Madawa ya Kulevya na aibu ya Tanzania - Yatosha sasa!


ITOSHE KUSEMA TU KWAMBA SAA ZA UJINGA ZIMEKWISHA, NARUDIA TENA NA NITASEMA TENA, HAKUNA PESA YOYOTE KWENYE BIASHARA YA MADAWA YA KULEVYA, MADAWA YA KULEVYA NI KAMA BANGE NA GONGO. WAZUNGU WALITUAMINISHA KWENYE FILAMU KWAMBA MADAWA YA KULEVYA YANA PESA, NI UONGO NA UZUSHI. MADAWA YA KULEVYA NI KIFO!! MADAWA YA KULEVYA YANAUA HARAKA SANA NA KILA ANAYE TUMIA BASI TAIFA LIMEMPOTEZA.
 
Labda nisahihishe kidogo. Serikali haijawahi kuteka mtu hata mmoja na haifikirii hilo. Inachofanya ni kuwalinda
Nafkili inategemea kutekwa au kulindwa inatokea kulingana na mazingira na waTanzania hupenda kujadili mambo ambayo hayana msingi. vitu vya maendeleo hampendi kujadili sasa watu wanatumia neno kutekwa ktk mijadala yao hawawezi kutumia neno kuchukuliwa na kuhifadhiwa kwa mahojiano. kwa hiyo jibu lake hapo ni inategemea
 
Kalama Masuod Suleiman au al maaruf kama "Kalapina" na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ni watu wanaotajwa kupambana kwa namna moja ama nyingine na matumizi ya madawa ya kulevya kwenye jamii ya watu wa Dar es salaam.

Kalapina ambaye anaendesha kampeni inayojulikana kwa jina la "Harakati" amekuwa akizunguka mitaani hasa maeneo ambayo yana watumiaji wengi wa madawa ya kulevya akitoa elimu pamoja na kuwakusanya watumiaji hao na kuwapeleka kwenye nyumba za kupunguza uraibu (Sober House) watumiaji hao. Pia hujishughulisha na miradi ya waliokuwa watumiaji wa madawa ya kulevya.

Makonda naye ametokea kuwa maarufu kwa kutaja majina ya washukiwa wa matumizi ya madawa ya kulevya pamoja na wauzaji. Pamoja na mpango wake kukutwa na vikwazo vingi sana, lakini Makonda amebakia kama mtu aliyechagiza kwa upya vita hiyo dhidi ya madawa ya kulevya. Ingawa Kampeni yake iligubikwa na sintofahamu nyingi, lakini naye ni mmoja ya watu walio kwenye orodha ya watu walionesha kupambana na biashara ya madawa ya kulevya.

Hawa watu wawili wanalinganishika linapokuja suala la kupambana na biashara ya madawa ya kulevya?
 
Baada ya muda mrefu sasa Taifa limejipanga na kutengeneza commission maalum ya kupambana na dawa za kulevya.
Sasa tu jiulize je kamisheni hii inaundwa kimapambano au kijamaa na kisiasa? Au hatujitambui?
Mtizamo wangu baada ya uundwaji wa kamisheni uteuzi wa KAMISHNA MKUU. kilichotakiwa kufuatia ni kutangazwa kwa nafasi za kazi WATANZANIA WAOMBE NAFASI watoe mchango wao kwa taifa.
Hata kama si ajira mpya lkn WATANZANIA waombe wakitokea ktk ajira zingine. Lkn kwa muundo wa sasa bado ni uteuzi wa kutazamana sura ,ujamaa zaidi hivyo TIJA ni sehemu Mdogo saana kupatikana.
Tumetoka kwenye tabu ya kupambana na dawa hizi kimazoea huku tukiwa mabingwa wa kuelezea mbinu za udhibiti wa dawa hizo na mafanikio ya ukamataji, lkn idadi ya vijana wanaotumia dawa hizo ikiwa inaongezeka mwaka hata mwaka.
Rai yangu kwa wahusika hatujachelewa tuache kupeana mapande ya ajira tufungue milango watu waombe kufanya kazi wachujwe kwa sifa stahili. Kuliko yule ni rafiki yangu/jamaa yangu nk
 

SERIKALI WANAJISUMBUA NN WAKATI Mh.JK ALIPEWA ORODHA HAPO MAGOGONI MJENGONI. WASITUONE MAZOBA WAKUENDELEA KUJADL MADAWA, WAKIPEWA MAJINA YA JAMAA ZAO WANACHOMA LIST.
 
Kwa nini kutumia Madawa ya kulevya ni kosa na unashitakiwa? Binafsi ningependekeza tuwekeze nguvu kwenye wauzaji na wasambazaji na siyo watuamiaji, kumkamata mtumuaji ni kumuonea tu, tunachopaswa kufanya ni kumsaidia ili asiweze kuendelea kutumia Madawa ya kulevya na siyo kumuweka Jela, huu ni ujinga kwani hakutatui tatizo, na kama tulikuwa tunatafuta ushahidi wote waliokamatwa kwa kutumia Madawa ya kulevya hapo mwanzo wakiachiwa waaendelea kutumia, ...
 

Mkuu hapo ndipo ulaji ulipo!Nilienda iringa,kuna kijana alikutwa na bangi msokoto mmoja!Nilikuta kashikiliwa kituo cha polisi ana wiki 2,jamaa hata mahakamani hawawafikisha watuhumiwa wa kutumia bangi!Walimshikilia mpaka Mama yake alipotoa mil 1.5 ndio akaachiwa!Mwanzoni alitoa laki 2 wakakataa,akaongeza mpaka laki 5 bado wakakataa!Wakampiga mil 2,mama akawashusha mpaka mil 1.5!
Yaani huu ni ulaji kwa polisi,wakiishiwa tu hela wanapiga doria na kujaza watu mahabusu!!!Kinachofuata ni pesa!
 
Kwa hakika madawa ya kulevya ni adhali kubwa sanaaaaa na tatizo limechangia kuua ndoto za vijana wengi katika nchi yetu ya Tanzania ikiwemo Africa nzima.Juhudi hizi za kudili na wauaji hawa ziendelee kabisa.

Geofrey Julius
Africa's youth first network
www.africasyouthfirstnetwork.org
 
nawe unaeamini serikali inapambana na wauza dawa za kulevya ni jinga la majinga.!
hata yule mange nae hawajui..anapewa info na zote zinahusu kambale..nyangumi hawajui.na ili uwaumbue tu hawa watu must uwe mtu wa karibu na system na pia upate ushahidi.
refer to amina chifupa..alipata ubunge na kuwa nao close...akatangaza vita walampoteza kwa kifo cha ghafla!
kuna alietangaza nia ya dhati kupamnana na dawa za kulevya baada ya amina?

leo mkawa mnamshangilia makonda

bila kujua huyu kijana no kibaraka wa walewale
makonda alipewa go on na mzee juma iwe kama kiki..manyangumi wakakutana mkuu wa kaya akatoa wasiwasi mpo salama..msihofu!
wakaanda list ndeefu ya kambale na dagaa ikiwemo hawa mapunda na mateja wanaomwaga udenda mitaani..mnashangilia wee!!
eti vita ya kupambana na madawa unakamata mateja...eti kila mzaz ataekutwa na kijana mtumiaji sheria i juu yake

hata lissu aliongea wee nyangumi mbona wanaachwa..
hivi leo ukishamiri ushirikina watu wanalogwa wanakufa wengine wako hoi kitandani..utawakamata hao waliologwa ili kukomesha uchawi eenh? halafu mnashangilia wee

sasa sikilizeni:
biashara ya dawa za kulevya ilianza tangu enzi za nyerere...na alieianzisha ni kiongozi mkubwa tu ndani ya serikali baada ya kuona inalipa
baadae wengine wakafuatia.
vigogo na watoto wao wanahusika mpaka sasa hivi biashara inaenda.
wana njia mpya..
ukimuona mzee juma shujaa kwa kuweza kuthibiti mitambo pale airport yote hii ni kwa kutafuta sifa kwa wananchi..na wanaonasa pale ni kambale na dagaa..nyangumi wana njia yao mpya na wote wanajua
wanatumia meli za mizigo kubwaa..
meli zikikaribia kutia nanga mzigo unashushwa...mtu mzito akipiiga simu na kutoa oda wote wanaufyata
mzigo unaingizwa kwenye nitumbwi ya uvuvi mpaka ferry
kuna sehemu haifikiw sana na watu imepaki na kuhifadhi mitumbwi chakavu..huko wanashusha mzigo safar inaendelea..
biashara ipo kama kawaida na unga unapatikana kama kawaida..
mnachezewa akili..

roma aliropoka ukweli kupitia post yake mtandaoni yule bwana mwenye makalio makubwa ka anachambia hamira akaamua kumnyamazisha kwa ubaya..
alikua namharibia sinema lake..

wasanii kibao wanawajua hawa nyangumi.
wametumika sana sabb ya tamaa zao
but sharti lao kuu ni moja..
ukimtaja anakupoteza mazima.


USIKUBALI KUCHEZEWA AKILI..

mi naenda kulala..
 
Ile senema ya kuwaita kituoni na kuwakojolesha ilikuwa maalum kwa watu maalum tu. Wengine kuwapunguza makali yao na wengine kuwaondolea upupo kwa matairi ili gari litulie.
Si waona wengine hadi sasa bado wananyonywa jasho lao. Kodi 12.8 billion wadhani mchezo. Zaidi ya bajeti ya wizara! Kweli akiamua kukuchezea cheusi chekundu, hufurukuti
 
leo walokamatwa wako wapi??
kesi zao zinaendelea?
usiulize
wako busy na kipisi cha bangi alivhokutwa nacho wema..
ile list ya watu zaidi ya mia mbili iko wapi?
wako wapi wale watu?
 
Vita ya Madawa ya kulevya Tanzania imeweka record moja matata maana ni vita vya muda mfupi sana na watu wa madawa wamewini... Mashamba ya Bangi yamechomwa sana ila bangi itaendelea tu...

Huko Philippines raisi Durerte hawamtaki tena kashindwa kumuua mwanae Maandamano na fujo kwa wafiwa hali ya inchi yao imekuwa tete.. na waasi wamechamamaa.

Hivi yule James Sianga yupo wapi vile? hivi ni bangi tu pekee ndio inachimwa hadharani tena mbichi lakini heroin mandrax n.k inachomwa mafichoni?
 
Umeandika maelezo mengi na hasa ukijikita kwenye kulaumu huku ukionesha hakuna lililofanyika au lililofanyika ni dogo

Ajabu umeshindwa hata kuwataja hao nyangumi iwapo kweli unawajua na angalau kuweka maelezo yao kwa kuanzia. Kwanini tuamini maelezo yako? Nadhani ingependeza ungekuja na uzi unaoonesha ushiriki wa hao unaowahita nyangumi na jinsi ambavyo wameachwa bila kuguswa.

Vinginevyo itaonekana ni majungu ya kutofurahishwa na kazi inayofanyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…