madawa ya kulevya imekuwa ni kama dhahabu vile upatikanaji wake ndo uingizwaji wake wamepunguza kwa kiasi kikubwa sana .Na imani na serikali yangu na ninamini tunawezs tuna mihimili mitatu kama sijakosea mihimili hiyo yote ni yakinifu kabisa inawezekana kutunga sheria kali na ambayo ikatekelezeka kwa uwadilifu kabisa .

Nikajiukiza serikali ni wakina nani nikakumbuka kumbe hata mimi ni serikali tambua serikali ni mimi na wewe tukiungana tunaweza. Nakuja pata mashaka makubwa juu ya taifa hili lina watu wa aina gani inafika kipindi tunatetea hata watumiwa bila aibu wanaungana pamoja na kupaza sauti kabisa kutetea na kutuludisha nyuma .barozi wa swala hili si msani pekee hata wewe unaweza ukianzia nyumbani kwako mpka mtaani ndoto nyingi za watu zimepotea wazazi wengi mategemeo ya watoto wao yamepotea baada mtoto kuja kuwa msaada kwa mzazi anakuja kuwa mzigo madawa ya kulevya ni hatari sana nipongeze wale wote wanaopambana juu ya swala hili nikianzia kwa MH.Rais mpka mimi mwenyew mtu wa chini kabisa tukisema Dar safi si dar ya kupanda miti au kuweka mazingira safi hata watu wawe safi kiakili kuleta maendeleo katika taifa hili ningeomba vita hii iwe ya taifa nzima msiba sikia kwa mwenzio tu subiri wako ukufike kama utapiga kelele kushangilia vitu visivyokuwa na msingi Tukiamua tunaweza mapambano dhidi ya madawa ya kulevya .

Wanasema vita ni kubwa kutokana na hali halisi ambayo ukiamua kipambana utakuwa umejumuisha mihimili mabalimbali na watu wengi mashuhuri . umaskini wa fikra , fedha na mawazo unawafanya wa amini atuwezi sababu ya flan tangu mdogo niliaminishwa sheria ni msumeno unakata kote kote sasa wasinifanye nione sheria ni kiwembe tena chenye kutu au butu. Mapambana dhidi ya madawa yanawezekana kutokomezwa either kupunguza kwa kiasi kikubwa au kutokomeza kabisa.
 
Hivi ufanisi wa upambanaji dhidi ya malaria ulikuwa kwa kiwango gani vile..!?
Maana haka ka-nchi bhana..
 
Kwalweli anayebeza zoezi hili hayajamfika, au kuona mtu wake wa karibu anavyoteseka na hivi vitu. Ndiyo maana Nchi kama China ilichofanya ni kuachana kwanza na sera za haki za Binadamu na kuamua kuwanyonga hadharani wote wanaojihusisha na mihadarati lakini huku watu wanaitwa kiungwana ili wakae round table warekebishe mambo, lakini reaction zao zinavuka viwango wanapiga mayowe na kuwahusisha na wapambe wao ili waonekane wameonewa. kwakweli haya mambo yanatia hasira sana! Lakini makonda aliisha liona hilo mwanzoni ndiyo maana alianza kwa kutoa angalizo na kuahidi kwamba amejitolea kufa na kupona.
Hawa wanafiki nadhani kizazi chao kipo kila mara nakumbuka hata wakati wa Taifa stars chini ya maximo walikuwa wanapiga kelele maximo hafai aiache timu leo hii tumebaki na pakacha letu wako kimyaa! Wameridhika
Wanampigia makonda kelele ataachana na hii kampeni tutarudi kule kule. Na list ya kikwete, na list ya kitwanga mezani ikipigwa vumbi.
Ingewezekana kizazi hiki cha wanafiki hawa ni kukiondoa na kukifuta chote. Wanakwamisha sana maendeleo ya Nchi hii.
Too much siasa kwenye kila kitu.
 
Malaria inauwa kuliko ngada,na imetushinda kama mbu tu katushinda haya hao makingpin?dawa ya dawa ni kuhalalisha baadhi ya dawa.
 
Kwanza nianze kwa kukupongeza kwa dhati kabisa RC. Makonda.
Wewe ni shujaa wa leo na kesho. Umeruka dhambi ya unafiki na kuwa mkweli.
Vitabu vya dini vinakataza sana unafiki. Na wewe umeonekana ama kwa hakika hupendi unafiki.

Umeweka mbele maslahi ya watanzania na Umeonyesha utiifu wako kwa nchi yako na kwa Rais wetu ambaye ama kwa hakika amekua akikerwa na uovu unaofanywa ndani ya Taifa hili.

Ama kwa hakika kila mmoja ameona nguvu ya wauza madawa waliyonayo kila kona na idara ya nchi hii. Siamini kwamba bunge liliamua kuacha shughuli zake na kuamua kujadili kauli yako ya kupingana na Mbunge mmoja tu bila nguvu kutoka mahali pengine.

Pia tumeona jinsi wabunge wetu walivyoungana kudhoofisha juhudi zako za kupambana na uuzwaji wa dawa za kulevya nchini pamoja na kwamba wamejipambanua kuwa wanapinga mbinu inayotumika.
Kwa mwenye akili anajua wazi kuwa kupinga mbinu uliyotumia ni kupinga vita yenyewe.

Vita ni vita tu : Hakuna vita isiyo na madhara. Huwezi kuanzisha vita halafu unaogopa madhara ya vita hiyo. Hapo una maanisha vita iachwe. Hao wanaopinga madhara ya kuwataja watumiaji eti ni kuwadhalilisha wanasahau kuwa ndio hao hao siku zote polisi inapokamata kimya kimya wamekua wakipiga kelele kuwa wanawaonea na kukamata watu ovyo bila sababu na kuwabambikia bangi /madawa ya kulevya.

Polisi wakiwaachia hao hao wanalalamika kuwa polisi wanakula rushwa na kuwaachia watuhumiwa wa madawa ya kulevya. Leo hii imani yao kwa jeshi la polisi inatoka wapi kama sio mbinu ya kupinga na kukwamisha zoezi hili la kupambana na hii biashara haramu?

Kwa nini Bunge halikuunda tume au kamati maalum ili kufanya uchunguzi wa kina kwa waliotuhumiwa na ikiwezekana kuchunguza mali za wale askari waliohusishwa na kuwasaidia wauza unga kukwepa mkono wa dola na ikiwezekana kupitia vielelezo alivyonavyo Mh. Makonda ili kubaini ukweli au uongo wa Makonda ndipo watoe mapendekezo?

Ukiangalia kwa umakini maazimio ya Bunge yanawabeba zaidi waliotuhumiwa kuliko RC Makonda ambaye anaonekana wazi kuwa ana taarifa za kutosha juu ya hao aliowatuhumu.

Ukiona mtu anasimama adharani kudili na magenge ya watumiaji wa madawa ya kulevya ujue huyo mtu amejitoa muhanga.
Naamini RC Makonda umejitoa muhanga kuokoa watoto wetu na kizazi kijacho.

RC Makonda Historia itakusoma kama shujaa na wanaokaa na kujifanya kuwa wanakutafutia utaratibu wa kisiasa wa kupambana na madawa ya kulevya watahukumiwa na majina yao hayatakumbukwa kamwe.

Hivi kama usingejitokeza adharani na kusema wazi na kuwataja kwa uwazi kuwa kuna askari wanaoshirikiana na wauza unga na wanatoa siri na kuvuruga zoezi la kukamata hao wauza unga ni nani angesema.?
Je , hizo tuhumu hao wapinzani wako ndio mara ya kwanza kuzisikia?

Nani ambaye hajui kuwa kuna ubabaishaji na kuharibiwa kwa vielelezo mara kwa mara na madawa yanageuzwa kuwa chumvi? Matokeo yake wakamataji wanaonekana ni wajinga na hawajui wajibu wao?

Je hao wapinzani wako siku zote walikua wapi kuhakikisha wanatunga sheria bora za kuwapa mazingira bora zaidi wakamataji na namna bora zaidi ya kuhifadhi na kuyagundua madawa ya kulevya badala ya kutegemea ofisi moja tu ya mkemia mkuu wa serikali peke yake ambayo haina maabara mikoani?

Hivi nani hajui kuwa vita dhidi ya madawa ya kulevya inahitaji utashi wa kisiasa zaidi kuliko sheria na vyombo vya dola peke yake? Ni askari gani ataweza kwenda kumkamata bilionea na kumweka ndani kwa madawa ya kulevya ?Na ni bilionea gani atakubali kuwekwa ndani kwa tuhuma ya madawa ya kulevya bila kutoa mabilioni na kuwahonga wote waliomkamata kisha kuwa yeye ndio rafiki yao na mtu muhimu kwao?

Ni nani atakayeweza kukataa hongo ya bilioni moja ili amwachie mtuhumiwa wa madawa kama hakuna nguvu kubwa ya kisiasa inayotamka kwa wazi kuwa sasa basi? Akikataa kupokea hiyo rushwa ujue anakua ni adui namba moja na hakuna mtu wa kumtetea! Akikataa mkamataji basi atachukua mpelelezi! Akikataa mpelelezi basi atachukua kule kwa mkemia na Madawa yatageuka chumvi.

Ni lazima wanasiasa na wabunge wote waungane na Jeshi la polisi kwa wazi ili wauzaji nao waone hawana wa kumtegemea kwani kila jicho liko nyuma yao.
Hata magaidi huwa yanatajwa hadharani na kwa wazi ili kila mtu ayatafute na kuyakamata. Usipowataja wauzaji na watumiaji basi watazagaa mitaani na kupewa heshima kumbe ndio wanaotumaliza.

Kwa hili RC Makonda usirudi nyuma kamwe.

MAPENDEKEZO YANGU KWAKO SHUJAA WA SASA NA SIKU ZIJAZO RC MAKONDA:
(1) Muombe Mh. Rais aunde tume maalum ili kuwachunguza kwa kina wale wote waliotajwa ili kuweka uwazi zaidi na hatimaye wajipime wenyewe kama wanaacha au wanaishia kwenye mikono ya sheria.

>Tume hiyo iundwe na watu makini na waadilifu sana wakiwemo Majaji, viongozi wa dini ,askari waadilifu na wastaafu kama Akina Nzowa , Tosi,Mwamunyange,shehe mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Alhaji Mussa, watu wa haki za binadamu,baadhi ya waandishi mashuhuri, wafanyabiashara waadilifu, madaktari waadilifu kwenye upande wa phamasia, madaktari mahiri kutoka ndani na nje ya nchi na wataalam wa madawa ya kulevya kutoka ndani na nje ya nchi.

(2) Wachaguliwe madaktari wa serikali na wa binafsi na wakemia kutoka ndani na nje ya nchi ili kila aliyetuhumiwa achukuliwe DAMU na kuipelekwa kwenye maabara za ndani na za nje ili kulinganisha matokeo ya vipimo vya damu husika.

Hatutaki mtu aonewe wala atafute huruma kwa yale aliyotenda. Mbinu za kisayansi za kuwapima damu kama wanavyopimwa wachezaji huko nje zitumike. Ili tuwajue

(3) Tangaza dau na zawadi kwa mtu atakayefanikisha kukamatwa kwa madawa ya kulevya kuanzia sasa.

(4) Hakikisha unatoa ushirikiano kwa vyombo vingine vya sheria akiwemo pia waziri wa Sheria ili sheria ya mihadarati ifanyiwe marekebisho ili watumiaji wamadawa wabainike na kuadhibiwa pia kwa kupitia vipimo vya damu ili kuondoa dhana ya kubambikiwa kesi.
Iwe kama ilivyo kwa madereva ambao wanapimwa kupitia pumzi zao au vipimo vya damu na wanapewa adhabu.

(5) Hakikisha ndani ya mkoa wako maabara za mkemia mkuu wa serikali zinafunguliwa kwenye Hospitali za Temeke ,Mwananyamala na Mnazi mmoja ili kupunguza urasimu uliopo kwenye ofisi moja tu ya mkemia jambo linalochelewesha na kuharibu upelelezi wa makosa ya mihadarati ikiwemo bangi.


Hii ni vita takatifu uliyoianzisha na :-
Mungu yupo nawe.
Mh. Rais yupo nawe.
IGP yupo nawe.
Kamanda Siro yupo nawe.
Waziri wa mambo ya ndani yupo nawe.

Usirudi nyuma mpaka wajisalimishe wote.
 
Mungu yupo nawe?
Hii ndiyo sentensi wengi huwa wanatumia daily kujipa moyo. mungu yupi huyo? Yule jamaa hajielewi, anakurupuka kuitaita watu tu bila mpangilio, ni ka mtoto mdogo mpenda misifa,.

Bunge kusimama against Makonda au watu kama Yusuph na Mbowe haimaanishi wanauza, wanalinda heshima yao kutokana na ujinga anaoufanya huyu jamaa. Anayehisi huyu jamaa anaweza pambana na wauza madawa anajidanganya, sio kwa IQ ile, angekua na nia kweli tungejua, sio kukaa anakurupuka kuitaita watu maarufu kwenye TV, tena majina yameandikwa kwa kalamu kwenye karatasi ovyo tu anagawa watu watoe copy. Kila kitu kinaenda ovyo ovyo tu. Waafrika kazi ipo, tatizo letu kubwa ni kua na idadi kubwa ya vilaza alafu wengi wao wanashika nafasi za juu sana, wanapewa support na watu wengi mno kwa kuwa wenyewe nao team moja.
 
Ni tanzania pekee mkuu wa mkoa anaanzisha kampeni ya vita kubwa kama hiyo halafu tunaita ya kitaifa!!

Ni tanzania pekee tunaanzisha vita ya madawa ya kulevya halafu kamishna wa kitengo cha madawa ya kulevya anateuliwa baadae!
 
Back
Top Bottom